Malengo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malengo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by donjackfield, Apr 10, 2011.

 1. donjackfield

  donjackfield New Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  p { margin-bottom: 0.08in; }a:link { }  MALENGO

  Maendeleo mengi yaletwayo na binadamu yote yalianza na hao watu kuwa na malengo,wanasayansi walikuwa na malengo ya kufika mwezini na wakafanikiwa.Malengo ni zaidi ya ndoto,ni ndoto zinazochukuliwa hatua(zinafanyiwa kazi).Mtu asiye na malengo anahihishi kwa kutegemea bahati,kwa nini utegemee bahati wakati unaweza fanya vitu utakavyo wewe?anza kuwa na malengo katika maisha.Malengo ni muhimu katika maisha kama ilivyo hewa,bila hewa maisha hakuna.Nitolee mfano kampuni kubwa duniani,hizi zina malengo ya miaka 20 na zaidi,ni jinsi gani wataongeza fedha,ni vipi watazalisha bidhaa,technolojia gani watatumia na mengineyo.Tujifunze kupitia kampuni hizi,nasi pia tunahitaji malengo yetu binafsi,jenga malengo ya miaka kumi ijayo,jione miaka kumi ijayo utakuwa wapi,unafanya nini,umeoa au umeolewa,kazi gani unafanya,unawatoto wangapi,unaishi na mzazi au unanyumba yako.Vuta picha hiyo ya wewe miaka kumi ijayo itakusaidia katika kutengeneza malengo maishani.
  MWONGOZO WA PICHA YA
  MAISHA YAKO MIAKA 10 IJAYO:

  A: KITENGO CHA KAZI:miaka 10 ijayo:

  1:Ni kiasi gani cha mshahara nakihitaji?
  2:Majukumu ya aina gani nayahitaji?
  3:Ni sifa ya aina gani naahitaji nikiwa kazini?


  B: KITENGO CHA NYUMBANI:miaka 10 ijayo:

  1:Ni standard gani ya maisha ninaihitaji?
  2:Ni nyumba ya aina ipi nitaishi?
  3:Likizo zangu nitaenda wapi?
  4:Ni fedha kiasi gani nitatumia kwa watoto mpaka wanakua watu wazima?


  C: KITENGO CHA JAMII:miaka 10 ijayo:

  1:Marafiki wa aina gani nahitaji kuwa nao?
  2:Jumuiya gani nahitaji kujiunga nazo?
  3:Uongozi gani nahitaji kuwa nao?

  Ni kweli mengi yanaweza tokea hapo katikati ya safari,lakini hayo yote yaangalie kwa kona hii,hayaja kuharibia lengo lako bali yamebadilisha njia ya kufikia lengo lako.Kuna watu watajitokeza na kukuambia hili haliwezekani na maneno mengine mengi.Lakini kama kweli unauhakika na unachofanya na unaona kuna matunda hauta achana nalo.Nataka zungumzia uwekezaji,sio kwenye kampuni bali kwako mwenyewe.Ni nini unawekeza maishani mwako?elimu?starehe?ujinga?umaskini?tabia njema?au mbaya? na mengineyo.Nitazungumzia uwekezaji wa aina mbili moja ni elimu,la pili waanzisha fikra.


  ELIMU:hii ni moja ya vitu unavyotakiwa kuwekeza,lakini tunajua elimu ni nini?elimu ya ukweli ni ipi?Kuna watu wanapima elimu kwa miaka mingi wakaayo shuleni hadi vyuoni,na wengine wanapima elimu kwa wingi wa vyeti walivyonavyo iwe vya dilpoma ama degree.Vyeti hivyo vitakufanya upate kazi lakini usipo kuwa na ustadi kazini vyeti havitasaidia.Wengi wanavyeti lakini wanakosa ustadi na ubunifu endelevu kazini,hao wote wamesoma lakini hawajaelimika.Elimu ni kiasi cha maarifa uliyonayo kichwani,na jinsi gani uyatumiajo hayo maarifa maishani.Wengi wetu tunakosa kuyatumia maarifa yetu vizuri.


  VIANZISHA FIKRA:Mengi yanatokea baada ya mtu kufikiria,mtu alifikiria kunauwezekano wa kwenda mwezini na kweli fikra yao ikafanikiwa.Tuwe na tabia ya kukusanya fikra tofauti ambazo ni endelevu kupitia watu,vitabu,tv na kadhalika.Hivi vitakujenga upeo wako wa kufikiri,utapata mbinu mpya za kufanya mambo.Kunasiku nilikuwa nasoma makala kwenye blogu inaitwa MAISHA TANZANIA basi baada ya kumaliza makala zile nikapata idea,hii blogu ni kwa ajili ya vijana wa kitanzania na inabidi wapate ujumbe uliomo,wazo kuu lililonijia ni kwamba nitaongea na mwenye blogu na kupitia makala zake tutatengeneza kipindi cha televisheni(documentary) ili vijana wengi waweze pata maarifa pitia makala hizo.Fikra hiyo yote ni baada ya kusoma mambo endelevu yanayo fungua ubongo.
  CHUKUA HATUA
  1:Kuwa na malengo ya nini wataka fanya miaka kumi ijayo na zaidi.
  2:Andika chini plani zako za kazi utakayo fanya,majukumu ya kifamilia na kijamii.
  3:Weka malengo yako kuwa mwongozo wako.
  4:Fanikisha lengo moja moja,hata likiwa dogo kiasi gani.
  5:Wekeza katika elimu na sio shule,soma mambo endelevu ya kufungua ubongo.

  BY: JACKSON L FUTE
   
Loading...