Malecela na Lowassa wasusia kikao cha kamati kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela na Lowassa wasusia kikao cha kamati kuu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Aug 13, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wajumbe wote wa kamati kuu ya CCM wamehudhuria kikao cha CC kinachoendelea Dodoma isipokuwa mwanasiasa mkongwe, John Samuel Malecela pamoja na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

  Haikuweza kufahamika sababu ya wajumbe hao kukosekana katika kikao hicho muhimu cha chama. Kulikoni?
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Don't be suggestive! The duo might be having some 'udhuru' of course!
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mmh! Mbona nimeona TBC wakionyesha Mzee Malecela yupo na alikuwa akisalimia na Spika Sitta.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hapo sasa!
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kumuona kwenye TV au kuwepo Dodoma ni tofauti na kuhudhuria vikao,

  Hali tete CCM, CC YAAHIRISHWA
   
 6. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nimemuona kwa macho yangu anasalimiana na spika sitta! mh! Hata kama sijamuona lowassa sipaswi kukuamini kwa hili umeonesha kutokuwa mwaminifu!
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du; Mkuu, Kikao kimefanyika na Mzee BM alikuwepo na JK aliki-Chair. Huenda kiliahirishwa asubuhi lakini Mchana-Jioni kimefanyika. Kulikuwa na Makabrasha wanayogawiwa makubwa kuliko kawaida.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hali tete CCM, CC YAAHIRISHWA

  Sadick Mtulya, Dodoma

  UKIUKWAJI mkubwa wa taratibu wakati wa kura za maoni, tuhuma za rushwa na wanachama kupinga maamuzi ya baadhi ya kamati za siasa za mikoa kugeuza matokeo, ni mambo ambayo yanaendelea kuisumbua CCM kiasi cha kamati kuu kulazimika kuahirisha kikao ambacho kilitakiwa kufanyika jana.

  Ratiba ya awali ilionyesha kuwa kamati hiyo ingefanya kikao chake jana na leo kujadili ajenda za halmashauri kuu baada ya kamati ya maadili kumaliza kuzipitia ajenda hizo.


  Lakini, taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa kamati ya maadili ilishindwa kumaliza kazi ya kupitia ajenda hizo kutokana na wingi wa malalamiko yaliyowasilishwa na wagombea na baadhi ya wanachama kupinga matokeo ya kura ya maoni na maamuzi ya kamati za siasa.


  Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwaambia wajumbe wa kamati kuu jana akisema: "... kikao chetu cha leo cha CC kimepata udhuru kidogo, hivyo tumekiahirisha hadi kesho saa 3:00 asubuhi.


  "Sababu kuu ni kamati ya maadili ya chama hadi sasa (saa 9:26 alasiri) bado haijamaliza kazi yake."


  Kikao cha kamati ya maadili kilianza jana majira ya 5:00 asubuhi mara baada ya sekretarieti ya CCM kumaliza kikao cha kuandaa ajenda za kamati kuu. Sekretarieti ilikuwa na kikao chake kuanzia juzi.


  Hata hivyo, vyanzo vyetu vilisema uzito wa malalamiko yaliwayosilishwa kuhusu mchakato mzima wa kura ya maoni ya kuchagua wagombea ubunge na udiwani ulivyofanyika Agosti mosi, hasa vitendo vya rushwa, ndio sababu kubwa ya kamati ya maadili kushindwa kumaliza kikao chake kwa wakati.


  "Kwa asilimia kubwa karibu wagombea wote waliojitokeza kwa ajili ya kuchaguliwa katika kura za maoni ya CCM, walivunja maadili ya chama, hasa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa," alisema mmoja wa watu walio karibu na kamati kuu.


  "Suala hili ndilo limesababisha kamati kushindwa kumaliza kikao chake kulingana na ratiba."


  Baada ya kauli ya Makamba, baadhi ya wajumbe wa kamati ya maadili, akiwamo rais mstaafu wa serikali ya awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa walitoka katika kikao cha ndani cha kamati hiyo na kuchukua nyaraka zao zilizokuwepo katika meza kuu ya ukumbi wa White House na kurudi nazo ndani, kuashiria kuendelea na kikao cha kamati ya maadili.


