Malecela avunja ukimya!

Malecela ni yule aliyewahi kubadili jina na kuitwa jumanne akapewa magari zaidi ya 64 kwa ajili ya kampeni na waarabu. nakumbuka nyerere alimwambia John ukisha kuwa raisi utalipajie hiyo mali. Mwalimu akamwambia Ali akimpitisha Jumanne atampigia mrema debe.
CCM ni dampo kweli hata aongee nani dampo limeoza linatoa funza hakuna wa kumsikiliza.Hana jipya ana hasira ya kunyimwa ulaji yeye na kilango.
Debe tupu hupiga kelele sana
 
Malecela amewataka wote wanaolumbana wakome mara moja kwani hayana tija na kwamba vyombo vya habari viendelee kufichua ufisadi badala ya kutumika kutukanana. Amekwepa sana kuzungumzia specific issue japo alipobanwa maswali kuhusu Dowans alisema kwamba hiyo ni sawa na kupiga bakora maiti ya farasi kwa kuwa suala hilo lilimalizwa na Bunge na kwamba kama kuna mwenye hoja tofauti alirudishe bungeni kwa utaratibu unaokubalika na si kulumbana kwenye vyombo vya habari. Akasema mambo ya CCM yamalizwe na CCM, ya Bunge yamalizwe bungeni, ya serikali ichukue hatua kwa yale yaliyo eneo lake, ili kila kitu kiwe na mwisho.. Akakumbushia wabunge waliowahi kutimuliwa chama na hatimaye ubunge wakiwamo Mwakitwange, Choga na Masha. Mengine baadaye, msimulizi yuko bize
 
Mtanzania, Malecela ni Mgogo. Ili uweze kuishi Dodoma, inabidi uwe Mvumilivu sana. Wagoggo AKA AGWE, wana kauvimilivu sana. Wao huwa hawana maneno maneno kama sisi/nyinyi. Hata wakoloni hapo walipita tu bila kupata matatizo yoyote. Ukichunguza sana unakubali kuwa Wagogo ni Wazaramo walioenda Dodoma kuchukua Mbuzi wa Arobaini........ mengine yatakuja endelea.

Naona kama Mkuu Sikonge unaelekea katika ukweli, hao ni wazee wa zamani. Lakini vijana wao wa sasa wako Ngangari mno.
 
Malecela ni yule aliyewahi kubadili jina na kuitwa jumanne akapewa magari zaidi ya 64 kwa ajili ya kampeni na waarabu. nakumbuka nyerere alimwambia John ukisha kuwa raisi utalipajie hiyo mali. Mwalimu akamwambia Ali akimpitisha Jumanne atampigia mrema debe.
CCM ni dampo kweli hata aongee nani dampo limeoza linatoa funza hakuna wa kumsikiliza.Hana jipya ana hasira ya kunyimwa ulaji yeye na kilango.

Hivi Mkuu bado unaishi zama za kufikirika, hata hili bado unalizungumza, na wala hujui kwa nini Mwalimu alimuondoa Malecela. Tuna safari ndefu.
 
tunaendelea kusubiri executive summary ya alichozungumza malecela
bila shaka hataacha kuzungumzia swala la dowans
hili la kutishiana kufukuzwa ubunge kama akina choga, mwakitangwe amekoroga, watu kama akina mwakyembe nani kwa kuambia wanaogopa kufukuzwa ubunge?
 
Hivi Mkuu bado unaishi zama za kufikirika, hata hili bado unalizungumza, na wala hujui kwa nini Mwalimu alimuondoa Malecela. Tuna safari ndefu.

Usijali sana, huo ni ukweli pamoja na mambo ya muungano.hata hivyo kesha
safari kweli ni ndefu kwani dampo lanuka mno.
 
Ingawa ukilinganisha na vigogo wengi wa CCM, huyu angeweza kuwa na moral authorty (mamlaka ya kimaadili) ya kukemea -- bila kutafuna maneno -- ufisadi ndani ya serikali na chama tawala kwa sababu yeye anaonekana ni Mr Clean -- hajaguswa na uchafu wote huu unaotokea na unaoendelea kutokea.

