Malawi, Tanzania fail to agree on Lake Nyasa border dispute

And I quote "Attorney generals to evaluate 1890 treaty".. Hapo ndipo watanzania tutakapopigwa bao! Huyu werema ataweza kweli, maana jamaa anaonekena ni kilaza mkubwa kweli.
Tujiandae kupoteza iwapo tutalazimika kukubaliana na maamuzi ya kidiplomasia na kisheria
 
Membe amesema kuna mambo mawili (2 issues) ambayo wameshindwa kuelewana. Tungependa kuyafahamu hayo mambo mawili ili tutoe inputs zetu kwa ajili ya kukinusuru kipande hicho muhimu cha nchi yetu.
 
Nilishauri hapa hapa kuwa CDM watuwakilishe kwenye mazungumzo nikaonekana mnazi. Sasa hawa DHAIFU wamepoteza muda na resources kujadili hoja za Malawi badala ya kupeleka hoja zao. Ukienda kwenye negotiations na defensive position umekwisha, ndo ivyo tena kazi imebakia kwa Werema ku-Stamp ziwa kuwa la malawi lote
 
Safi,
Naomba uweke hiyo ramani, pia watu wengi humu hawajui kuwa Membe na Chiume ni wanasiasa watao matamko tu na si wataalam wa hayo mambo. Kazi yenyewe inafanywa na watu wengine...:hat:
Ramani iliyotolewa na timu ya Tanzania ikiongozwa na Membe na Tibaijuka & wataalamu wao Patrick Rutabanzibwa na John Haule na Kiongozi wa wanasheria D. Chidowu; walikuwapo wataalamu wa Wizara ya Maji.

Ukisoma mazingira, Wamalawi wametishika na Chiume alisema "Tunataka haya mambo yaishe haraka ili tufanye mambo yetu bila woga" that means wana woga na ndio maana wamekubali kuasitisha kufanya utafiti.

Timu ya Tanzania ikiyoenda iliwatisha pia maana imeonakana Tanzania tuko serious kwa sasa tofauti na mwanzo. Mwanzo tuliona hawa ni wenzetu tukawavumilia, sasa tuko makini!

attachment.php
 

Attachments

  • tz-map.jpg
    tz-map.jpg
    94.8 KB · Views: 456
Halafu ukisoma hata hiyo story yao, utaona tumewabana hadi wakakubali kuacha kufanya utafiti.
Pamoja na kwamba mkuu ulikuwepo huko naomba kutofautiana na wewe kwenye hilo.

Hilo lilikuwa ni ombi la Membe.

Katibu wa wizara ya Mambo ya Nje Malawi amesema hilo ombi litajadiliwa kwenye baraza la mawaziri na amegusia ugumu wake kwa kusema linakiuka masharti ya mkataba wao na kampuni ya utafiti wa mafuta
 
And I quote "Attorney generals to evaluate 1890 treaty".. Hapo ndipo watanzania tutakapopigwa bao! Huyu werema ataweza kweli, maana jamaa anaonekena ni kilaza mkubwa kweli.


Una maana huyu jamaa yetu anayetumia kichwa chake kufuga nywele?
 
paulss, points zako ni zenye ukweli unaouma kwa Mtanzania yeyote yule nikiwemo mimi. Hapa tunahangaishwa na kosa lililotengenezwa na ubabe wa Nyerere. Naelewa ni vigumu kuamini na inauma lakini huo ndio ukweli. Kwanza, hata kama mpaka ungekuwa unapita katikati, haiwezekani mtu mwenye akili zake timamu kusema Tanzania tunamiliki 50% ya lile ziwa. Ukijaribu kupitia tu ramani upya utaona hata kama mpaka ungekuwa unapita katikati, basi Tanzania tutamiliki sehemu isiyozidi 30% au 20% kwani kusini zaidi ni sehemu ya Msumbiji harafu ukiangalia kule mwisho kabisa unaona liko ndani ya ardhi ya Malawi. Hili ni moja tu ambalo halihitaji utaalam wa aina yeyote ile. Pili, ni kuwa wenzetu wanayo treaty kama msingi wa kile wanachokiamini na sisi tunazo hoja kabambe zilizokosa ushahidi wa treaty (Makubariano).

