Malawi, Tanzania fail to agree on Lake Nyasa border dispute

Tukisema Nyerere alikua Raisi bora,wenye hoja nyepesi nyepesi na za udini,wata lipuka na kutapatapa.Swali ninalojiuliza, kwanini hawakuuliza enzi za Mwinyi?Nyerere alikua hai.Kwanini sio mkapa?Mkapa alikua mbabe.kwanini sasa wakati wa JK?Ni dhaifu na msaniii.Inahitajika common sense.Tumetenganishwa na ziwa ndio mpaka, hapo inabidi iwe nusu kwa nusu, vinginevyo walihamishie kwao.
 
Swali langu ni kuwa, why this argument comes now? The lake was there for generations, why raising interest now? Who saw the opportunity of winning which triggered the argument?
Our leaders on this one are more of opportunists than people with a genuine desire to protect our territory

I wouldn't be surprised if Membe views this as an opportunity to get funds to finance campaigns of his bid to get CCM to endorse him as their presidential candidate
 
Kujenga hoja ni kitu gani katika suala hili? Tanzania inadai sehemu ya Ziwa hilo, na hilo ni jambo la kihistoria kama ilivyokuwa mikataba ile ya wakoloni. Wakazi wa Tanzania walio kando ya Zia Nyasa wamekuwa wakiiishi kwa kulitumia na kulitegemea ziwa hilo kiuchumi na kijamii...na wao wanajua hilo ziwa kwa urefu wa matumizi yao, ni lao.

Kwahiyo, Tanzania ina haki ya Ziwa hilo, hata bila ya kuwa na Takwimu zozote, kwakuwa kuna watanzania wanaishi na kulitumia ziwa hilo kila uchao. Wamalawi, ni kweli wamejiandaa, na wanaweza kuwa na hoja nzito katika kuwakilisha utetezi wao!! Tanzania tumeingia kichwa kichwa baada ya wamalawi kuanza kulitumia ziwa hili kibiashara zaidi..na kudai lote ni mali yao. Sasa tuka react...hatukutengeneza facts za kutosha labda. Lakini fact kubwa ambayo watanzania tunapaswa kuipigania..ni watu wetu wanaoishi kando kando ya ziwa liwe..ambao maisha yao yote na ya vizazi vyao vyote..wamelitumia na kulitegemea.

Hoja nzuri sana Mkuu! Bila kujali hilo ziwa ni la Malawi au Tanganyika, la muhimu zaidi ni wenyeji walioko kando kando ya ziwa kwa karne na karne kabla ya huo mkataba wa kikoloni.

Haiingii akilini kwamba mkataba baina ya mabepari wawili huko Ulaya wa kurudishiana visiwa walivyodhulumiana unaweza kukiuka kwa kiasi kikubwa hivyo haki za msingi za binadamu wengine ambao ziwa husika ni urithi wao wa asili; kisa tu wao "wafurahishane" - huu ni zaidi ya wendawazimu. Ndio yale yale ya haturuhusiwi kutumia Nile water ili kuwalinda wamisri eti nao ni mkataba!

Hii ni hoja muhimu sana ya kuisimamia na tukiwa na wajenga hoja wazuri (sio Werema, et al.) hiki kinachoitwa "Heligoland Treaty" kinaweza kuwa nullified na hata wakazi walioishi kwa wasiwasi kwa miaka mingi kutokana na "mkataba" huo wakalipwa fidia. Lakini, je, wajenga hoja tunao? Hili nalo ni tatizo lingine.
 
aliposikia kauli ya Mwalimu alijua huyu jamaa hana msalie mtume yuko tayari kwa lolote lile...siye huyu anatoa kauli eti wanaotaka vita ni vyama vya upinzani!!!! Sijui tangu lini Membe na Lowassa wamekuwa kwenye vyama vya upinzani.[/FONT][/SIZE][/QUOTE]
hivI bado kuna watuwanaodhani kuwa Nyerere alikuwa Saint asiye Na tuhuma mbaya dhidi ya raia wake
 
tatizo kubwa ni kwamba hatuji tunachodai katika ziwa hilo...membe bwana
Unadhani Membe hajui? Anababaisha tu ili tusijue ukweli

Huyo ameshanunuliwa. Cha msingi tuanze kufuatilia mienendo ya hawa wawakilishi pamoja na akaunti zao
 
Eeti tukubaliane? Hawa nikuwapiga tu maziwa yote yapo mipakani zitakuja nchi zingine kuchukua maziwa yao pia! JK anatuua!
 
