.........Hapo sasa Mbu mzazi ni mzazi, mie nilishuhudia dadangu alipoolewa, mamake alikuwa Mgeni rasmi haswaaa tena mgeni rasmi asiyecheka wala kutabasamu!! nilimwelewa kwani nafsi ilikuwa inamsuta maana yeye alimkimbia (wakimia maana walikuwa watatu) akenda kwa mwenye pesa (ndivyo tulivyoambiwaga). But kuna ile ya mmama amenyang'anywa watoto wakingali wachanga...huyo ukisema umzuie kushiriki kwenye shughuli ya mtoto wake utakuwa unamuonea kupita kiasi! Maana sometimes bana inabidi mtu uchunguze authenticity ya 'stori' ulopewa.
Kuna mkaka mmoja alilelewa na Baba wa Kambo!! iakaambiwa kuwa Babake alikwendaoa mzungu akamtelekeza mama mtu huko Unyakyusani. Wakati wa arusi kijana kakomaa anamtaka babake aje arusini, watu wakamwambia ni haki yake, wakaafiki.........ikaanza saka baba yangu, saka baba yangu, Mbeya hayupo, Dar hayupo.........akaenda Arusha akampata!, kumbe ni Babake Mkubwa!! Yaani Mama alizaa na shemeji mkubwa na ndo ikawa chanzo cha talaka!
Harusi, misiba ni vitu vya siku moja na si malipo ya kulea. Kwa hiyo na mimi nakubali kuwa biological parent ndiye anayepaswa kuwa muhusika mkuu kwenye issue hata kama hakuchangia hata senti tano kwenye kukuza mtoto. Mimi mfano ikitokea nikaachika afu hubby akaniacha nikae na wanangu hata kama nia yake ilikuwa kukomoa, kwangu hilo ni zawadi kubwa sana kwa hiyo mzazi mmoja kupewa jukumu la kulea watoto kama hilo jukumu liko ndani ya uwezo wake ni kushukuru kwa kweli. Ku separate na watoto kunauma (kwa mtu mwenye akili timamu) waache walau wapate faraja ya kuwa wazazi kwenye harusi/misiba.
Na kingine kama binti au kaka anaolewa afu upande wa ukweni wajue kuwa mzazi halisi yupo kawekwa kando; mtafanya wakwe waogope familia yenu. Inatoa picha ya ubabe fulani hivi ambayo watu wengine wanafikia hata kusema kuwa hata huyu tulochukua atakuwa hivi hivi.
Linapokuja suala la binti anataka kuchumbiwa, JE? zile taratibu zetu za kupeleka posa sijui ndio kifunga uchumba,
mahari nakadhalika, Je?....hapa napo pakoje? !
Watafutwe ili washirikishwe ndugu na jamaa wa mke, au haya mambo yeshapitwa na wakati? Sidhani kama ni jambo la ajabu kuona siku ya harusi hata mama mlezi anapewa tuza zake kwa kumlea vyema mtoto japo mzazi wake yupo!
Umeona AshaDii! Kuna vitu vingine bana mtu wa nje hawezivielewa kivile kwa kuwa si yeye alokivaa kiatu kile...kunamaudhi mengine hukufanya mpaka sometimes u'mnunie' hata spouse wako kisa unaona anamtetea Ex lol!!
Kuna mdada mmoja yeye ameolewa akiwa na watoto wawili wa Ex- ni baada ya kuteswa na kupigika ipasavyo na Ex akamhakikishia kabisa kuwa hakuna atakae'mpenda'........akapendwa yeye na wanae.......Ex kagoma kutoa matunzo anadai akitaka awalipie wanae ada basi agaiwe na mbuchuchu kwanza!!............Mdada current spouse yuko njema na hana shida kabisa juu ya watoto hawa na watoto wanampenda kuliko! but sometimes mtu unajisikia tu vibaya maana unaona kama unamtwisha mzee wa watu mzigo uso na lazima.
Asa huyu Ex- kama si ubahau nn...... mbwai!! ah
Mbu, Ahsante sana kwa mada hii inayogusa maisha halisi ambayo wengi wetu tumepitia au ndio tunapitia kwa sasa. Nimependa sana michango iliyotolewa hapo juu.
Jamani kabla ya kuachana tusikimbilie kugombania nguo, magari, na viwanja. Tugombanie hati za kisheria, haki na mipango ya malezi ya mtoto. Tupoteze muda kwa kukimbizana na wanasheria..hayo yatalipa huko mbele
Nawasilisha..
I wish Tulizo angekuja kwenye huu ulimwengu tuliopo kabla ya kuongea hilo.
Hapa inahitaji ushirikiano wa hali ya juu wa watoto hasa kama wana akili zao na wazazi husika. Watoto wengine hawana makuu hata pale mzazi wa kambo anataka kutoa discpline kutokana na kuvunja sheria za nyumbani pale, lakini watoto wengine huwa hawakubali asilani kuadhibiwa kwa namna moja au nyingine na mzazi wa kufikia akishatamka "you're not my father/mother" basi hapo uje huwezi kusikilizwa tena na inakuwa ngumu sana yule biological parent anapomuunga mkono na mguu mwanae kwamba wewe kama mzazi wa kufikia huna mamlaka yoyote ya kumpa adhabu ya aina yoyote mwanae pale anapokosea.
Pia chuki zilizojengeka kati ya Wazazi walioachana zinaweza kabisa kuchangia kuongeza ugumu wa malezi ya watoto hao hasa pale ambapo wanamuona mzazi mmoja ndiye mkosaji mpaka kufikia kwa ndoa kuvunjika.
Ni kazi mno kusema kweli lakini wengine wana bahati zao hupata watoto wenye tabia njema sana kama huwajui unaweza kudhani mzazi yule si wa kambo na hata Wazazi wengine pia huwapenda watoto wao wa kufikia kama vile ni watoto wao kabisa.
Observation yangu mama mpya inakuaga ngumu sana kum accept mtoto ambaye si wake,but kina baba mara nyingi huwa so kind sijui kwanini.Mama wachache wanaweza kutoonyesha tofauti kati ya watoto wa kuwazaa na wakambo.But mtoto bado ana right ya kuona wazazi/mzazi wake hata kama separation ilikuwa ni ya ugomvi
...kwenye hoja ya msingi niligusia mila na tamaduni zinavyoweza leta athari pia kwenye jambo hili.
Hapa sitazungumzia ukabila, mfano binti wa kizaramo kalelewa na baba wa kambo huko Usukumani
kiasi cha binti kwa kiwango kikubwa kachukua mila na tamaduni za huko.
Linapokuja suala la binti anataka kuchumbiwa, JE? zile taratibu zetu za kupeleka posa sijui ndio kifunga uchumba,
mahari nakadhalika, Je?....hapa napo pakoje? Watafutwe ili washirikishwe ndugu na jamaa wa mke, au haya mambo yeshapitwa na wakati? Sidhani kama ni jambo la ajabu kuona siku ya harusi hata mama mlezi anapewa tuza zake kwa kumlea vyema mtoto japo mzazi wake yupo!
...Enheee, hapa ndio napataka.
Iweje wewe mama mzazi uliyemlea binti mfano ana 2-3 years, ukahangaika nae kwa uzima na ugonjwa, mpaka binti kavunja ungo, kamaliza madarasa na leo anaolewa halafu eti shughuli ya kuozesha isiwe yako? Huyo mama/baba mzazi aliyemtelekeza/kunyang'anywa mtoto ananafasi gani kwenye shughuli hiyo kama sio 'mgeni mwalikwa' tu kwasababu za ki itifaki? Nishayashuhudia haya, msinibishie.
Kwa upande wa kijana wa kiume ni hivyo hivyo, mama mlezi kwenye scenario ya hapo juu inaingiliana vile vile.
Hapana, naamini mama na baba mlezi wana nafasi kubwa kwenye kuamua shughuli nzito kama hiyo, hata panapotokea msiba.
Haya mambo kiukweli si ya kupuuzwa, maana kila siku ya mwenyezi mungu kuna jipya linalozuka kugombea uhalali wa mtoto.
Kuna watu walifikia hata kugombea maiti!
Mkuu, Tulizo haitaji kuja kwenye huo ulimwengu kwani amekulia kwenye huo ulimwengu.
Binafsi, Kuna mengi mabaya ambayo nayakumbuka hadi sasa, nami nimeapa kuwa nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuepusha watoto wangu kuingia kwenye maisha kama haya ya wazazi wa kambo wasio thamini viumbe wengine ..Hebu fikiri unalelewa na mzazi wa kambo ambaye yuko tayari kuzima Jiko la kupikia, kumnunulia chips mtoto wake na kuacha watoto wengine wakiangalia kwa uchungu au kusubiri kurushiwa vipande vya mabaki na mdogo wao kama mbwa uliza kisa ...baba yao kasahau kuacha hela ya chakula na Mama wa kambo ingawa anayo hela lakini hawezi kuchezea hela yake kulisha watoto wa mtu mwingine.
Picha kama hii inaweza kukaa akilini hadi unakufa.. na inarudi kila unaposoma thread kama hizi..
My apologies..a bit out of topic..
Nyamayao pole sana kama mpaka leo unamsaka baba. Wish u will see him one day
Sorry Nyamayao nimekusoma. Samahani sana. Nilidandia treni kwa mbele.