Malezi:"Nafanya kazi sana kukuhudumia" je kuna ulazima wa hii kauli kwa watoto??

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Imefika steji wazazi wengine hawajui hata kwanini walizaa, lengo lilikuwa ni starehe tu mara anatokea mtoto. , yani hata ndege naona wanatuzidi akili maana wao huhakikisha wamejenga kiota na kutunza chakula ndio wanapoamua kuzaliana ili watoto wasipate shida.

Sasa huku imeonekana kama watoto wamezaliwa kwa hitilafu za kondom kupasuka maana wazazi wengi wamegeuza kuhangaika kwao kuwa lawama kuu kwa kosa hata dogo akifanya mtoto, unakuta ntoto karudi nyumbani hana hata kosa anaomba hela ya shati jipya la shuleni mzazi anaanza kulalamika "anahangaika ama kufanya kazi sana kumtunza" na hiki kisingizio kinatumika kwenye kutoa adhabu.

Mi nadhani hakuna umuhimu wa kulalamika unahangaika kiasi gani ama kufanya kazi kiasi gani kumtunza mtoto wako, Ni wajibu kumtunza mtoto wako
 
Ktk elfmoja ni mzaz mmoja tu anaweza kulalamika hivi, mbona umelielezea kama tatizo kubwa ktk jamii?
 
niliwahi kuambiwa nifanye usafi ndani, ile naelekea ndani nikaambiwa tena "kama hauwezi kufanya usafi bc chukua begi lako na uondoke.
 
Tatizo tunazaa zaa tu bila mpango. Hayo ndio matatizo ya kukurupukia vitu viko nje ya uwezo wako.
Kila mtu azae idadi ya watoto anaowamudu.
 
Hii kauli inapomtoka mzazi ujue inaambatana na huzuni isiyo kifani kutoka kwa mzazi.

Hebu fikiria una mtoto hakuna anachokosa kuanzia chakula, nauli ya shule na stencils kama zote lakini kati ya watoto 145 (kwa idadi ya kayumba) anakuja kuwa wa 120.

Mleta mada kama bado kuzaa omba yasikukute
 
Mimi nakusaidia utakuja kunisaidia nini wewe ?

In short huku Afrika wazazi wengine hawajui hata kwanini walizaa, lengo lilikuwa ni starehe tu mara anatokea mtoto.

Na kibaya zaidi wanajichukulia perfect, hata kama hataki kabisa kujishughulisha na majukumu lakini mtoto akifanikiwa utasikia baba ni baba tu.

Wengine kazi yao kupiga machine tu kuhusu watoto hajui hata wanakulaje.

Anakwambia tu wakikua watamtafuta baba yao
 
Kuna siku nilimuuliza bi mkubwa hivi sisi watoto wako ulituzaa kwa kupangilia au ilitokea tu , alinikata jicho hilo akaniambia nisubiri wa kwangu niwapangilie . Naona enzi hizo walikua wanazaa tu kutimiza majukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kauli inapomtoka mzazi ujue inaambatana na huzuni isiyo kifani kutoka kwa mzazi.

Hebu fikiria una mtoto hakuna anachokosa kuanzia chakula, nauli ya shule na stencils kama zote lakini kati ya watoto 145 (kwa idadi ya kayumba) anakuja kuwa wa 120.

Mleta mada kama bado kuzaa omba yasikukute
Dada yangu alirudia form 4 mara tatu mfululizo na chuo aliwahi kufukuzwa akatafutiwa kingine, wazazi hawakukata tamaa wakamsomesha upya, Leo hii kaajiriwa anapokea mshahara kama wengine wale vipanga wa darasani, Jukumu moja wapo la mzazi ni kutokata tamaa na mtoto
 
Dada yangu alirudia form 4 mara tatu mfululizo na chuo aliwahi kufukuzwa akatafutiwa kingine, wazazi hawakukata tamaa wakamsomesha upya, Leo hii kaajiriwa anapokea mshahara kama wengine wale vipanga wa darasani, Jukumu moja wapo la mzazi ni kutokata tamaa na mtoto

Sawa mzazi hatakiwi kukata tamaa lakini mtoto naye atimize wajibu wake ipasavyo asipotimiza inaleta msongo wa mawazo kwa mzazi. Tuna watoto na tumesomesha wadogo zetu tunajua maumivu pale mtoto anapokuwa hafikii matarajio yetu
 
Ni wajibu na lazima wazazi wore kuwahudumia na kuwapatia watoto wao mahitaji yote ya msingi, na hili sio ombi kwasababu hakuna mtoto aliye omba azaliwe na badala yake starehe zetu ndizo zilitufanya tuwatengeneze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa maisha umekuwa mgumu sana.

Mke akuroge, Jirani akuroge, kazini Wakuroge, Mchepuko Ukuroge, Njia panda urogwe.. n.k.

Unahisi maisha utakayoishi yanafananaje?

Acha walalamike, ipo siku Mungu atawasaidia katika madhaifu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iyo siku nilikuzaa natamani ningetumia huo muda kuogelea mtoni.

Kanisani kulikuwa kuna wimbo unasema. "WATOTO ni Baraka kwenye familia *2
WATOTO ni neema Toka kwa Mungu.

Alikuwa anasema nyie ni laana. Najuta kukuzaeni..

Jamanieeee wazazi tuwapende wanetu na km ni single mom. Mrudishe mtoto kwa babake kuliko kumtesa wewe mwenyewe, bora akateswe na mama wa kambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom