Makusanyo ya kodi yazidi kupaa

Makusanyo ya kodi yazidi kupaa

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli. Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa.

Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa. Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA. Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida.

Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi.

Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma. Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.
 
Yaani huu mtego wa kusifu na kuabudu umefikia hatua ya kukera sasa.

Taasisi kubwa kama TRA kweli nayo inatumika kijinga hivi? Taasisi kama hii badala ijitathmini based on misingi ya kuanzishwa kwake au based on market inajitathmini based on tangu kuingia kwake madarakani! Shame on this aisee
 
Ooh kumbe viongozi waliopita walikuwa wanasaidia ukwepaji kodi?....
Hongera sana awamu ya tano kwa kuondoa hili tatizo na tunaomba awamu ya tano idumu kwa miaka 50 mbele
 
Mbona hajaongelea Asilimia mia na hamsini ya mshahara waloongezwa wafanyakazi wa TRA mwezi wa tisa huku watumishi wengine wakiwa kapa.
 
Kila mradi wanasema tunatekeleza kwa pesa zetu wakati mikopo serikali hii imejawa na washamba sana
 
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli. Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa.

Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa. Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA. Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida.

Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi.

Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma. Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.
Nimesoma zaidi ya mara 3 kwa kufikiri kuwa nitakutana na namba, ila nimeishia kuona ya mwezi September na sasa ni Novemba.
 
Lazima yaongezeke maana kuingia stand tu yenyewe sasa hiv ni pesa hapo bado hujasafiri .

Lkn siku moja asilimia kubwa ya watu fahamu zao zitafunguka na hapo ndipo itakua mshike mshike nasemaje tutatafutana humu
 
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli. Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa.

Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa. Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA. Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida.

Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi.

Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma. Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.
Rubbish
 
Ooh kumbe viongozi waliopita walikuwa wanasaidia ukwepaji kodi?....
Hongera sana awamu ya tano kwa kuondoa hili tatizo na tunaomba awamu ya tano idumu kwa miaka 50 mbele
Watanzania ni watu waungwana sana,ila viongozi wetu siyo mfano wa kuigwa.Wamejipa Tax Exemption wakati wao wanavipato vinono na marupurupu Kibao lakini si walipaji kodi.Tuweke sheria ya kiongozi kuwa mlipa kodi na anayekwepa/asiyelipa apoteze sifa ya kuchaguliwa/kuteuliwa.Hilo lingefanya kila Mtanzania kulipa kodi na hakutakuwa na misamaha.
 
Sasa kama makusanyo yameongezeka kwa nini deni la taifa linazidi kupanda?
Inashangaza kwa sababu spidi ya ukusanyaji kodi inakwenda sawa na spidi ya deni la taifa kupaa. Miaka minne deni linakaribia kuwa sawa na deni la miaka kumi la uongozi wa JK!!!!
 
Back
Top Bottom