Sababu ya pili ambayo ingemwezesha kufanya hivyo inatokana na yale masaibu yaliyompata wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais ktk chama chake mwaka 2005 -- kwa sababu mtandao ule wa wabaya wake ndiyo ule ule sasa umekumbwa na kashfa mbali mbali za kifisadi. Kwa hiyo angekuwa amejipatia "an axe to grind."

Lakini hajafanya hivyo kabisa, amekaa kimya tu kama mtu mwenye woga mkubwa -- utadhani anaogopa naye mdhambi yake ya ufisadi yatakuja kutolewa hadharani.

Labda naye anayo? Wana JF mnasemaje? -- yaani mbali na kashfa yake ile ya early 80 ya kuwatukana wananchi (waliokuwa wakikosa ticket za kusarfiria TRC) kwa kuwaambia "they can go to hell if they so wished."

Malecela angeweza sana kukisaidia chama chake na nchi kwa ujumla kama angejitokeza hadharani na kuwa upande wa haki -- wa wapiganaji wa ufisadi.

Ni kweli, mkewe Anne amewahi kunguruma hapa na pale lakini kuna udhaifu pale, hasa anaporejeshewa mapigo, na hususan kwa kuwa yeye ni mwanamke.

Kuna Malecela mwingine kajiunga na JF na amenza kupost za "upiganaji" Sijui kama kuna uhusiano.
 
Malecela amewataka wote wanaolumbana wakome mara moja kwani hayana tija na kwamba vyombo vya habari viendelee kufichua ufisadi badala ya kutumika kutukanana. Amekwepa sana kuzungumzia specific issue japo alipobanwa maswali kuhusu Dowans alisema kwamba hiyo ni sawa na kupiga bakora maiti ya farasi kwa kuwa suala hilo lilimalizwa na Bunge na kwamba kama kuna mwenye hoja tofauti alirudishe bungeni kwa utaratibu unaokubalika na si kulumbana kwenye vyombo vya habari. Akasema mambo ya CCM yamalizwe na CCM, ya Bunge yamalizwe bungeni, ya serikali ichukue hatua kwa yale yaliyo eneo lake, ili kila kitu kiwe na mwisho.. Akakumbushia wabunge waliowahi kutimuliwa chama na hatimaye ubunge wakiwamo Mwakitwange, Choga na Masha. Mengine baadaye, msimulizi yuko bize

Mkuu Halisi
Asante kwa kutujuvya
 
John malecela sio msafi hawezi kukemea uchafu. Hataki kufa kwa presha, hawa wazee wa dampo wanajuana vizuri sana.Labda kwasababu sasa wana kambi ila si dhani kama atapenda mishale irudishwe kwake. lets wait and see.
 
Which reminds me, aliwahi kuwajibu watu waliokuwa wanalalamikIa usafiri wa kwenda Kigoma miaka ya 80 alipokuwa waziri wa mawasiliano kwamba "THEY CAN GO TO HELL", na sisi tumjibu hivyohivyo ?
 
Kwani Tingax2 yuko kambi gani? Tukijua kambi yake itasaidia kuelewa alikuwa anamaanisha nini,maana kwa siasa za sasa hasa ndani ya CCM ni kambi tu ndo zinadetermine msimamo wa mtu (for obviously personal gain), na SIO maslahi ya nchi
 
John malecela sio msafi hawezi kukemea uchafu. Hataki kufa kwa presha, hawa wazee wa dampo wanajuana vizuri sana.Labda kwasababu sasa wana kambi ila si dhani kama atapenda mishale irudishwe kwake. lets wait and see.

Hebu jadili hoja usijadili mtoa hoja. Tabia hiyo ndiyo ya OVYO kabisa inayopotosha mada na mara nyingi inatumiwa na watu kama Rostam ambaye baada ya kushindwa katika Dowans sasa akakumbuka kuhusu Power Pool ya Mwakyembe.

