Malawi yakataa kudharauliwa na Jakob Zuma

Malawi yakataa kudharauliwa na Jakob Zuma

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,308
Serikali ya Malawi imeghadhabishwa na matamshi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob ZUMA yaliyoonekana kudharau MIUNDOMBINU nchini Malawi.

Malawi sasa imemtaka balozi mkuu wa Afrika Kusini nchini humo kuelezea matamshi ya kusikitisha yaliyotolewa na Rais Jacob Zuma
kuhusu nchi hiyo.

Balozi huyo, Cassandra Makone alitakiwa na serikali ya Malawi kufafanua matamashi ya Zuma yaliyotafsiriwa na wengi kumaanisha
kuwa Malawi bado iko nyuma sana alipokuwa anazungumzia miundombinu ya Afrika Kusini.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Quent Kalichero aliambia shirika la habari la AFP kuwa Makone aliitwa na serikali ili kueleza
alichomaanisha Rais Zuma.

Balozi huyo alifanya mkutano na afisaa mkuu katika wizara ya mambo ya nje George Mkondiwa ingawa Kalichero inaarifiwa alikataa kutoa maelezo ya mkutano.

Mnamo siku ya Jumatatu, Zuma alizua utata alipokuwa anawashawishi madereva wa nchi hiyo kukubali kutozwa kodi za barabarani mjini Johannesburg.

''Tuko mjini Johannesburg, na hii ni Johannesburg. Sio kama barabara ovyo ya kitaifa nchini Malawi,'' alinukuliwa akisema Zuma.

Hata hivyo msemaji wa Zuma Mac Maharaj alisema kuwa taarifa hiyo ilitafsiriwa visivyo.

Aliongeza kuwa Zuma alikuwa tu anasisitiza kuhusu mfumo mzuri wa barabara Afrika Kusini ikilinganishwa na nchi zengine katika kanda yaAfrika Kusini.

Hata hivyo, Maharaj aliomba radhi kwa matamshi hayo akisema kuwa watu wengi wameghadhabishwa nchini Malawi.

chanzo: BBC.

JE WATANZANIA NA WAPENDA UKWELI ZUMA YUKO SAHIHI AU AMEKOSEA?
UTAMADUNI WA KUKUBALI UKWELI MBONA NI MGUMU KWA AFRICA?
HUKU KWETU UKISEMA UKANDA FULANI SI KAMA ULE KIMAENDELEO NI UBAGUZI ILA YAWEZA KUWA NI UKWELI.
KUSEMA UKWELI YAWEZA LETA UADUI TUJIHADHARI!!
 
Malawi na jamani ni nchi ya hata kuizungumzia? Ni afadhali hata ya Haiti kuliko Malawi. Hii Malawi ni choka mbaya sana kama Bangladesh
 
Huyu bi Joyce amegeuka mtetea sasa,kila jogoo asiye na interest naye anamwona mwewe tu!
 
Malawi enzi za utawala wa makaburu SA walikua upande wa Makaburu, labada kabifu bado kapo kwa Mbali.!!
 
Kwa sababu madereva hao walipotakiwa kulipa ushuru wa barabara za A. Kusin walisema huko Malawi walikopita hawalipii Ushuru.

oooh kumbe? yaani wao wamefika nchi za watu halafu wakaleta jeuri? so Zuma alikuwa anawaambia madereva wa A Kusini wasiwe kama wa Malawi sio?
 
Haha ha haaa .Duh nimecheka sana.Lakini Zuma nae alikua undiplomatic.Hakuchagua Maneno.Kulikua nahaja gani ya kusizitiza point yake kwa kufanya negative reference kwa nchi nyingine

Hana Tofauti na Ehud Barack alipofanya reference mbaya kwa Tanzania

Hata hivyo huyo Kibaraka Joyce aimarishe Miundombinu kuliko kutafuta sympathy ya wananchi wake
 
This is what Zuma said;
"We can't think like Africans in Africa, generally
We are in Johannesburg. This is Johannesburg
It's not some national road in Malawi"

My take: Those remarks are a challenge to other African leaders. I say so because Swaziland is said to be one of the poorest countries in the world but they have got really nice roads it's as if you are driving on South African roads, the roads between Manzini and Mbabane. It's not something that I've read! I've seen them

