BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
KLHN Wire
Alipoulizwa kuhusu mipango yake ya kisiasa ya baadaye na hasa kama ataingia tena katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais Mzee Malecela alisema kuwa imekuwa ni utamaduni ndani ya CCM kwa Rais aliyeko madarakani kuachwa kukamilisha vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba na hivyo mpango huo kwake kwa mwakani haupo. Hata hivyo alionesha kuwa ana mpango wa kuendelea kulitetea jimbo lake la Mtera ambalo ameliongoza kwa karibu miaka 40 sasa.
Utamaduni huu wa kumuachia mgombea wa CCM akae madarakani kwa awamu mbili inabidi upigwe vita hasa pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha kwamba yule aliye madarakani hastahili kupewa awamu nyingine. Kikwete Urais umemshinda hivyo huu utamaduni ndani ya CCM inabidi usitishwe haraka sana kwa maslahi ya nchi.