  Kampeni na kura za maoni za CCM zilitawaliwa na vitendo vya rushwa na kusababisha wagombea wengi na viongozi wa matawi na kata wa chama hicho kukamatwa na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Hadfi sasa ni wagombea watatu tu ambao wameshafikishwa mahakamani.


  Mbali na vitendo vya rushwa, upigaji kura za maoni ulitawaliwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu uliosababisha vurugu kwenye baadhi ya vituo na hivyo kusababisha wagombea wengi kukata rufaa baada ya matokeo kutangazwa wakidai kuwa kulikuwa na rafu nyingi.


  Vikao vya kamati za siasa za mkoa ambazo hutoa alama kwa wagombea navyo viliamsha tatizo jingine kutokana na wanachama karibu katika kila mkoa kufanya maandamano kwenda kwenye ofisi za chama hicho kupinga taarifa zilizokuwa zimezagaa kuwa washindi kwenye kura hizo wamepewa alama za chini zinazomaanisha kuwa hawastahili kupitishwa na chama kugombea.


  Kamati ya maadili inaongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti CCM, na wajumbe wengine ni pamoja na makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, na makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume ambaye pia ni rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


  Wengine ni Makamba, marais wastaafu, Mwinyi na Mkapa.


  Katika hatua nyingine, wajumbe wote wa kamati kuu jana walihudhuria kikao isipokuwa mwanasiasa mkongwe, John Samuel Malecela pamoja na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


  Haikuweza kufahamika sababu ya wajumbe hao kukosekana katika kikao hicho muhimu cha chama.


  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ni spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Samuel Sitta, na naibu wake, Anne Makinda, spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Amir Kificho, mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Ghalib Bilal pamoja na Abdallah Kinana.


  Katika hatua nyingine, wanachama 40 wa CCM Kata ya makulu jana walikamatwa wakati walipokuwa wakiandamana kwenye kundi la wanachama 100 kupinga kubadilishwa kwa jina la Ally Bilingi aliyeshinda katika kura za maoni za udiwani katika kata hiyo.


  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bilingi, Steven Ngogo aliliambia Mwananchi kuwa waliamua kwenda ofisi ya CCM ya Wilaya ya Dodoma Mjini kuhakikisha kama kweli ushindi wa Bilingi ulibatilishwa.


  "Tulikuwa zaidi ya 90, lakini wenzetu zaidi ya 40 wamekamatwa na Polisi majira ya saa 6:00 mchana wakati tulipokuwa tunakuja huku kama kweli jina la Bilingi ambaye alishinda kwa kura 190, limeondolewa,'' alisema Ngogo.


  Ngogo alifafanua kwamba taarifa ya kubadilishwa kwa ushindi wa Bilingi ziliwafikia mapema na kwamba ilisemekana uamuzi huo ulitokana na kamati ya siasa ya kata kumpa alama ya D.


  Hata hivyo, mwenyekiti wa wilaya hiyo, Denis Bendera aliwahakikisha wanachasma hao kuwa hakuna matokeo yeyote yaliyobatilishwa.


  "Hakuna matokeo yeyote ya kata na viti maalum hadi sasa yaliobatilishwa. Lakini Agosti 15, ndio majibu yatatolewa rasmi na mtapewa siku tatu za kupinga,'' alisema Bendera.

  Kamanda wa polisi wa Dodoma, Steven Zelothe alisema: "Kwa sasa siwezi kuzungumzia kukamatwa kwa hao watu... wewe si unajua kwamba kwa sasa Dodoma ina ugeni mkubwa wa rais, makamu, mawaziri," alisema Zelothe.
   
 9. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Luteni hiyo link ni ya lini maana hata sijaelewa kuna comment za leo! Unamaanisha tayari mwananchi la kesho limeshakuwa released! Hili linaripoti habari ya juzi leo malechela ameonekana kikaoni jk akisema kikao kimefunguliwa sio makamba aliyezungumza leo! Malechela alikuwa kikaoni kuhusu lowasa sijui.
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo unasoma heading tu husomi maelezo
   
 11. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du, kamanda mbona tunaanzisha ligi kwa vitu halisia. Hiyo news ni ya jana. Leo saa 3 ilikuwa CC ikutane ikahairishwa hadi baadaye mchana/jioni. Inawezekana wakati Mwananchi wanaenda mitamboni kikao cha CC kilikuwa hakijaanza. JK amefungua kikao rasmi na Mzee malecela ameonekana akisalimiana na mdau wake Sitta'
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hali tete CCM, CC YAAHIRISHWA

  Gazeti la Mwananchi
   
 13. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  la lini? Nataka kujua linaripoti habari ya siku gani? Unajua timing yako mbaya ungepost hiyo link asubuhi ulikuwa mda huu ni michanganyo tu unafanya! Maana iliyoitwa kesho ndio leo na iliyo itwa leo ni jana!! Mkuu vipi?
   
 14. M

  Mutu JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umesomeka Luteni,anyebisha abishane na gazeti.
  Waliona kwenye Tv inaweza kuwa picha za maktaba
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kumbe inawezekana.........sasa tatizo nini
  elewa kuna vikao zaidi ya vitatu vinaelelea Dodoma kuna NEC, CC na Kamati ya nidhamu sasa kama wewe ulimwona JK akifunga kikao utueleze ni kikao gani halafu vikao vingine vimefungwa na nani.
   
 16. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hizo habari zipo out-dated, ni za mwananchi la leo ambazo kimsingi ni habari za jana. Mzee Malechela yupo kwenye kikao na ameonekana kwenye taarifa ya habari ya TBC saa 2 usiku huu kama wadau hapo juu walivyodokeza.
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Superman na Tuntu

  Mnanishangaza kweli ina maana kama habari ni ya jana isijadiliwe, sijasikia watu wakisema habari ya Lowassa ya mwaka 2008 alipojiuzuru tusiijadili kwa vile ni out-dated, kwa maana nyingine mnataka kutuambia tuwe tunajadili habari za kuanzia kesho yake na kuendelea tu zilizopita hapana.

  Malecela na Lowassa hawakuhudhuria kikao iwe jana juzi au kesho hiyo ni issue nyingine, Mwananchi limeripoti habari ndiyo hiyo, mnaponibana mimi sijui niwaeleweje, waulizwe Mwananchi kwa nini wamechelewa kuiandika wanaandika habari out-dated? si mimi ndugu zangu.
   
 18. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, simaanishi kuwa haipaswi kujadiliwa bali nilijibu juu ya hili..

  Na hapa..

   
 19. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Sasa huu mjadala unazidi kufanya wale wanaoamini kuwa JF ni kijiwe cha porojo waconfrim hisia zao. Hivi kutokuhudhuria au kuhudhuria kwa hao wawili kuna athari gani kwa jamii kuwarant wana JF kutumia precious time yao kujadili. Kwani hawawezi kuwa na udhuru? Na kuahirishwa kwa kikao si jambo la kawaida?, especially kama kuna kikao tangulizi ambacho bila chenyewe kumalizika kikao kinachofuata hakiwezi kufanyika-- kweli hiyo hali ina quality ya kupewa uzito wa "hali tete" Si wameeleza kwa nini waahirishe, rufani ni nyingi kzuipitia na kuzitolea maamuzi inachukua muda- simple na sioni utete hapo lol

  Hivi thread kama hii ina manufaa gani kuelekea kwenye uchaguzi na mstakabali wa taifa letu? Oh mara kaonekana kwenye TV, oh mara gazeti la mwananchi limeandika, oh habari ya jana... who cares! anyways. Kama wananchi wa Mtera walimuona hafai wakamnyima kura, JF tunampapatikia wa nini, hana tena mvuto wa kujadiliwa hapa jamvini, huo ndio ukweli na tusipoteze muda kumjadili mtu ambaye keshamalizwa na wapiga kura wa jimbo lake.
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,838
  Likes Received: 11,956
  Trophy Points: 280
  mtu kakuletea habari bado unataka ujue gazeti la lini inamaana wewe umekaa mezani unaagiza kama chips niletee tomato souce na uma wake kabisa mbona umesahau vijiti ehe tujishughulishe.
   
Loading...