Mali zenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 za Wakili Median Mwale zataifishwa rasmi na Serikali

Unaiba hela unajenga majumba na kununua viwanja?

Angenunua hisa huko Marekani au akazifiche Cayman au New Jersey.
Hapo ndipo utakapogundua kwamba Chenge ana akili kuwazidi wanasheria wenzake wote....nyoka mwenye makengeza
 
1089206


MKURUGENZI wa Mashitaka (DDP), Biswago Mganga amesema serikali imetaisha rasmi mali za Wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 kutokana na makosa ya kutakatisha fedha haramu.

Mganga amesema, mali hizo zilizotokana na zao la utakatishaji fedha haramu baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumtia hatiani na kuamuru mali hizo zitaishwe na serikali. Akizungumzia na waandishi wa habari jana mjini Arusha wakati wa makabidhiano kati ya osi ya DPP na Hazina, Mganga alitaja mali hizo kuwa ni magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.

Mali zingine zilizotaishwa ni nyumba mbili ikiwemo iliyopo Plot Namba 261 Block C Njiro na nyumba nyingine iliyopo Plot Namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.

Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kutaisha mali hizo na kwamba Aprili 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaisha rasmi na kuwa mali ya serikali. “Kwa mujibu wa sheria mali zinapotaishwa kuwa mali ya serikali zinakuwa chini ya Katibu Mkuu Hazina” alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali Hazina, Benezeth Rutta alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa Wizara ya Fedha na zinapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa. “Mali hizi baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada” alisema Rutta.

Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Selemani Nyakulinga amesema mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dola za Marekani milioni 17.2. Alisema fedha hizo zilikuwa zinaibwa kutoka mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kusaidia kutibu Ukimwi nchini Tanzania zikitoka Hazina ya nchi ya Marekani.

Amesema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni raia wa Kenya, wakishirikiana na Watanzania akiwemo Wakili Mwale . AMesema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua mali mbalimbali, zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama kuridhia na kutaisha mali hizo kuwa za serikali
 
Sijaona cha kifahari hapo, ukweli hio nyumba sio ya kifahari, hata hizo gari vile vile..
 
Pesa zilizotoka Treasure ya USA zitapoteaje kwa mfano!Ndo maana wamebainika.
Serikali imetaifisha rasimi Mali za Wakili maarufu Nchini Median Mwale zenye thamani ya sh,bilioni 1.2 zilizotokana na zao la utakatishaji mara baada ya mahakama kuu kumtia hatiani na kuamuru Mali hizo zitaifishwe.

Akiongea katika zoezi la makabidhiano kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP na Hazina,Mkurugenzi wa Mashtaka , (ASP )Biswalo Mganga alizitaja Mali hizo kuwa ni pamoja na Magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa kituo kikuu cha polisi,jijini hapa.

Mali zingine zilizotaifishwa ni pamoja na Nyumba mbili ikiwemo iliyopo ploti Namba 261 block c Njiro na nyumba nyingine iliyopo ploti namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.

Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia mahakama kuu kanda ya Arusha,kutaifisha Mali hizo na kwamba April 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasimi na kuwa Mali ya serikali.

"Kwa mujibu wa sheria Mali zinapotaifishwa kuwa Mali ya serikali zinakuwa chini ya katibu mkuu Hazina" Alisema.

Naye kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Mali za serikali Hazina,Benezeth Rutta Alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa wizara ya fedha zinapangwa kadri serikali itakavyoona inafaa.

"Mali hizi Mara baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana Mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada" Alisema Rutha.

Kwa upande wake kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi ,Selemani Nyakulinga Alisema Alisema kuwa mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dolla la marekani milioni 17.2 kutoka mfuko wa global fund kwa ajili ya kusaidia kutibu malaria na HIV Nchini Tanzania zikitoka kwenye Hazina ya nchi ya Marekani.

Alisema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni RAIA wa Kenya wakishirikiana na watanzania akiwemo Wakili Median Mwale .


Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua Mali mbalimbali zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama iliamuti na kutaifisha Mali hizo kuwa mali za serikali.





View attachment 1088100View attachment 1088102View attachment 1088104View attachment 1088105
 
Back
Top Bottom