On the other hand those remarks show how stupid black South Africans are. I've always asked them if they would have been able to acquire that level of development had it not been for whites. A fellow blackman looking down on another because is from another African country
 
haha ha haaa .duh nimecheka sana.lakini zuma nae alikua undiplomatic.hakuchagua maneno.kulikua nahaja gani ya kusizitiza point yake kwa kufanya negative reference kwa nchi nyingine

hana tofauti na ehud barack alipofanya reference mbaya kwa tanzania

hata hivyo huyo kibaraka joyce aimarishe miundombinu kuliko kutafuta sympathy ya wananchi wake

mkuu wasiseme ukweli???
 
Kuna ukweli kwa matamshi ya Zuma. Kwa mfano ukitoka Jburg kwa ndege kuja Tanzania, Uwanja wetu wa ndege wa Dar-JKN waweza kuulinganisha na kakijiji fulani ka Wafugaji wa kimasai! Tofauti kubwa sana.
 
Yesterday Walter Bigoya, a writer from Mkuki na Nyota publishers, was a guest on one of SA FM shows. He was invited to talk about Successes of African liberation. He also bashed black South Africans on the aspect of xenophobia. Well done, baba!
 
Kuna ukweli kwa matamshi ya Zuma. Kwa mfano ukitoka Jburg kwa ndege kuja Tanzania, Uwanja wetu wa ndege wa Dar-JKN waweza kuulinganisha na kakijiji fulani ka Wafugaji wa kimasai! Tofauti kubwa sana.

Kaka na wewe unaulinganisha uwanja wetu wa mwewe na viwanja vya watu kweli!!??, Niliwahi kutua na mgeni wangu hapo wakati ndio tu nakaribia kutua akaniuliza kama kuna Simba au Twiga alipoona minazi iliyojazana kule kiwalani wakati tukiwa angani.
 
Kuna ukweli kwa matamshi ya Zuma. Kwa mfano ukitoka Jburg kwa ndege kuja Tanzania, Uwanja wetu wa ndege wa Dar-JKN waweza kuulinganisha na kakijiji fulani ka Wafugaji wa kimasai! Tofauti kubwa sana.

Kuna wale Wa Jumuia yetu ya EAC ya kaskasni walisema wakipewa Bandari ya Dar Ni miezi 6 dar inakuwa kama Dubai. Hata sisi tulilalamika kudharauliwa kwani ule pia ni Ukweli?
 
Kaka na wewe unaulinganisha uwanja wetu wa mwewe na viwanja vya watu kweli!!??, Niliwahi kutua na mgeni wangu hapo wakati ndio tu nakaribia kutua akaniuliza kama kuna Simba au Twiga alipoona minazi iliyojazana kule kiwalani wakati tukiwa angani.
Punguza ulimbukeni!
 
Punguza ulimbukeni!

Mie limbukeni kaka,lkn huo ndio ukweli uwanja wa ndege hatuna ukilinganisha na vya wenzetu. Kama hujatembea kwa wengine ukaona viwanja vyao utakuwa sahihi kuniita limbukeni, lkn kama umetembea kama nilivyotembea mimi kuona viwanja vya wengine utakuwa haupo sahihi kuniita limbukeni, maana utakuwa unajua ukweli ila unataka kuubadilisha tu kuwa uadui.mchana mwema mwerevu.
 
This is what Zuma said;
"We can't think like Africans in Africa, generally
We are in Johannesburg. This is Johannesburg
It's not some national road in Malawi"

My take: Those remarks are a challenge to other African leaders. I say so because Swaziland is said to be one of the poorest countries in the world but they have got really nice roads it's as if you are driving on South African roads, the roads between Manzini and Mbabane. It's not something that I've read! I've seen them

On the other hand those remarks show how stupid black South Africans are. I've always asked them if they would have been able to acquire that level of development had it not been for whites. A fellow blackman looking down on another because is from another African country

Jamaa ametupasha wote,na hii ni kawaida ya wa SA hasa weusi kujiona bora na nchi yao siyo sehemu ya umasikini wa bara la Afrika. Wageni toka mataifa jirani ya SA na barani Afrika watanyanyasika mara kizazi cha viongozi walioshiriki vita ya ukombozi kitakapo ondoka madarakani!
 
Back
Top Bottom