Makusanyo ya kodi yazidi kupaa

Makusanyo ya kodi yazidi kupaa

Ujinga mtupu.. kama mmefunga ofisi kikimbia chadema wasirudishe form ..kwa nini msipoke namba za makusanyo
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli. Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa.

Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa. Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA. Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida.

Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi.

Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma. Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.
 
Sasa kama makusanyo yameongezeka kwa nini deni la taifa linazidi kupanda?
Mkuu MANI kuna mambo unaweza kutukana kabisa. Mtu anasimama anabana pua "sasa hivi mapato yangu ni makubwa mno"
Unashangaa madeni halipi? Mishahara haongezi wakati bei zinapanda, watoto wetu pamoja na kusoma ajira hakuna! Kula kitu ni hovyo kuliko Jana mapato yalipo kuwa madogo.
 
Hakuna namna ya kuthibitisha kuwa mapato yameongezeka wakati takwimu haziwekwi wazi kwa kila walaya, mkoa hadi jumla ya nchi nzima.

Hadi pale hili litakapofanyika, kwa sisi tunaojitambua tutaendelea ku-treat taarifa feki kama hizi kama, Normal Public Relations Exercise tuliyozoea. That's all.
 
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli. Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa.

Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa. Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA. Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida.

Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi.

Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma. Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.
Takwimu zote za awamu ya 5 ni "cooked". Kuanzia makinikia, korosho hadi makusanyo ya TRA.

Hakuna takwimu inayotoka public bila Meko kuiona na kuchakachua.

Kwa mfano; tume ya Prof Mruma iligundua kuwa kwenye kila container la makinikia la 20 feet kuna mabaki ya Gold 0.7 Kg. Lakini Meko aliposoma ripoti ya Mruma akaona ikiripotiwa 0.7 Kg haiwezi ku-justfy ile hypithesis yake kuwa ACACIA wanaiba dhahabu. Hivyo akamuambia Prof Mruma atoe decimal point na ikasomeka 7. 0 KG. Na ndiyo kisa cha kupata USD 190 BILLION au Tsh 450 Trillion ambazo ndiyo tunawadai ACACIA.

Mwisho wa siku hakuna kitu kama 7.0 Kg ya dhahabu na hakuna Tsh 450 Trillion.

Nao TRA wankusanya kati ya Tsh 950 Bilioni na 1.2 Trilioni kwa mwezi. Wangekuwa wankusanya Tsh 1.5 tusingekuwa na deni la Serikali kubwa hivyo kwa kipindi kifupi. Hii ni Serikali ya fake data
 
Watanzania ni watu waungwana sana,ila viongozi wetu siyo mfano wa kuigwa.Wamejipa Tax Exemption wakati wao wanavipato vinono na marupurupu Kibao lakini si walipaji kodi.Tuweke sheria ya kiongozi kuwa mlipa kodi na anayekwepa/asiyelipa apoteze sifa ya kuchaguliwa/kuteuliwa.Hilo lingefanya kila Mtanzania kulipa kodi na hakutakuwa na misamaha.
Sheria utungwa kwa ajili ya masikini
 
Back
Top Bottom