Mungu wangu, ni diplomasia gani hiyo ambapo mijadala mpaka hivi sasa tuwe tunajadiliana 'ON MALAWIANS OWN CHOSEN TERMS OF THEIR DARLING 1890 TREATY'!!!!!!!!!!

Wakuu sikuu zote mambo katika mijadala wala si muhimu tu kusema eti tayari mko mezani mnajadiliana chochote kitu isipokua ki-ufundi ukishakosea kwenye vipengele vya 'MISINGI' na 'MWELEKEO' wa mjadala wenyewe basi hadi hapo matokeo yote ya nini hitimisho tayari watu mahiri vichwani wanakua wanajua hata kabla ya kufikia robo ya safari zima hilo.

Wakuu hadi hapa ni vema ikaeleweka bayana kwamba Ulinzi wa KILA PUNJE YA MCHANGA, VIUMBE, HEWA NA HEWA YA KILE KINACHOUMBA KITU KINACHOITWA TANZANIA wala si jambo la hiari, usiri wala kukasimiana bali ukweli wa mambo ni kwamba hili ni jukumu letu sote KILA MWANANCHI kulitekeleza kwa udhati kabisa wa moyo na JWTZ wao watatekeleza nao upande wao siku wakiwiwa sawa sawa na hao wanadiplomasia wetu wasioweza kutueleza hata punje ya nini wanachojadi kwa upande wetu.

Nionavyo mimi mpaka hapa, Kaka Denisi Mwamunyange kama vipi sisi wananchi wa kawaida ni bora watu tukakutane tena na nyinyi jeshi letu tukiwa kuleee maili 9 upande wa pili kusini mwa mji wa Mzuzu.

Kikubwa tu ni kwamba kitambulisho chetu kikuu kitakua ni lugha ya Kiswahili kilichonyooka pindi siku utakapoamua maeneo haya KIKAZI na vijana wako.
 
Nilikuwa Malawi na naomba nitoe maoni yangu hivi:

Kwanza hapa naona watu wanamshambulia Membe wakati timu ilikuwa ni Tibaijuka na timu yake!

Wizara ya Maji na akina Membe na timu yake na Tibaijuka na Rutabanzibwa waliwabana sana na hasa Ruta ambaye alisifiwa sana kuwa na uwezo mkubwa sana kuwabana katika vikao vya awali kabla ya mawaziri kukutana.

Halafu ukisoma hata hiyo story yao, utaona tumewabana hadi wakakubali kuacha kufanya utafiti.

Tanzania imesema wazi kwamba mpaka ni katikati ya ziwa na kwamba Mkataba wa Heligoland Kifungu namba 6 kinataka nchi zijadiliane kuhusu mpaka na si kama ilivyo kwenye mkataba husika na kwamba hayo yamefanyika katika maeneo mengine except Malawi and Tanzania.

Na pia nitaambatanisha ramani ambayo Tanzania imewabana nayo.

Lkini pia, sisi Watanzania na vyombo vyetu tukatae kutumika kwa maslahi ya wengine tuwe na Utanzania.
 
Safi,
Naomba uweke hiyo ramani, pia watu wengi humu hawajui kuwa Membe na Chiume ni wanasiasa watao matamko tu na si wataalam wa hayo mambo. Kazi yenyewe inafanywa na watu wengine...:hat:
 
Na pia nitaambatanisha ramani ambayo Tanzania imewabana nayo.

Lkini pia, sisi Watanzania na vyombo vyetu tukatae kutumika kwa maslahi ya wengine tuwe na Utanzania.

Asant sana Mkuu kwa taarifa. Nasubiri kwa hamu sana kuona hiyo kitu hapo kwenye red.
 
Labda wampe Tundu lissu matokeo tungeyaona lakini huyu jamaa anayeweka mikono mifukoni tumekwisha

Hapo kwenye red Mkuu umeniacha hoi!

Hivi kwa nini hili jamaa huwa linaweka mikono huko wakati linaongea? Ni kuongeza kujiamini au ni kitu gani? Umenikumbusha enzi zetu za shule za msingi mambo yakiharibika unaweka mikono mfukoni, nafikri uminisoma au umenifehamu!!!?

Hili li-mjamaa ni legelege hujapata kuona kama watalituma hilo haki ya nani imikula kwetu!! Na hawa jamaa naona wamekubali kwamba basis ya mazungumzo yao iwe kwa kuzingatia mkataba wa 1890, sasa hapo tutachomoka kweli? Mimi nilifikri wanajaribu kutathimini mikataba yote iliyokuwapo na iliyopo?!! Uuuuwiiii jamaa wanatupiga bao hawa!!

Naomba Serekali isitupelekee hili jamaa Kilaza, Kihiyo n.k
 
I am not a lawyer, lakini nadhani dispute ipo kwa sababu ya trties nyiingi za ziwa za kikoloni why 1890 only? Not 1892?
 
Hainiingii akilini kabisa eti ziwa lipo mpakani mwa nchi mbili udai lote lako, ina maana mwisho wa ziwa ndo mpaka? Huo si uchizi?

Hapo lazima kila nchi imegewe sehemu ya hayo maji kuepusha shari, unataka kuniambia nani atakubali asiyatumie maji na anayaona na anayahitaji kwa shughuli mbalimbali na let's say hakuna chanzo kingine cha maji.

Kwanza sometimes maji yanasogea zaidi na kumeza ardhi, kwahiyo watasema kote kulikomezwa kwao tena, hatuna mkataba nao sis na automatically huo wa wakoloni haupo kwani hawatawali
 
Mkuu n00b lete ramani hiyo tafadhali kupunguza pepelepepele za watu, as well hii inatokana na usiri/kukosekana kwa mirejesho kwenye mambo haya na maendeleo yake
 
Tanzania haiwezi ku-negotiate haki ya ziwa Nyasa kwa kutumia Anglo-German contract halafu wakatarajia kushinda. Hili haliwezekani. Wanachojaribu kufanya ni sawa na ku-negotiate matumizi ya maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract. Haiwezekani Tanzania ikashinda. Ndo maana Malawi wao watatusukumia huko!

Ni kweli kuwa tutakuwa tumekubaliana kwenye umoja wa Afrika kuwa mipaka ya wakoloni inasimama kama ilivyo, lakini si bila exception. Kuna maeneo ambayo mgawanyo wa wakoloni hauwezi kuheshimiwa kwa sababu za kibinadamu. Je tulisaini kwenye umoja wa Afrika tukiikubali mipaka ya wakoloni bila exception?

Exception zilikuwepo na ndo maana Mwalimu Nyerere alitamka kuwa hili halikubali. Sasa tukishakubaliana kuwa hatujakubaliana kuwa tutaheshimu mipaka ya wakoloni bila exception turudi kwenye ukweli sahihi. Tanzania na malawi zimetenganishwa na ziwa Nyasa (call it Malawi, or Kamuzu; it doesn't matter). Ukweli ni kuwa walioko ng'ambo ya kule ni wamalawi, walioko ng'ambo ya huku ni watanzania; hapo ndo pakuanzia.

Malawi inapata haki kwenye ziwa kwanza kwa sababu mikataba ya wakoloni inasema hivyo; lakini pili kwa sababu kuna wamalawi wanaishi hapo karibu na ziwa for Generations. Haki ya Tanzania kwenye ziwa hili haitokani na mkataba wa Anglo German, inatokana na watanzania zaidi ya 600,000 wanaoishi na kulitegemea ziwa hilo for generations. Mkataba wa waingereza na Wajerumani waachieni wamalawi wacheze nao; watanzania tunacheza na haki ya watanzania waliopo hapo kando ya ziwa - na ikilazimika tutaenda vitani kwa ajili ya kulinda haki ya watanzania hao kulitumia ziwa hilo kama lao, si la kuazima; kwa sababu wajerumani na waingereza walipokubaliana hawa watanzania hawakuhusishwa!

Chochote tulichokubaliana huko nyuma; ambacho kinawanyang'anya maelfu hayo ya watanzania haki ya kutumia ziwa Nyasa kama lao; hakina uhalali wowote! Suala la kuwa watanzania wamesema 50/50 au sijui latitude ngapi na ngapi halina maana yoyote! Chenye maana ni haki ya watanzania kulitumia ziwa hilo kama lao - si la kuazima katika maeneo yote ambayo wapo!

Sasa suala itakuwa watanzania wanalitumia ziwa kama lao hadi wapi? Hilo ndo la kujadiriana na watu wa malawi; kwa sababu na wao wanalitumia ziwa. Na iwe wazi kuwa watanzania hawako tayari kujadiri umiliki wa ziwa Nyasa; Watanzania wako tayari kujadiri umiliki wao wa ziwa unaishia wapi? Hili ndo inatakiwa twende nalo mbele.

Kamwe tusijadiri haki ya kutumia maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract; hatutashinda! Madai ya Malawi hata kama kwa logic yanaonekana ni ya kizandiki; lakini yako backed na documents. Na kwa wamalawi uhalali wa hizo documents hauko questionable.