Nimetanguliza kusema kuwa tunahangaika na ubabe uliotengenezwa na Nyerere kwasababu yeye aliyajua haya (treaty). Na alielewa kuwa hata mipaka yetu na nchi nyingine kama vile Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, DRC n.k. ni ile iliyotengenzwa kupitia treaties kama hizi, yaani, mikataba ya wakoloni ila badala ya kutafuta ufumbuzi kwa kuzungumza na mwenzake Banda, Nyerere akatumia ubabe na kutuaminisha watanzania kuwa duniani hakuna mtu mpumba.. kama Banda huku akitudanganya kwakusema Tanzania haitafungwa na mikataba ya wakoloni. Iweje isifungwe na mikataba ya wakoloni inapotokea hali ikawa mbaya kwa upande wetu na ikafungwa na mikataba ya wakoloni hao hao inapotokea hali ikanoga kwa upande wetu (kama tulivyowaminya Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda mpaka tukawa na eneo kubwa linalozidi ukubwa wa nchi hizi zote nne zikiunganishwa)?

Napenda nirudie wazo nililolitoa huko nyuma kuwa nikiwa mmoja kati ya watanzania wanaofaidika na rasilimali za ziwa nyasa, ni bora viongozi wetu wakajikita katika kijadili mbinu zakutufanya watanzania wa eneo hilo tuendelee kunufaika na rasilimali hizo. Wapo wanaoshabikia vita ila pengine watanzania wa aina hiyo wanatoka mikoa ya mbali na ziwa nyasa. Mimi siishabikii kwani natokea vijiji ambavyo vitabadilika kuwa battle ground kama vita itatokea. Tutapoteza wazee wetu wakati huo mtu wa Mara yupo kwake na wala hajuwi kuna vita vinaendelea upande wa kusini mwa Tanzania.

Mungu Ibariki Afrika! Mungu ibariki Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
Sawa lakininni lazima kuwe na basis ya kukataa mikataba na katika hili msimamo wa Tanzania hautokani tu na watanzania wote uliowataja kusihinkaribu na ziwa. Ukweli ni kwamba mikataba hiyo haikuwa na nguvu ya kisheria pale serikali yetu ilipotamka kutoitambua na kutozingatia masharti ambayo Mwalimu aliyatoa mara baada ya kupata uhuru.

Tunakubaliana kuwa uhalali wa mikataba ile wa Tanzania hatuikubali "wholesale", yaani kuna maeneo tuliona hayako sawa tukayakataa na tukaweka msimamo wetu.

Sasa hili lilopo kwenye article linaashiria kuwa actually tunajadiriana based on hiyo hiyo mikataba. Inaonekana labda team yetu imeshaona loop holes kwenye hiyo hiyo mikataba na inataka iwakaange wamalawi kwa mafuta yao?

Hiyo ramani uliyoiweka si ndo ile ya Waingereza ambayo baadaye waliimodify tena??
 
@ Paulss, points zako ni zenye ukweli unaouma kwa Mtanzania yeyote yule nikiwemo mimi. Hapa tunahangaishwa na kosa lililotengenezwa na ubabe wa Nyerere. Naelewa ni vigumu kuamini na inauma lakini huo ndio ukweli. Kwanza, hata kama mpaka ungekuwa unapita katikati, haiwezekani mtu mwenye akili zake timamu kusema Tanzania tunamiliki 50% ya lile ziwa. Ukijaribu kupitia tu ramani upya utaona hata kama mpaka ungekuwa unapita katikati, basi Tanzania tutamiliki sehemu isiyozidi 30% au 20% kwani kusini zaidi ni sehemu ya Msumbiji harafu ukiangalia kule mwisho kabisa unaona liko ndani ya ardhi ya Malawi. Hili ni moja tu ambalo halihitaji utaalam wa aina yeyote ile. Pili, ni kuwa wenzetu wanayo treaty kama msingi wa kile wanachokiamini na sisi tunazo hoja kabambe zilizokosa ushahidi wa treaty (Makubariano).
Kumbe mkuu hapa tatizo ni Semantics.Mtoto wako alikupa chungwa nusu. Tukaonana njiani nikasema....ebwana ee pasu kwa pasu hilo chungwa. Sitakuwa sahihi kisarufi/maana?

