Malasusa: Chagueni mtu makini si chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malasusa: Chagueni mtu makini si chama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Geza Ulole, Oct 17, 2010.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,087
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Malasusa: Chagueni mtu makini si chama
  Fidelis Butahe na Fredy Azzah
  MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa amewataka Watanzania kuchagua kiongozi makini badala ya chama. Askofu Malasusa ambaye pia ndiye Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, alisema hayo jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT Usharika wa Kitunda Relini, iliyofanyika katika ukumbi wa Msimbazi.

  Katika halfa hiyo ambayo Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye alikuwa mgeni rasmi, Askofu Malasusa alitumia dakika nane kuwaeleza watu waliofika kwenye harambee hiyo aina ya kiongozi anayefaa kuchaguliwa. Dk Malasusa alisema Watanzania wamechoka kudanganywa na akawataka kuamka na kuchagua kiongozi mwenye sifa bila kujali anatokea chama gani.
  Mkuu huyo wa KKKT hilo alikuwa akirudia kusema maneno hayo mara kwa mara wakati akiongoza mnada wa kuuza vitu mbalimbali, ikiwemo picha yake, ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, saa na khanga. Kabla ya kumkaribisha Sumaye kuzungumza na umati uliokusanyika kwenye harambee hiyo, Dk Malasusa alisema, "Kipindi hiki ni cha kutulia na kufanya lile ambalo Mungu ametuelekeza. Taifa hili ni la Mungu, tumlilie atatuonyesha kiongozi bora." Aliendelea: "Huu sio wakati wa kuchagua chama. Ni wakati wa kuchagua mtu ambaye ni kiongozi bora.
  Tumedanganywa vya kutosha miaka mingi, na kuchagua chama. "Tunahitaji kutulia na kumuomba Mungu ili atuelekeze njia ya kupata na kuchagua kiongozi bora na atakuwa nasi katika Uchaguzi Mkuu". Kauli ya Dk Malasusa inakuja siku chache baada ya viongozi wa makanisa Katoliki, KKKT na Pentekoste mkoani Kilimanjaro, kutoa waraka unaowataka waumini wao kuchagua mgombea anyafaa kuwaletea maendeleo badala ya chama cha siasa.

  Wakati akipiga mnada wa khanga, ambayo ilikuwa na rangi ya njano, Askofu Malasusa alimtazama mmoja wa watu waliotaka kununua khanga hiyo na kumuuliza: "Vipi hii inakufaa? Inaonekana inafanana sana na rangi ya kile chama chako. Lakini sasa hivi ni kuchagua mtu siyo mambo ya chama".

  Kauli hiyo iliwafanya watu waliokusanyika ukumbini humo kuangua kicheko huku wakipiga makofi. Dk Malasusa aliwataka waumini wa KKKT kutumia muda mrefu kutafakari na kumwomba Mungu, ili nchi iweze kupata viongozi bora na uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu. "Hiki ni kipindi kizuri na sisi kama sehemu ya raia wa nchi hii, tunapaswa kutulia. Tumuombe Mungu atupe kiongozi mzuri," alisema Askofu Malasusa na kuongeza: "Mkristo wa kweli hafanyi mambo kwa kukurupuka, hutulia na kumua kwa kumsikiliza Rohom Mtakatifu ".

  Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Kanisa alimfagilia Sumaye akisema katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi alizoshika, aliitumikia serikali na kanisa kwa uaminifu. "Katika nafasi mbalimbali alizoshika, Mheshimiwa Sumaye aliitumikia nchi hii kwa uaminifu, pia alilitumikia Kanisa," alieleza. Hivi karibuni Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Askofu Dk Valentino Mokiwa aliwataka wananchi kupokea hela za wagombea wanaotoa rushwa lakini wasiwapigie kura. Akizungumzia ujenzi wa kanisa hilo linalotajiriwa kugharimu takribani Sh900 milioni, Askofu alisema makanisa ni sehemu muhimu ya kubadili mienendo ya watu. "Watu wasipomrudia Mungu, tutaendelea kujenga magereza na kuongeza sheria bila mafanikio.

  Jengo hilo ni muhimu sana, naomba tujenge nyumba ya Mungu," alisisitiza. Hata hivyo, Sumaye hakutaka kuzungumza chochote kwenye harambee hiyo zaidi ya kuiongoza hafla hiyo kama mgeni rasmi. "Katika shughuli kama hizi huwa sitoi hotuba. Waliponiletea kadi ya mwaliko, niliwauliza nani mwingine atakayehudhuria hafla hii? "Waliponiambia ni Mkuu wa Kanisa Baba Askofu Malasusa, nikawaambia mimi nitakuja lakini, Askofu naomba ndiye awe mgeni rasmi," alieleza Sumaye mara baada ya kukaribishwa.

  "Kwa hiyo mimi nitakuwa MC (msemaji), kama yupo mliyemwandaa basi nitakuwa msaidizi wake," alieleza na kuendelea kuongoza harambee hiyo. Waumini wa KKKT nchini na Watanzania kwa ujumla, waliombwa kutoa michango yao ya hali na mali ili kuifanikisha ujenzi wa kanisa hilo, litakalo kuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3,000 kwa wakati mmoja. Kanisa la sasa linalotumika na usharika huo, lina uwezo wa kuchukua waumini 800. mwishio


  Malasusa: Chagueni mtu makini si chama

  MY TAKE:
  Haki ya Mungu Kikwete ukishinda safari hii ni kwa wizi tu! Hamna sababu nyingine watu wamekuchoka waliokuiita Chaguo la Mungu sasa wamekuchoka nathani marafiki wako ni mafisadi na wale unaoweza kuwarubuni tu!
   
 2. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama hivi ndivyo basi nasema kwa sauti kuu, BWANA YESU ASIFIWE SANA! Askofu Malasusa ametupa njia. Mwenye masikio na asikie yale ambayo roho wa wa Bwana anasema: Chagua Mtu si chama. Mtu utakayemchagua awe ni yule ambaye roho wa Mungu anakuthibitishia moyoni kuwa kuwa atakuwa kiongozi bora na si mtawawala na mtumia tumbo na familia yake.
   
 3. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mhhhh!!!
   
 4. D

  Divele Dikalame Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila shaka Mungu ni yule wa Ibrahim, Isaka na Yakobo huwa hana kigeugeu kama hao maaskofu walitwambia JK ni chaguo la Mungu tukafuata, leo hii wageuke kutwambia tumchague Dakta Slaa ni mtu makini, mwenye akili na maarifa anagundua hao maaskofu ni wasanii wala wasimuhusishe bwana Yesu na matashi yao ya kidunia, wanaomtaka JK wampe kura na hao wanamtaka Slaa wampe kura, bwana yesu,Roho mtakatifu wala roho wa Mungu wasihushwe na propaganda za kidunia, Yesu, Roho wa Mungu wala roho mtakatifu hawawezi kuwaunga mkono wagombea wazinzi wanaovunja amri za Mungu.
   
 5. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Viongozi wa dini waache habari ya siasa wahubiri dini, maana wakati mwingine wanaongea sababu wanashabikia chama fulani, au mgombea fulani. pamoja na nia nzuri wanazoweza kuwa nazo lakini wengi wao huwa wako subjective ndani ya mioyo yao ingawa kwa nje huwa wanataka waonekane hawako upande wowote
   
 6. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  amen
   
 7. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwa wakiristo kiongozi wa dini/dhehebu anaitwa baba au mama. hakuna baba au mama huku duniani ambaye anaweza akamuacha mwanae akue atakavyo,lazima atamuongoza njia sahihi za kupita ili awe salama. kwa hiyo kumtenganishe mtumishi na msitakabali wa nchi siyo rahisi kama unavyofikiria. interest ya watumishi wa Mungu ni kuona wanaongoza watu ambao wako na maisha mazuri au bora kama chama fulani kinavyoyatamka ila hakiyafanikishi....
  Waache Wachungaji wachunge kondoo kama walivyoamriwa na Mungu na wasiwaache makondeni wasije raruriwa na marushwa na usanii wa akina RA,EL,BM and the likes.

  .....................2010 hatudanganyiki ng'o......
   
 8. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  you don't know christianity bro/sisy.
  kwenye ukiristo watumishi wa Mungu wanaongozwa na roho mtakatifu kuwaongoza kondoo. kama alisema 2005 JK ni chaguo la Mungu halafu mwaka 2010 wakasema siye tunawasikiliza kama tulivyofanya 2005! by the way this time hakuna mtumishi wa Mungu aliyetaja jina la mgombea yeyote...mimi nimfuatiliaji mzuri sana,ila sijasikia popote.
  kuna kajikikundi kawatu kanasambaza sumu ya udini hapa nchini kwa masilahi binafsi na watu wameunga tera bila kujua interest za hiyo agenda....
  Mungu tunaye muabudu hawezi kuacha nchi iangamie wakati ana watu wa kutoa mwelekeo sahihi.
  wachungaji/maaskofu wote wanasema mtu mwenye sifa ndiye apewe kura..kama JK ana sifa za kuwashinda wenzie atapata urais lakini kama hana atakosa.

  ....mimi nimeona anafaa ila SLAA anafaa zaidi,hivyo nitamchagua bila kigugumizi.
   
 9. m

  mapambano JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa dini kama hawa ndio watawagawa watz. Shame on you, mnatumia jina na nyumba ya mwenyezi mungu kwa matamanio yenu binafsi. Chuki za kidini hapa JF ni dalili tosha ya matatizo ya viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa. Anyway, flind followers will always be there, they never question or analyse anything. Kwao chochote anachosema kiongozi wa dini ni sawa...akisema JK ni changuo la mungu, SAWA...shame on you!!
   
 10. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  chama kinahusika pia

  Jamani si tunaongelea kuchagua chama chenye irani nzuri kwa maendeleo ya Taifa au?

  mtu anaweza kuwa na sifa nzuri sasa anakuwa si mgombea binafsi bali atapaswa kutekeleza sera za chama chake ambacho huenda hawana sifa nzuri
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  2005 Walivyosema JK chaguo la mungu mkashangilia - sasa hivi kutoa tu elimu ya uraia kwa waumini wao kinawauma - mkome huu ndiyo Mkuki wenu wa mwisho ili next time mkipewa madaraka kuyaheshimu Urais si kuuza karanga na kwa bahati nzuri watanzania wengi wameshashtukia.

  Kwanza huku ni kujihisi bure kwani kuna ubaya gani mtu kusema "Chagueni mtu makini na si chama?" hapo anakuwa amefanya kosa? kama mlizoa mtelemko chaguzi zilizopita mwaka huu lazima mpande mlima. hakuna udini wowote acheni kuzushia watu.

  Sijaona kosa lolote alilofanya Kakobe na wala Askofu Malasusa kuhusu waumini wao. CCM acheni kulialia.
   
Loading...