Malalamiko kwa bus la BM za dar moro

Naimani wewe ni mtanzania Halisi na unajua Hali Halisi ya watanzania ,,,,vingine vishida vya kawaida pia usipende ubinafsi
Maana Kuna baadhi ya kero umezitaja inawezekana unasumbuliwa na karoho kaubinafsi mfano system port huitumii mwwnzio anashida unatarajia Nini hapo
Amani ya bwana iwe nanyi

Niende kwenye mada husika.Katika safari zangu nimepanda moja ya hizi bus za Benson Makundi.
Nikakata siti za upande wa mbele zilizojitenga ambazo wanaziita wenyewe "VIP".Zimekua na usumbufu mkubwa bora kukata tiketi siti za kawaida.
Unaposema VIP means ni very important person."Hapo inatakiwa extra care+extra service +comfortability.
Abiri unashindwa kuinjoi tokana na kero za abiria wenzako na wahudumu (konda)wa basi anaangalia tu.Huwezi kusizia hata dakika mbili.

Watu wamesimama na kuegemea hizo siti,Wengine wamekaa chini.Karaha kwenye kupishana mana abiria wengine wapo njiani wengine inabidi waingie ama washuke.
Mwingine anakalia mkono wa kiti anachomeka waya wake wa USB ana chaji simu yake hapo pembeni yako.Hana habari.

Najua kuna watu watakuja kutoa povu kwanini nisifikishe lawama zangu kwa wahusika?
In any business "complain is gift".Sasa inategemea itapokewa vipi.Pili ni angalizo kwa member wenzangu wanapotaka kutumia huduma hizi wajitafakari.
Tatu nadhani njia rahisi kumfikia muhusika na kwa wakati.Nne kuna member wenzangu wamepitia changamoto kama hizi so watatumia uzi huu kushauri ama kulalamika kwa faida ya wote.

Asante.
 
Back
Top Bottom