The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Mali na Urusi zimetia saini mikataba inayolenga kupanua ushirikiano wa biashara ya pande zote mbili na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.
Makubaliano hayo ni pamoja na ahadi ya ushirikiano kuhusu nishati ya nyuklia, kulingana na maelezo yaliyotolewa na Kremlin.
Tangazo la mikataba hiyo lilikuja wakati wa ziara ya kiongozi wa kijeshi wa Mali Kanali Assimi Goïta mjini Moscow, ambayo ilijumuisha mazungumzo ya saa mbili na Rais Vladimir Putin, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.
Goïta ameimarisha uhusiano na Urusi tangu alipochukuwa mamlaka mwaka 2021, huku akipunguza uhusiano na Ufaransa amabyo ni koloni la zamani la taifa hilo.
Hii inaashiria mwelekeo mpana wa kikanda, huku nchi jirani za Burkina Faso na Niger pia zikielekea Urusi baada ya kuondolewa madarakani kwa viongozi wa kiraia.