cheichei2010
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 932
- 350
Our leaders on this one are more of opportunists than people with a genuine desire to protect our territorySwali langu ni kuwa, why this argument comes now? The lake was there for generations, why raising interest now? Who saw the opportunity of winning which triggered the argument?
Kujenga hoja ni kitu gani katika suala hili? Tanzania inadai sehemu ya Ziwa hilo, na hilo ni jambo la kihistoria kama ilivyokuwa mikataba ile ya wakoloni. Wakazi wa Tanzania walio kando ya Zia Nyasa wamekuwa wakiiishi kwa kulitumia na kulitegemea ziwa hilo kiuchumi na kijamii...na wao wanajua hilo ziwa kwa urefu wa matumizi yao, ni lao.
Kwahiyo, Tanzania ina haki ya Ziwa hilo, hata bila ya kuwa na Takwimu zozote, kwakuwa kuna watanzania wanaishi na kulitumia ziwa hilo kila uchao. Wamalawi, ni kweli wamejiandaa, na wanaweza kuwa na hoja nzito katika kuwakilisha utetezi wao!! Tanzania tumeingia kichwa kichwa baada ya wamalawi kuanza kulitumia ziwa hili kibiashara zaidi..na kudai lote ni mali yao. Sasa tuka react...hatukutengeneza facts za kutosha labda. Lakini fact kubwa ambayo watanzania tunapaswa kuipigania..ni watu wetu wanaoishi kando kando ya ziwa liwe..ambao maisha yao yote na ya vizazi vyao vyote..wamelitumia na kulitegemea.
Unadhani Membe hajui? Anababaisha tu ili tusijue ukwelitatizo kubwa ni kwamba hatuji tunachodai katika ziwa hilo...membe bwana
Nilikuwa Malawi na naomba nitoe maoni yangu hivi:
Kwanza hapa naona watu wanamshambulia Membe wakati timu ilikuwa ni Tibaijuka na timu yake!
Wizara ya Maji na akina Membe na timu yake na Tibaijuka na Rutabanzibwa waliwabana sana na hasa Ruta ambaye alisifiwa sana kuwa na uwezo mkubwa sana kuwabana katika vikao vya awali kabla ya mawaziri kukutana.
Halafu ukisoma hata hiyo story yao, utaona tumewabana hadi wakakubali kuacha kufanya utafiti.
Tanzania imesema wazi kwamba mpaka ni katikati ya ziwa na kwamba Mkataba wa Heligoland Kifungu namba 6 kinataka nchi zijadiliane kuhusu mpaka na si kama ilivyo kwenye mkataba husika na kwamba hayo yamefanyika katika maeneo mengine except Malawi and Tanzania.
Na pia nitaambatanisha ramani ambayo Tanzania imewabana nayo.
Lkini pia, sisi Watanzania na vyombo vyetu tukatae kutumika kwa maslahi ya wengine tuwe na Utanzania.
Na pia nitaambatanisha ramani ambayo Tanzania imewabana nayo.
Lkini pia, sisi Watanzania na vyombo vyetu tukatae kutumika kwa maslahi ya wengine tuwe na Utanzania.
Labda wampe Tundu lissu matokeo tungeyaona lakini huyu jamaa anayeweka mikono mifukoni tumekwisha
...Wameshagundua jamaa ni DHAIFU hivyo wanahisi labda hana ubavu wa kutetea mipaka ya nchi. Thubutu uchezee mipaka ya Tanzania wakati wa Mwalimu...Alikuwa anatoa kauli yake na anaisimamia mtindo mmoja bila woga. Na yeyote aliyejaribu kuchezea mipaka ya Tanzania aliposikia kauli ya Mwalimu alijua huyu jamaa hana msalie mtume yuko tayari kwa lolote lile...siye huyu anatoa kauli eti wanaotaka vita ni vyama vya upinzani!!!! Sijui tangu lini Membe na Lowassa wamekuwa kwenye vyama vya upinzani.
