sangujoseph
Senior Member
- Nov 30, 2015
- 164
- 184
Mwalimu Julius kambarage Nyerere Mimi ni [HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] mwenye uchungu na taifa langu na serikali yangu ambae sijawahi kukushuhudia ukiwa madarakani Bali nilichokiwahi kukisikia kuhusu wewe juu ya uwezo wako wa kutawala na falsafa yako ya kutoa nafasi Kwa wachache kusikilizwa maoni yao.
Mwalimu nyerere kutokana na historia yako ya Maisha natamani hata siku moja Nije kwenye kaburi Lako nikueleze ni jinsi Gani mambo yanavyoenda tangu nchi ulipoiacha oktoba 14 miaka 17.iliyopita babu nchi yangu imefikia sehemu mbaya matatizo kila kukicha.
Babu yangu Nyerere tangu uondoke wewe nchi imekuwa haina viongozi wenye wito na uzalendo wa taifa na hata kuheshimiana wenyewe imefikia hatua kiongozi anamdharau mwenzake sababu wana itikadi tofauti wa kivyama au hata kabila sababu Tu mwengine ana miliki dola au mwenzake hamiliki au mwingine anadhani anaonewa sababu mwenzie ana
DOLA.
Babu yangu Nyerere nchi sasa imevamiwa na wageni wao ndo wanaonekana wanaishi vizuri na kunufaika na rasilimali za nchi ilihali wazawa tunapigwa na jua kila kunapozidi kucha huduma za muhimu hakuna matajiri wanatutesa. Sisi wa hali ha chini Sababu tu wanajua hatuna pakusemea et wanadai tukienda tu kusema watatugeuzia sisi.
Babu yangu Nyerere Vijana siku hizi hatupendi kufanya kazi tunahitaji maisha mazuri wakati tunashinda tukicheza poor NA tukibishana kuhusiana NA ugomvi wa Diamond na Alikiba lakini wengine wanashinda Gym kila siku kuvutia wadada.
Babu yangu Nyerere kuna tatizo kubwa limezuka ghafla la KULAWITI na KUBAKA babu yangu hili ni janga jipya zaidi ya "JANGA la SCORPION" kwa utafiti mfupi nilioufanya nimegundua katika siku 7 magazeti huripoti kesi 4 za kulawiti na kubaka.
Babu yangu Nyerere nchi sasa haina UZALENDO kila mtu ni mkosoaji kila anapinga jambo linalofanywa na serikali wanasiasa uchwara wako tayari kuona TANZANIA inasemwa vibaya ili wapate cha kuombea kura bila kujali kuwa linalosemwa ni taifa lake na yeye anahusika lakini babu tusaidie na pia tuondokane siasa maana siku hizi ukikosoa UPINZANI unaanbiwa wewe ni CCM ukikosoa SERIKALI unaambiwa wewe ni CHADEMA.
[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] #ilovetz#maoniyangu