Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Watu wengi hapa Jamii forum wanapenda sana kutumia avatar yenye sura ya Malcom Little AKA Malcom X. Nadhani wanaijua vizuri historia ya mwanamapinduzi huyu aliyefariki dunia mwezi february mwaka 1965 akihutubia ndani ya audubon ballroom New York.
Malcom X alikuwa muuzaji wa dada poa, ambaye pia alikuwa ni jambazi, alikamatwa na kufungwa jela, huko jela ndipo uwezo wake wa kujenga hoja ulipojionyesha. Alipotoka kifungoni akaja uraiani akiwa mwanaharakati wa hatari. Historia yake mbaya huko nyuma haikuwa sababu ya yeye kutokuwa na mchango chanya kwa jamii inayomzunguka.
Wanasiasa wengi sana wanapozizungumzia historia zao, huelezea matatizo mengi waliyokabiliana nayo, ambayo yalichangia katika kutengeneza uwezo wao wa uongozi.
Nadhani badala ya watu kumnyooshea mtu kidole kwa sababu siku za nyuma aliwahi kuwa mtu wa aina mbaya machoni mwa watu, kilicho muhimu ni kutazama nafsi yake ina kipi chema kwa ajili ya kizazi cha leo na kile cha kesho na keshokutwa. Waafrika tunapenda sana hii tabia ya kumnyooshea mtu kidole na kuongelea udhaifu wake ambao pengine ni asilimia 0.001 kulinganisha mema anayoyafanya leo kwa faida ya mamilioni ya watu.
Kwa kuitazama historia ya Malcom X aliyekuwa pimp wakati wa ujana wake, asingeweza kupewa heshima ya kuhutubia chuo kikuu cha Oxford. Dunia inamkumbuka Malcom X aliyewapa kiburi cha kujiamini watu weusi kote duniani wala haina muda na yule aliyekuwa akikesha kwenye madisco ya New York.
Dunia itamkumbuka Barrack Obama aliyeongoza Marekani kwa vipindi viwili wala haitamkumbuka yule aliyevuta ganja akiwa hostel na wanafunzi wenzake. Watanzania tujifunze kuyaweka maisha ya wanasiasa wetu kwenye mizani sahihi. Tunapomaliza kuwanyooshea vidole kwa sababu ya kashfa za udhaifu wao, tukumbuke kuangalia lengo zuri la nafsi ambalo huishi milele.