Tanzania haiwezi ku-negotiate haki ya ziwa Nyasa kwa kutumia Anglo-German contract halafu wakatarajia kushinda. Hili haliwezekani. Wanachojaribu kufanya ni sawa na ku-negotiate matumizi ya maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract. Haiwezekani Tanzania ikashinda. Ndo maana Malawi wao watatusukumia huko!
Ni kweli kuwa tutakuwa tumekubaliana kwenye umoja wa Afrika kuwa mipaka ya wakoloni inasimama kama ilivyo, lakini si bila exception. Kuna maeneo ambayo mgawanyo wa wakoloni hauwezi kuheshimiwa kwa sababu za kibinadamu. Je tulisaini kwenye umoja wa Afrika tukiikubali mipaka ya wakoloni bila exception?
Exception zilikuwepo na ndo maana Mwalimu Nyerere alitamka kuwa hili halikubali. Sasa tukishakubaliana kuwa hatujakubaliana kuwa tutaheshimu mipaka ya wakoloni bila exception turudi kwenye ukweli sahihi. Tanzania na malawi zimetenganishwa na ziwa Nyasa (call it Malawi, or Kamuzu; it doesn't matter). Ukweli ni kuwa walioko ng'ambo ya kule ni wamalawi, walioko ng'ambo ya huku ni watanzania; hapo ndo pakuanzia.
Malawi inapata haki kwenye ziwa kwanza kwa sababu mikataba ya wakoloni inasema hivyo; lakini pili kwa sababu kuna wamalawi wanaishi hapo karibu na ziwa for Generations. Haki ya Tanzania kwenye ziwa hili haitokani na mkataba wa Anglo German, inatokana na watanzania zaidi ya 600,000 wanaoishi na kulitegemea ziwa hilo for generations. Mkataba wa waingereza na Wajerumani waachieni wamalawi wacheze nao; watanzania tunacheza na haki ya watanzania waliopo hapo kando ya ziwa - na ikilazimika tutaenda vitani kwa ajili ya kulinda haki ya watanzania hao kulitumia ziwa hilo kama lao, si la kuazima; kwa sababu wajerumani na waingereza walipokubaliana hawa watanzania hawakuhusishwa!
Chochote tulichokubaliana huko nyumba; ambacho kinawanyang'anya maelfu hayo ya watanzania haki ya kutumia ziwa Nyasa kama lao; hakina uhalali wowote! Suala la kuwa watanzania wamesema 50/50 au sijui latitude ngapi na ngapi halina maana yoyote! Chenye maana ni haki ya watanzania kulitumia ziwa hilo kama lao - si la kuazima katika maeneo yote ambayo wapo!
Sasa suala itakuwa watanzania wanalitumia ziwa kama lao hadi wapi? Hilo ndo la kujadiriana na watu wa malawi; kwa sababu na wao wanalitumia ziwa. Na iwe wazi kuwa watanzania hawako tayari kujadiri umiliki wa ziwa Nyasa; Watanzania wako tayari kujadiri umiliki wao wa ziwa unaishia wapi? Hili ndo inatakiwa twende nalo mbele.
Kamwe tusijadiri haki ya kutumia maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract; hatutashinda! Madai ya Malawi hata kama kwa logic yanaonekana ni ya kizandiki; lakini yako backed na documents. Na kwa wamalawi uhalali wa hizo documents hauko questionable.
Eneo tulilopigania na Waganda (Amin) ni dogo sana kuliko eneo lote la ziwa Nyasa linalohusisha idadi ya watu wanaokaribia milioni moja.
Kusema ukweli vita huwa ni "a necessary evil" ndo maana wamarekani wanatumia sehemu kubwa ya GDP yao kujiandaa na kupigana vita. Baadhi ya vita huwa ni ya lazima. Ikilazimika Tanzania inabidi iende vitani kupigania maslahi ya watanzania wapatao millioni moja wanaoishi na kutegemea ziwa nyasa for Generations ambao leo hii wanaambiwa si lao sababu tu kumeonekana uwezekano wa kupatikana humo mafuta na Gesi!