Nilishawahi kusema, tusipindishe hoja kwa sababu tu zimetolewa na fulani. Itafika mahali hatutakuwa na hoja kabisaaaa!!!! Maana utataka kujua 'halisi' ni nani, kama ni Rostam basi hana haki ya kusema kuna wezi pale Ubungo Tanesco. Leo hii mimi naamini hata Rostam, Chenge, Jeetu Patel, pamoja na uchafu wao, wana haki ya kuzungumzia uchafu wa wengine lakini wajue hiyo haiwasafishi kwa kuzingatia kwamba maji taka hayaogwi na kuchafua wengine hakuwasafishi na mwizi akikamatwa hata akitaja wenzake haachiwi na pia wasitunge.

Jambo la msingi kwenye mada hii, ni tusiibue hoja za kutungwa alizorushiwa Mzee Malecela na wenzake kama Dk. Salim na wengineo. Najua baada ya hapa watu wataanza kumshambulia ili kumnyamazisha, hawatafanikiwa ng'o!
 
asante halisi......lakini tinga tinga hana jipya.....

......tangu tuhuma za EPA,IPTl na madudu dudu mengine mbona hajasema?

.....leo hili linaivua nguo ccm kaaanza kushupalia.....hana jipya....kama mwananchi namuambia go to hell(kauli yake akiwa waziri)
 
Mzee Malecela kama kawaida yake atakuwa katikati kujaribu kuweka mambo sawa.

Huyu mzee pamoja na kufanyiwa fouls zote na CCM lakini hakupiga kelele za kuonewa.
Sema Malecela ingawa ulishindwa kuonyesha busara wakati wa kuhukumiwa Zitto lakini umekuwa ukimuongoza vema Mkeo(Anna Kilango) Bungeni,pia hukuwahi kulalamika kwa kuhujumiwa mara kadhaa ingawa si vizuri kunyamazia hujuma za kutuletea viongozi wasanii.
 
Malecela alifanya kosa fulani baada ya mchakato wa 2005; alikuwa too royal kwa CCM. Mzee wa watu alifanyiwa mizengwe ya ajabu na CCM wakati ule huku akiwa ndiye mtu pekee aliyekuwa kaijenga CCM ile kwa mikono yake kuliko mtu mwingine yeyote aliyetaka kiti cha urais wakati ule. Jampo alilotakiwa kufanya wakati huo ni kuacha partisanship na kuchukua statesmanship roles zaidi. Leo hii angekuwa anaogopwa na hata akina JK.
 
Nasikia harufu ya kuanguka kwa Jumanne a.k.a John Malecela, mzee upande wowote atakao simama utamlipukia tu. Kwanza kambi yake ni kambi pinzani na mtandao hivyo akisema lolote kuwakosoa watampoteza tena safari hii bila huruma maana jamaa wamejeruhiwa na mai waifu wake. na akijaribu kuwabeba na kujipendekeza wananchi watamtosa bila huruma amuulize Zitto. Kwa sasa watalaam wa kupima upepo huwa kimya na kujifanya wapo busy na mambo ya kimataifa (wapi Salim).

Mzee funika kombe mwanaharamu apite siasa hizi za leo ni WIZI MTUPU

Nakuhakikishia Mkuu Burn, hakuna lolote litakalomtokea J. S. M. endapo atamua kusema ukweli wote. Ukweli ambao atakuwa ameujenga kwa hoja za kutosha. Ukweli wenye mafunzo yanayoaminika na kuheshimika.

Mzee Malecela anaweza kuharibu kama atataka kusema mambo yasiyoaminika, yasiyo na ukweli na ambayo atakuwa ameyajenga kwa nia ya kutetea maslahi ya chama badala ya Taifa au maslahi yake binafsi badala ya Taifa.

Tanzania ya sasa, yaani hapa tulipo sasa, yeyote atakaejiandaa vyema na kuleta matumaini kwa wananchi atakuwa ameshinda. Atakuwa ameshinda hasa na kumshinda yeye itakuwa kazi kubwa.

Kinachotakiwa kwa nchi hii sasa hivi ni kwa Wazee wetu (kama hawa) waliowahi kulitumikia Taifa hili kwa nidhamu na ujasiri, kusema sasa. Kusema bila uwoga wala haya. Wanatakiwa watukumbushe, watuamshe na kutufundisha kuhusu wapi tulipokosea, na njia ya kweli ni ipi. Mzee Malecela ni mmoja wa Wazee hao.
 
Back
Top Bottom