Malaria sasa kuwa historia nchini

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,511
Alitoa agizo hilo jana alipofungua barabara ya Msata-Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 64 na kubainisha kuwa tangu kujengwa kwa kiwanda hicho, ni halmashauri nne tu zilizonunua dawa hizo kutoka kiwandani hapo kwa Sh. bilioni 1.3.

Rais Magufuli alisema kwenye kiwanda hicho viuatilifu ambavyo ni maalumu kwa ajili ya kuzuia mazalia ya mbu, vimejazana huku watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wamejikita kwenda kununua dawa za kutibu malaria Ulaya na kuziacha dawa za kiwanda hicho ambazo lita moja inauzwa Sh. 13,000.

Alisema wizara hiyo ingetumia dawa hizo kuangamiza mazalia ya mbu, ndani ya miaka mitano ugonjwa wa malaria ungetokomezwa nchini.

Rais Magufuli alisema ameiagiza Wizara ya Fedha kununua kwa niaba yake kiasi chote cha viuatilifu kilichopo kiwandani hapo kwa nia ya kuzigawa kwa kila halmashauri.

"Leo ni Juni 22, nimesema hadi Juni 30 wakurugenzi wote wawe wameenda kuchukua dawa hizo, sasa ole wake atokee mkurugenzi asiende kuchukua," alisema Rais Magufuli.

PEMBEJEO FEKI
Awali Rais Magufuli alisema kuna wakuu wa wilaya ambao wamekuwa wakijinufaisha kwa fedha za umma kupitia orodha zenye wanufaika hewa wa pembejeo.

Alisema kumekuwa na ugawaji wa pembejeo hata kwa watu waliofariki dunia miaka 30 iliyopita, hivyo kumwagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba kushughulikia suala hilo.

"Kuna watu waliokwishafariki (dunia) miaka mingi halafu wanapewa pembejeo, sasa sijui walikuwa wanawafufua halafu wanakuja kupokea pembejeo kisha wanarudi kaburini," alisema Rais Magufuli.

Alisema baada ya serikali kumaliza kushughulikia tatizo la wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa na vyeti feki, sasa wanageukia ugawaji wa pembejeo feki.


Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom