Makundi ya kipalestina yaapa kuifanya Israel kutokuwa na amani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Jihad al Islami: Kambi ya muqawama haitoruhusu adui kuwa na utulivu

Msemaji wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amegusia mazungumzo yaliyofanyika baina ya wakuu wa kambi ya muqawama huko Beirut Lebanon na kusisitiza kuwa, kambi ya muqawama kamwe haitouruhusu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa na utulivu.

Kwa mujibu wa televisheni ya Falastin al Yaum, Musab al-Breim amesema hayo na kuongeza kuwa, kambi ya muqawama inaendesha harakati zake katika janibu zote za kisiasa, kijeshi na za kwenye medani, kuanzia Palestina hadi maeneo mengine na kamwe kambi hiyo haitoruhusu adui Mzayuni aishi kwa utulivu na amani.

Matamshi hayo ya Msemaji wa Jihad al Islami ya Palestina yamekuja baada ya mkuu wa harakati hiyo Ziyad al-Nakhalah na Saleh al-Arouri, Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, kuonana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah.

Msemaji wa harakati ya Jihad al Islami amesisitiza kuwa, mshikamano imara ndani ya kambi ya muqawama unaakisiwa na unaonekana wazi katika medani mbalimbali za kupambana na adui Mzayuni.

Wakati huo huo mchambuzi mmoja Mzayuni amekiri kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeonesha udhaifu mkubwa katika medani tofauti na hali ni mbaya ndani ya jeshi hilo tofaudi na jinsi viongozi wa Israel, iwe wa kijeshi au wa kisiasa wanavyojaribu kuwaonesha walimwengu.

Shirika la habari la Tasnim limemnukuu Tal Ram, mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa gazeti la Kizayuni la Maariv akiandika: Utendaji kazi wa jeshi la Israel una hali mbaya na maandamano dhidi ya serikali ya Netanyahu yamezidi kuliweka jeshi hilo la Israel, katika hali mbaya.

4bv61e35847fe81lv16_800C450.jpg
 
Mi naona solution ni kuunda nchi moja
Nchi moja haiwezekani,.. wapalestina wanataka hijab vazi la kina mwanamke na waisrael hawataki kutawaliwa na sheria za dini ingine. sasa hivi tukienda hija bethlehem hatuna haja ya kutawaliwa na sharia law ila ukifanya nchi moja basi madai ya sharia law kwa sisi spiritual jews yatatukera.
 
hivi nitisho vya kila wiki. walianza the black september 1970 wakaja PFLP mpaka kuja HAMAS kutaka kuleta uhuni kwa watoto na wajukuu wa rebeca lakini hawakufua dafu. hebu soma kitabu kiitwacho the greatest operation of sayet maktal na kingine cha MOSSAD kiitwacho the Asasination of Mohamed mahboh hapo utagundua waisrael wana akiri sio ya kibinadamu tuu bali pia ni akiri ya malaika inayowajalia kufanya revenge kwa wapalestina wawaleteao vifo.

Kuna mpalestina aliyeitwa Mohamea al wazir ambaye ndiye aliyepanga mauaji ya wanamichezo wa Israel pale munich 1972, huyu jamaa alikuwa na ulinzi mkali sana. Nyumba yake pale tunisia ilikuwa na fence, mbali na fence palikuwa na kibanda cha mlinzi, mbali na kibanda cha mlinzi palikuwa na mlinzi mmoja akaae ndani ya nyumba na mwingine basement masaa 24. halafu nje ya nyumba kuna gari liko mita kumi na mbili lina mlinzi aangaliae kila mtu aoongeaye na mlinzi kibandani. basi MOSSAD waliingia ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kumchinja mohamed al wazir risasi mia nane mbele ya mke na watoto watatu. halafu kabla ya kutoroka wakapiga simu polisi kuwa kuna mauaji yametoke kwa mpalestina . Moissad walitorooka salama na hawakukamtwa,
 
Nchi moja haiwezekani,.. wapalestina wanataka hijab vazi la kina mwanamke na waisrael hawataki kutawaliwa na sheria za dini ingine. sasa hivi tukienda hija bethlehem hatuna haja ya kutawaliwa na sharia law ila ukifanya nchi moja basi madai ya sharia law kwa sisi spiritual jews yatatukera.
Wayahudi huko hawataki hata kusikia jina la Yesu, unalielewa hilo?
 
Huoo ni uwooooongo buanaaaaa.


Israel ni Taifa La Mungu.


Mytapigwa na US, mtapigwa na UK, Mtapigwa na NATO 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom