Malengo yangu ya kuweka Tsh 20,000 kila siku

Jumaaofficial

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
250
209
Habari wana JF,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 elimu yangu kidato cha 4 katika harakati zangu za utafutaji wa pesa nimefanikiwa kuanzisha duka.

Kiukweli mwanzo kipindi naanza hali ilikua ngumu sana kwani mtaji wangu ulikua mdogo, lakini namshukuru Mungu amenisaidia hadi leo biashara yangu imekua kubwa. Nimekua na malengo mengi sana na namuomba Mungu aendelee kunipa baraka zake nifikie malengo yangu hasa kwangu kama kijana nimekua nikitamani vingi sana.

Kuwa na gari nzuri nyumba nzuri nk.

Kuna siku nilikaa nikafikili hivi ni lini nitapa sehemu ya kupata ma-milioni ya pesa jibu nikawa sipati.

[HASHTAG]#nikatumia[/HASHTAG] muda wangu mwingi kusoma vitabu vya ujasiriamali nikagundua, kwamba hakuna alifanikiwa kwa kupata mapesa rundo bali njia ya kufanikiwa ni kujiwekea akiba ambayo itakua the big Point ya kufanikiwa.

Nikaamua kila siku niweke Tsh 20k per day kwa mwezi target yangu iwe 600,000 kama mshahara wangu katika biashara zangu, kwa mwaka milioni 7,200,000. Kwasasa nipo mwezi wa 3 nimefanikiwa kwa asilimia 55% kwa hii imeniongea nguvu zaidi ya kupigana ili nisifeli.
 
Hongera sana kijana..cha msingi ni kuzuia msingi wako wa biashara usiyumbe na kulipa kodi kwa wakati kuepusha usumbufu.la muhimu sana ni kuheshimu matumizi yako, na cku zingine ukipata zaidi unaongeza kiwango cha akiba..kila mwisho wa mwezi au week akiba iende bank ili kujiwekea profile zuri endapo siku utataka kuongeza mtaji kwa njia ya mkopo.
 
Unapiga ishu gani mkuu inayokuingizia sh 20 elfu kwa siku??
Duka kasema... sema hajagusia la nini...

Bila shaka atakuwa snaingiza mishahara ya watu... kama anaweka 20000 inamaana anapata tuseme faida ya 40000 ikipungua 35000

40000 × 30 = 1,200,000

Hongera kwa malengo uliyojiwekea.
 
Nidhamu ya pesa inamchango mkubwa sana ili kufanikiwa. Utaratibu wa kujiwekea akiba ni mojawapo ya kujenga hiyo nidhamu na kutimiza malengo.

Hongera sana
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 elimu yangu kidato cha 4 katika harakati zangu za utafutaji wa pesa nimefanikiwa kuanzisha duka.

Kiukweli mwanzo kipindi naanza hali ilikua ngumu sana kwani mtaji wangu ulikua mdogo, lakini namshukuru Mungu amenisaidia hadi leo biashara yangu imekua kubwa. Nimekua na malengo mengi sana na namuomba Mungu aendelee kunipa baraka zake nifikie malengo yangu hasa kwangu kama kijana nimekua nikitamani vingi sana.

Kuwa na gari nzuri nyumba nzuri nk.

Kuna siku nilikaa nikafikili hivi ni lini nitapa sehemu ya kupata ma-milioni ya pesa jibu nikawa sipati.

[HASHTAG]#nikatumia[/HASHTAG] muda wangu mwingi kusoma vitabu vya ujasiriamali nikagundua, kwamba hakuna alifanikiwa kwa kupata mapesa rundo bali njia ya kufanikiwa ni kujiwekea akiba ambayo itakua the big Point ya kufanikiwa.

Nikaamua kila siku niweke Tsh 20k per day kwa mwezi target yangu iwe 600,000 kama mshahara wangu katika biashara zangu, kwa mwaka milioni 7,200,000. Kwasasa nipo mwezi wa 3 nimefanikiwa kwa asilimia 55% kwa hii imeniongea nguvu zaidi ya kupigana ili nisifeli.
Hongera sana mkuu,
Ni hatua kubwa sana hiyo.
Nashauri kama hujasoma bado pitia hiki kitabu hapa
8ee561b66c526bc66bb5c19cf9e3fd9a.jpg

You'll never regret
 
Nikaamua kila siku niweke Tsh 20k per day kwa mwezi target yangu iwe 600,000 kama mshahara wangu katika biashara zangu, kwa mwaka milioni 7,200,000. Kwasasa nipo mwezi wa 3 nimefanikiwa kwa asilimia 55% kwa hii imeniongea nguvu zaidi ya kupigana ili nisifeli.[/QUOTE]

Hongera saana kijana. Kwa umri wako kufikiria kitu kama hiki ni hazina kubwa!
Hivi karibuni nilitaka kukopa benki nikaambiwa interest ni 18%. Yaani kama unakopa 1,000,000/- baada ya kulipa deni zima unakuwa umelipa 1,180,000/-
Nikaona haina haja ngoja nijinyime na ku-save na nina uhakika kwa kipindi kifupi nita-raise hizo 1,000,000/-.
Faida ya kufanya hivi ni:
- Muda wa kuzisubiri ili zifikie kiwango unachotaka utakuwa mzuri kwako kufikiria kwa umakini uzitumie vipi
- Muda ukiwadia hutakuwa na papara ya kuzitumia kwa miradi ambayo hujaifanyia uchunguzi mzuri
Tunasubiri mrejesho ili tusikie umezitumia vipi hizo pesa ulizozi-save!
 
Kusave hela tena kipindi hiki cha JPM inahitaji nidhamu...

Mimi nimeweka lengo
Natunza 150,000/- kwa kila wiki
Kuanzia January had December

Kwa wiki 52 yaani 31/12/2018 itakuwa 7.8M

Namshukuru Mwenyezi naingia wiki ya mwisho February ili nianze March

Naendelea kufanya utafiti biashara gani niinvest tupeane mawazo Ndugu zangu

.nafikiria Fixed Deposit kwa kila miezi 3 then nachukua zote naanza upya
 
Habari wana JF,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 elimu yangu kidato cha 4 katika harakati zangu za utafutaji wa pesa nimefanikiwa kuanzisha duka.

Kiukweli mwanzo kipindi naanza hali ilikua ngumu sana kwani mtaji wangu ulikua mdogo, lakini namshukuru Mungu amenisaidia hadi leo biashara yangu imekua kubwa. Nimekua na malengo mengi sana na namuomba Mungu aendelee kunipa baraka zake nifikie malengo yangu hasa kwangu kama kijana nimekua nikitamani vingi sana.

Kuwa na gari nzuri nyumba nzuri nk.

Kuna siku nilikaa nikafikili hivi ni lini nitapa sehemu ya kupata ma-milioni ya pesa jibu nikawa sipati.

[HASHTAG]#nikatumia[/HASHTAG] muda wangu mwingi kusoma vitabu vya ujasiriamali nikagundua, kwamba hakuna alifanikiwa kwa kupata mapesa rundo bali njia ya kufanikiwa ni kujiwekea akiba ambayo itakua the big Point ya kufanikiwa.

Nikaamua kila siku niweke Tsh 20k per day kwa mwezi target yangu iwe 600,000 kama mshahara wangu katika biashara zangu, kwa mwaka milioni 7,200,000. Kwasasa nipo mwezi wa 3 nimefanikiwa kwa asilimia 55% kwa hii imeniongea nguvu zaidi ya kupigana ili nisifeli.
Hongera sana kazana ndugu yangu, ila vikishafikia vimilioni milioni usibweteke ukazania umemaliza pambana sana na mwendo wako,kaa mbali na starehe za mjini utafanikiwa naongea haya kwa experience nilonayo.
 
Mawazo mazuri kijana

Ila naomba nikushauri kitu

Baada ya mwaka ukifanikiwa kupata hiyo milion 7 tafuta biashara nyingine ambayo utaweza kusimamia wekeza ili uongeze income yako ya per day.
 
Kusave hela tena kipindi hiki cha JPM inahitaji nidhamu...

Mimi nimeweka lengo
Natunza 150,000/- kwa kila wiki
Kuanzia January had December

Kwa wiki 52 yaani 31/12/2018 itakuwa 7.8M

Namshukuru Mwenyezi naingia wiki ya mwisho February ili nianze March

Naendelea kufanya utafiti biashara gani niinvest tupeane mawazo Ndugu zangu

.nafikiria Fixed Deposit kwa kila miezi 3 then nachukua zote naanza upya
Mmh mkuu unapiga mishe gan
 
Back
Top Bottom