Eneo tulilopigania na Waganda (Amin) ni dogo sana kuliko eneo lote la ziwa Nyasa linalohusisha idadi ya watu wanaokaribia milioni moja.

Kusema ukweli vita huwa ni "a necessary evil" ndo maana wamarekani wanatumia sehemu kubwa ya GDP yao kujiandaa na kupigana vita. Baadhi ya vita huwa ni ya lazima. Ikilazimika Tanzania inabidi iende vitani kupigania maslahi ya watanzania wapatao millioni moja wanaoishi na kutegemea ziwa nyasa for Generations ambao leo hii wanaambiwa si lao sababu tu kumeonekana uwezekano wa kupatikana humo mafuta na Gesi!
 
Mkuu wa majeshi David Mwamunyange mwenyewe anatokea kyela sijui kama ataruhusu ziwa alilokuwa anaoga na kuvasamaki akiwa mdogo linyanganywe na wamalawi
 
...Wameshagundua jamaa ni DHAIFU hivyo wanahisi labda hana ubavu wa kutetea mipaka ya nchi. Thubutu uchezee mipaka ya Tanzania wakati wa Mwalimu...Alikuwa anatoa kauli yake na anaisimamia mtindo mmoja bila woga. Na yeyote aliyejaribu kuchezea mipaka ya Tanzania aliposikia kauli ya Mwalimu alijua huyu jamaa hana msalie mtume yuko tayari kwa lolote lile...siye huyu anatoa kauli eti wanaotaka vita ni vyama vya upinzani!!!! Sijui tangu lini Membe na Lowassa wamekuwa kwenye vyama vya upinzani.

Hakika brother unaona fahari huutangaza ujuha wako wazi wazi. Kutetea mipaka ya nchi ni kuanzisha vita? Hivi ni lini, hata huo wakati wa Mwalimu nchi hii iliingai katika vita vya kulinda mipaka kwa style hii? Tulipompiga Amin, yeye alikuwa amevamia eneo la nchi hii na kujitangazia kuwa ni sehemu ya Uganda. Kilichopo hapa ni contention kati ya nchi mbili, kila moja ikiamini kwamba legitimately, ina haki ya kumiliki ziwa. Kukitokea hivi ni lazima watu wake mezani ni kuangalia areas za contention, vielelzo au ushahid mbalimbali na hatimaye kufikia muafaka. Tofauti na zamani (enzi za Mwalimu) sasa hivi kuna mahakama na vyombo mbalimbali vya kumaliza matatizo haya bila kulazimu kupigana. Hiyo style ya Sudan na Sudan ya Kusini haina nafasi katika dunia ya leo.

Hakuna wakati wowote ambao Membe alipata kutoa tamko la vita, zaidi ya kusema kwamba serikali na vyombo vyake vya dola vitakuwa imara kulinda mipaka. Hilo si tangazo la vita na aliwataka wenzetu wa Malawi kusitisha shughuli zote katika eneo la ziwa. Ni Lowassa na wapinzani walioona kwamba kauli ya Membe ilikuwa legelege na kutaka tufanye mobilization. Wenzetu walioendelea wako busy kushirikiana na majirani zao, siyo kuhasimiana. Unataka Membe atoe kauli kuhusu msimamo wa Tanzania mara ngapi? Msimamo wa nchi yetu ni kwamba ziwa lile ni mali yetu kwa ukubwa wa asilimia 50 ya kipande kilichobaki baada ya kuondoa kile cha Msumbiji. Ulitaka asemeje
 
Tanzania haiwezi ku-negotiate haki ya ziwa Nyasa kwa kutumia Anglo-German contract halafu wakatarajia kushinda. Hili haliwezekani. Wanachojaribu kufanya ni sawa na ku-negotiate matumizi ya maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract. Haiwezekani Tanzania ikashinda. Ndo maana Malawi wao watatusukumia huko!

Ni kweli kuwa tutakuwa tumekubaliana kwenye umoja wa Afrika kuwa mipaka ya wakoloni inasimama kama ilivyo, lakini si bila exception. Kuna maeneo ambayo mgawanyo wa wakoloni hauwezi kuheshimiwa kwa sababu za kibinadamu. Je tulisaini kwenye umoja wa Afrika tukiikubali mipaka ya wakoloni bila exception?

Exception zilikuwepo na ndo maana Mwalimu Nyerere alitamka kuwa hili halikubali. Sasa tukishakubaliana kuwa hatujakubaliana kuwa tutaheshimu mipaka ya wakoloni bila exception turudi kwenye ukweli sahihi. Tanzania na malawi zimetenganishwa na ziwa Nyasa (call it Malawi, or Kamuzu; it doesn't matter). Ukweli ni kuwa walioko ng'ambo ya kule ni wamalawi, walioko ng'ambo ya huku ni watanzania; hapo ndo pakuanzia.

Malawi inapata haki kwenye ziwa kwanza kwa sababu mikataba ya wakoloni inasema hivyo; lakini pili kwa sababu kuna wamalawi wanaishi hapo karibu na ziwa for Generations. Haki ya Tanzania kwenye ziwa hili haitokani na mkataba wa Anglo German, inatokana na watanzania zaidi ya 600,000 wanaoishi na kulitegemea ziwa hilo for generations. Mkataba wa waingereza na Wajerumani waachieni wamalawi wacheze nao; watanzania tunacheza na haki ya watanzania waliopo hapo kando ya ziwa - na ikilazimika tutaenda vitani kwa ajili ya kulinda haki ya watanzania hao kulitumia ziwa hilo kama lao, si la kuazima; kwa sababu wajerumani na waingereza walipokubaliana hawa watanzania hawakuhusishwa!

Chochote tulichokubaliana huko nyumba; ambacho kinawanyang'anya maelfu hayo ya watanzania haki ya kutumia ziwa Nyasa kama lao; hakina uhalali wowote! Suala la kuwa watanzania wamesema 50/50 au sijui latitude ngapi na ngapi halina maana yoyote! Chenye maana ni haki ya watanzania kulitumia ziwa hilo kama lao - si la kuazima katika maeneo yote ambayo wapo!

Sasa suala itakuwa watanzania wanalitumia ziwa kama lao hadi wapi? Hilo ndo la kujadiriana na watu wa malawi; kwa sababu na wao wanalitumia ziwa. Na iwe wazi kuwa watanzania hawako tayari kujadiri umiliki wa ziwa Nyasa; Watanzania wako tayari kujadiri umiliki wao wa ziwa unaishia wapi? Hili ndo inatakiwa twende nalo mbele.

Kamwe tusijadiri haki ya kutumia maji ya ziwa victoria kwa kutumia Anglo-Egypt contract; hatutashinda! Madai ya Malawi hata kama kwa logic yanaonekana ni ya kizandiki; lakini yako backed na documents. Na kwa wamalawi uhalali wa hizo documents hauko questionable.

Eneo tulilopigania na Waganda (Amin) ni dogo sana kuliko eneo lote la ziwa Nyasa linalohusisha idadi ya watu wanaokaribia milioni moja.

Kusema ukweli vita huwa ni "a necessary evil" ndo maana wamarekani wanatumia sehemu kubwa ya GDP yao kujiandaa na kupigana vita. Baadhi ya vita huwa ni ya lazima. Ikilazimika Tanzania inabidi iende vitani kupigania maslahi ya watanzania wapatao millioni moja wanaoishi na kutegemea ziwa nyasa for Generations ambao leo hii wanaambiwa si lao sababu tu kumeonekana uwezekano wa kupatikana humo mafuta na Gesi!

Sawa lakininni lazima kuwe na basis ya kukataa mikataba na katika hili msimamo wa Tanzania hautokani tu na watanzania wote uliowataja kusihinkaribu na ziwa. Ukweli ni kwamba mikataba hiyo haikuwa na nguvu ya kisheria pale serikali yetu ilipotamka kutoitambua na kutozingatia masharti ambayo Mwalimu aliyatoa mara baada ya kupata uhuru.
 
... ni mzaha wa kiayawani sijapata kuona kuingia mijadala ya ki-diplomasia kwa kutumia 'Malawian's 1890 Treaty' ambayo ni mkataba ambayo hata siku moja katika historia ya dunia HAIKUWAHI KUTAFUTA WALA KUSHIRIKISHA kitu maoni ya Mtanzania mle.

Ingawaje sisi wa leo hatukuepo bali Watanzania wa wakati huo walikwepo hapo hapo upenuni mwa Ziwa Nyasa lakini maoni yao hayako popote kwenye mkataba wanaozungumzia Wamalawi hivyo HATUWEZI HATA KIDOGO kuendesha mijadala yoyote inayopuuza HAKI YETU KUTUMIA MAJI YALIOKO HATUA MBILI TU KUTOKA KWENYE MAKAZI YA WATANZANIA eti tuende kuomba hata maji ya kunywa Malawi.

No, no, no Chiume, noooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom