Wakati wa sakata la Escrow, profesa Anna Tibaijuka alinukuliwa akisema, 10M zilikua hela zake za mboga, tulipokua tunafanya digest ya hiyo statement hapa kazini kwetu niliwaambia hivi wenzangu; "Wakati wa kinyang'anyilo cha kumpata mgombea form ccm, tutajua nani hasa anaeongoza kupiga pesa za nchi hi, hiyo statement ya huyo mama haijatoka tu hiv hivi, anayo siri Fulani moyoni mwake, tusubiri" Wameisha anza kuumbuana, si tayari mzee malecela kasha sema hapo, kumbe pesa za Ubungo terminal hua zinaingia mfukoni mwa mtu na sio serikalini; halafu kucha kutwa, watu wanaenda kuomba msaada nje ya nchi na pesa tunaziacha hapa hapa, bado kidogo tutamjua na anae miliki Car parking system za miji yote mikubwa nchi hi. Ya Kakobe naona yanaanza kutimia mdogo mdogo