@ Paulss, Nimetanguliza kusema kuwa tunahangaika na ubabe uliotengenezwa na Nyerere kwasababu yeye aliyajua haya (treaty). Na alielewa kuwa hata mipaka yetu na nchi nyingine kama vile Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, DRC n.k. ni ile iliyotengenzwa kupitia treaties kama hizi, yaani, mikataba ya wakoloni ila badala ya kutafuta ufumbuzi kwa kuzungumza na mwenzake Banda, Nyerere akatumia ubabe na kutuaminisha watanzania kuwa duniani hakuna mtu mpumba.. kama Banda huku akitudanganya kwakusema Tanzania haitafungwa na mikataba ya wakoloni. Iweje isifungwe na mikataba ya wakoloni inapotokea hali ikawa mbaya kwa upande wetu na ikafungwa na mikataba ya wakoloni hao hao inapotokea hali ikanoga kwa upande wetu (kama tulivyowaminya Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda mpaka tukawa na eneo kubwa linalozidi ukubwa wa nchi hizi zote nne zikiunganishwa)
Toa reference wapi Nyerere amesema Tanzania haitafungwa na mikataba ya kikoloni

Nijuavyo mimi Nyerere ndo alikuwa mhasisi wa kipengele cha 0AU charter kinachotaka nchi wanachama kuheshimu mipaka iliyoachwa na wakoloni.

Uzalendo wako upo wapi, mkuu
 
Swali langu ni kuwa, why this argument comes now? The lake was there for generations, why raising interest now? Who saw the opportunity of winning which triggered the argument?
There is a high potential of oil and gas below the waters of the lake. It has been noted recently after preliminary explorations of the same hence this argument now. Naamini Wamalawi hawana muda wa kuwazuia Watanzania wasivue samaki wala kunywa maji ya ziwa hilo, cha msingi kwao ni mafuta na gesi yote ni yao!
 
Ramani iliyotolewa na timu ya Tanzania ikiongozwa na Membe na Tibaijuka & wataalamu wao Patrick Rutabanzibwa na John Haule na Kiongozi wa wanasheria D. Chidowu; walikuwapo wataalamu wa Wizara ya Maji.

Ukisoma mazingira, Wamalawi wametishika na Chiume alisema "Tunataka haya mambo yaishe haraka ili tufanye mambo yetu bila woga" that means wana woga na ndio maana wamekubali kuasitisha kufanya utafiti.

Timu ya Tanzania ikiyoenda iliwatisha pia maana imeonakana Tanzania tuko serious kwa sasa tofauti na mwanzo. Mwanzo tuliona hawa ni wenzetu tukawavumilia, sasa tuko makini!

attachment.php

Bwana n00b,

Hebu acha kudanganya na unatakaiwa kuelimisha. Nimeshasema mara nyingi humu kwamba hii issue ni technical na zinatakiwa technical details kuwatoa nje wamalawi.

Badala yake unakuja humu JF kisha unafanya kama mshabiki wa mpira ambaye Simba anaenda kwenye jukwaa la Simba sasa unatarajia hapo atangaze sera gani. Definitely atatangaza mazuri ya Simba ili apigiwe makofi.

Ndicho mnachikitafuta nyinyi baadhi yenu humu ikibidi mpate kuambiwa mna uzalendo lakini mkijua hakuna ukweli unaotosheleza.

Sasa, unaleta ramani kama uthibitisho. Toka lini ramani iliyochorwa ikafuta agreement iliyo-set ule mpaka. Acheni kubabaika baada ya matokeo ambayo mimi kwa point kama hizi sikuwa na wasiwasi hata kidogo nilijua Tanzania tutatolew nje tu na hata hiyo September jiandaeni kuleta porojo kama hizihizi lakini ukweli ni kwamba tanzania haitaweza kupata hata tone moja la ziwa Malawi kwa hoja hizi finyu.
 
Bwaga ya moyoni;

Inawezekana 50 - 50% inawachanganya watu wengi hapa jamvini. Mimi nilivyoelewa ni hivi: ipo sehemu ya nchi kavu ya Tanzania na pia ipo sehemu ya nchi kavu ya Malawi halafu kati ya hizo nchi kavu lipo ziwa Nyasa (Ki Kwetu) au ziwa Malawi (Ki Kwao) badala ya mpaka kuwa pale ukingo wa Mashariki mwa ziwa hilo kama wanavyodai Wamalawi wakisaidiwa na Heligoland Zanzibar Treaty; sisi tunadai mpaka uwe pale katikati ya ziwa kutenganisha nchi ya Malawi na Tanzania kama tulivyofundishwa na walimu wetu na hiyo ndiyo maana ya 50 - 50% siyo 50% ya ziwa lote. Hata Malawi wanaposema wanamiliki 100% haimaanishi ziwa lote bali kati yetu na wao sisi hatuna chetu!
 
Last edited by a moderator:
watanzania wanaongea nini wakati malawi wanachonegotiate ni kuwafanya wabongo waridhie tuu,kwani tayari wao wanaamin kuwa ziwa ni 100% kwa upande wa TZ ila sijui kwanini na mOzambique wasifanye hivyohivyo?
 
Nilikuwa Malawi na naomba nitoe maoni yangu hivi:

Kwanza hapa naona watu wanamshambulia Membe wakati timu ilikuwa ni Tibaijuka na timu yake!

Wizara ya Maji na akina Membe na timu yake na Tibaijuka na Rutabanzibwa waliwabana sana na hasa Ruta ambaye alisifiwa sana kuwa na uwezo mkubwa sana kuwabana katika vikao vya awali kabla ya mawaziri kukutana.

Halafu ukisoma hata hiyo story yao, utaona tumewabana hadi wakakubali kuacha kufanya utafiti.

Tanzania imesema wazi kwamba mpaka ni katikati ya ziwa na kwamba Mkataba wa Heligoland Kifungu namba 6 kinataka nchi zijadiliane kuhusu mpaka na si kama ilivyo kwenye mkataba husika na kwamba hayo yamefanyika katika maeneo mengine except Malawi and Tanzania.

Na pia nitaambatanisha ramani ambayo Tanzania imewabana nayo.

Lkini pia, sisi Watanzania na vyombo vyetu tukatae kutumika kwa maslahi ya wengine tuwe na Utanzania.

Mkuu,

Kama ulikuwa Malawi basi hapo kwenye RED inaonyesha timu mliyokuwa huko mlivyo wababaishaji.

Hebu tujadili hoja yako ambayo asiye mchambuzi atadanganyika kudhani ni ya msingi. Unasema kwamba article 6 ya Heligoland-1890 iliacha nchi zijadili kuhusu mipaka. Halafu next statement yako unasema Tanzania inaamini mpaka ni katikati.

Sasa hapa ndipo kwenye uongo wako. Nili lini ilijadiliwa kwamba mpaka wetu uwe katikati na kukubaliwa na sisi na wenzetu walioko upande wa Malawi? Hatujajadili hata siku moja. Sasa utasemaje mpaka uko sehemu gani wakati hukuujadili kama ulivyotakiwa na treaty.

Hivyo conclusion ya ukatikati wa mpaka iko vichwani mwenu tu lakini hamkuwahi kui-excecute popote na ndiyo maana mnaleta ushahidi wa ramani badala ya mkataba.
 
Tatizo tulilonalo Watanzania ni kupenda kurukia mambo tusiyokuwa na utaalamu nayo,hivi hao watu waliliwakilisha Taifa huko katika majadiliano wameshindwa na timu ya Malawi? Mbona watu wote huko ni mabingwa na wasomi wenye kuheshimika hapa nchini? Kwanini wasipewe nafasi ya kufanya kazi zao za kitaalamu. Hivi kila anayeishi chuo kikuu naye ni msomi wa chuo kikuu?

Wacheni lawama za kukatishana tamaa hii nchi ni ya kwetu wote si ya wanasisa tu na wapenda vita la hashaa bali ni sisi wote wapenda amani na haki pia. Hivi nani kasema ya kwamba Tanzania imeshindwa katika mzozo wa mpaka na malawi, watu wanaacha mambo ya muhimu wanajadili upuuzi; hatufiki popote kwa kuhamasisha ugonvi na kuwatoa thamani wale waliyotumwa na serikali katika kuangalia njia bora ya kumaliza mgogoro huu. Hata ikiwa waliyokwenda huko ni mbumbumbu ndiyo waliyopo na wampewa jukumu hilo la uwakilishi, wewe mjuzi wa kila kitu uko wapi? mbona hutoki ukasikika unawadharau mawaziri kisa hawatoki upande wako,mnamvunjia heshima mkuu wa nchi kisa kawapa uhuru wa kujieleza mitandaoni nini hii,punda kakusaidia kuubeba mzigo na bakora unampiga bila huruma,akisusa mzigo wako hata kuusogeza huwezi. Acheni hizo; Watanzania wenzenu hawalali kwa kufanya kazi zenu, malipo yao hayalingani na kazi zao, nyiye kazi yenu lawama tu, JWTZ na wengineo wanaishi porini kama ndezi kisa nyinyi mlale vizuri na familia zenu halafu ikiamuliwa vita mstari wa mbele wewe mtu wa lawama hata mustin ya chakula huwezi kuibeba kuileta mstari wa mbele ya nini lawama na kutaka vita.

Tembelea vituo maalum uone jamaa waliyoathirika 78 kisha omba ndugu yako akapigane vita, wewe umsubiri kama akirudi salama lakini ana kilema kikubwa hujawahi kukiona yaani kwa kumuonea huruma unatamani bora angekufa hukohuko, siyo mtu bali ni mzigo hajafa na hawezi kutupwa. Basi waacheni wenye ujuzi wao wafanye kazi zao tusubiri matokeo lisilobudi hutendwa kwa uchungu mkubwa vita liwe wazo la mwisho na hata mwalim JK angekuwepo angeona busara kuzungumza kuliko washabiki wanavyoona kwa jicho la kengeza.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika.
 
And I quote "Attorney generals to evaluate 1890 treaty".. Hapo ndipo watanzania tutakapopigwa bao! Huyu werema ataweza kweli, maana jamaa anaonekena ni kilaza mkubwa kweli.

Maana yake ni kwamba hapo hakuna cha UN Water law of 1982 maana Tibaijuka anaijua sana imemgombanisha na wazanzibar na kama alijaribu kuisema hapa kwenye issue ya Malawi basi maana yake amebwaga manyanga haitumiki humu.

Helgiland treaty maana yake is there to stay. Huna jinsi na iwe hivyohivyo kama tulivyoonya mapema humu.
 
ngoja tuone hiyo september meeting, ila sioni kama kutakuwa na jipya sababu malawi wameshatuweka mtegoni kwa kusema wanasheria wakuu wa serikali wakutane kuupitia mkataba wa 1890, kwa nini wapitie mkataba huo pekee ili hali kila mtu anajua hauipi favour tz kisheria?

Kwani mkataba Heligoland treaty ni ya Malawi tu au ilisainiwa kwa maeneo mengi.
 
kwa hiyo bwana n00b kwa mujibu wa ramani hiyo hao ndipo kuna latitude 9 mpaka 11?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom