Makundi CCM yamzonga Kikwete

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
MAKUNDI ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), yanaonekana kumwelemea Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na sasa ameamua kutumia mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), kukemea vitendo vya kudhalilishana na makundi wakati na baada ya uchaguzi.

Rais Kikwete pia alionya juu ya vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri ndani ya chama hicho akisema kuwa visipochukuliwa hatua mapema, kuna hatari ya kukifikisha chama katika hatua mbaya.

Akifunga mkutano huo wa nane wa uchaguzi UWT, Rais aliwataka kufanya jitihada za kupunguza mgawanyiko uliotokea baada ya uchaguzi wao uliomalizika juzi.

Alisema imekuwa ni hulka sasa hasa baada ya kumalizika uchaguzi kwa wanachama kuendeleza na kuwekeana uhasama kama uliokuwepo wakati wa kampeni na wengine kuwaadhibu ambao hawakuwachagua hali ambayo ni mbaya sana kwa mustakabali wa chama.

"Ambaye hakukuchagua usimbague kwani hakushinda na sasa wewe ndiye kiongozi, hivyo una kila sababu ya kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuitumikia jumuiya yake kwa ukamilifu.

"Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu," alisisitiza.

Rais Kikwete aliwaasa wagombea wa nafasi mbalimbali wa UWT walioshindwa kutoweka visasi na walioshinda kutowapiga vijembe walioshindwa kwani kazi iliyo mbele ni kubwa kutokana na CCM hivi sasa kukabiliwa na hali ngumu ya ushindani wa kisiasa.

"Kweli tusipokemea vitendo hivi na kuviacha vikiendelea, tutakipeleka chama mahali pabaya, ninasikitika sana kusikia hata wanawake sasa wanajihusisha na utoaji rushwa ili kununua nafasi za uongozi kitu ambacho ni hatari sana," alisema Kikwete.

Alifafanua kuwa chama kinakoelekea si kuzuri ni lazima zifanyike jitihada za mabadiliko.

Aliwapongeza wajumbe kwa kukamilisha uchaguzi wa viongozi watakaoongoza jumuia hiyo kwa muda wa miaka mitano na hata waliojitokeza kugombea kwani kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi.

Rais Kikwete aliongeza kuwa madhumuni ya CCM yaliyotamkwa katika katiba ni kushinda katika uchaguzi wa serikali kuu na mitaa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda serikali kuu na serikali za mitaa.

Alisema ushindi wa CCM unapatikana kwa kukubaliwa na kuungwa mkono na wananchi wengi zaidi watakaojitokeza kupiga kura, hivyo kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa na jumuiya za chama zilizoundwa ni kufanikisha hilo.

Kikwete alifafanua kuwa demokrasia ya uchaguzi ina athari zake kwani baada ya hapo kuna kazi kubwa ya kujenga umoja na mshikamano ili kuziba nyufa na mipasuko iliyotokea wakati wa uchaguzi.

Alisema kuwa huwezi kumchukia mwenzako kwa vile ameomba nafasi unayoitaka wewe, kwamba nafasi hiyo ni haki ya kila mwanachama, hivyo hakuna haja ya kuchukiana.

Rais Kikwete alifafanua kuwa uchaguzi una mifarakano mingi lakini kiongozi akishapatikana ni lazima aungwe mkono na kwamba wenye kuonyesha mfano ni wale walioshinda kwa kutowabeza walioshindwa.

Awali, Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba, alisema kuwa wamefanya mengi ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na wamejipanga kuhakikisha wanaleta ushindi katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Source: Tanzania Daima
 
"Zifanyike jitihada za mabadiliko" Only words,angechukua hatua kwa wote waliobainika. actions speaks louder!
 
Kikwete muongo. Yeye mwenyewe ni tunda na mnufaika wa makundi na takrima. Naona anataka kutafuta umaarufu kwa kujifanya ameona makosa yake wakati si kweli. Mitandao ipo hasa huo wa rafiki yake Lowassa aliyeanza kampeni za urais hata kabla ya kipenga. Sijui ni fisadi na juha gani atampa kura yake Lowassa ili amle?
 
Hata mimi sikumwelewa. Lakini ninachojua ugomvi wake au tofauti baina yake na Mwandosya zina historia ndefu hata kabla ya uchaguzi wa 2005.

Kinachochanganya kidogo ni reference to uchaguzi uliopita ikiwa na maana ya 2010, does it mean kwamba Mwandosya alikuwa na nia ya kumfanya JK awe 'a one term president'?

Kwa kweli idara ya Mawasiliano huko kwa Salva ni muhimu iliweke hili sawa, sidhani kama kuacha mfano huo uelee kama ulivyo ni tiba ya kuvunja makundi huko tunako elekea; Mwandosya mwenyewe mgonjwa and the last thing he needs ni kuwa katika wingu hili lisilo na ufafanuzi wa kina;
 
Kwa wale wanaoelewa zaidi, Je, hapo kuhusu Prof. Mwandosya alikuwa na maana gani? Kwamba kambi ya Mwandosya ilihusika katika mambo ya ajabu aliyotendewa?

Mchambuzi, unajua hata mimi nimeshtuka.

Nimesoma nika copy hiyo part ili niquote na kuuliza. Kikwete ana maana gani?

Ina maana ni Mwandosya aliyemfanyia mambo ya ajabu? Au kampeni yake?

Na je, kusema haya sasa kunajenga au kubomoa? Maana wengine kwa sababu tumesoma kauli "vague" tunaweza kutafsiri kauli kama Mwandosya alimfanyia Kikwete mambo ya ajabu lakini Kikwete kwa ukomavu wake wa siasa akamuweka tu katika serikali yake.

Je ni ukomavu wa kisiasa kusema haya kwa kumtaja mtu jina?

"Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu," alisisitiza.
 
Mchambuzi, unajua hata mimi nimeshtuka.

Nimesoma nika copy hiyo part ili niquote na kuuliza. Kikwete ana maana gani?

Ina maana ni Mwandosya aliyemfanyia mambo ya ajabu? Au kampeni yake?

Na je, kusema haya sasa kunajenga au kubomoa? Maana wengine kwa sababu tumesoma kauli "vague" tunaweza kutafsiri kauli kama Mwandosya alimfanyia Kikwete mambo ya ajabu lakini Kikwete kwa ukomavu wake wa siasa akamuweka tu katika serikali yake.

Je ni ukomavu wa kisiasa kusema haya kwa kumtaja mtu jina?

Exactly, na pia je, uchaguzi uliopita ana maana 2010 Mwandosya alikuwa anajaribu kumfanya JK awe a one term president? Nisingependa kuamini JK alimaanisha kinachotafsiriwa na ni muhimu idara yake ya Mawasiliano iliweke hili sawa;
 
Kikwete yeye ndio baba wa mipasuko na makundi ndani ya MAGAMBAZ PARTY
 
Itakuwa ni aibu sana na ajabu, pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua; natolea mfano kwangu katika uchaguzi uliopita, Prof. Mark Mwandosya hakushinda, lakini kwenye serikali yangu nilimuweka licha ya kuwa nilifanyiwa mambo ya ajabu sana ambayo ni vigumu kuyavumilia lakini kwa mwanasiasa, lazima uwe mkomavu," alisisitiza.
Mashishanga anajua vizur haya ya uhasama.
 
Huyu Vasco da Gama namshangaa sana habari ya kumtaja mtu baada ya miaka nane kupita ina maana gani tena, anataka tuamini kuwa Prof Mwandosya alimfanyia mambo mabaya?
 
Mchambuzi, unajua hata mimi nimeshtuka.

Nimesoma nika copy hiyo part ili niquote na kuuliza. Kikwete ana maana gani?

Ina maana ni Mwandosya aliyemfanyia mambo ya ajabu? Au kampeni yake?

Na je, kusema haya sasa kunajenga au kubomoa? Maana wengine kwa sababu tumesoma kauli "vague" tunaweza kutafsiri kauli kama Mwandosya alimfanyia Kikwete mambo ya ajabu lakini Kikwete kwa ukomavu wake wa siasa akamuweka tu katika serikali yake.

Je ni ukomavu wa kisiasa kusema haya kwa kumtaja mtu jina?

Hii statement ya Prof. Mwandosya inahitaji kurekebishwa vinginevyo tasfiri yake siyo nzuri kwa Prof na wafuasi wake lakini pia Rais haimpi heshima. siyo mfano mzuri kutolewa na our president.
 
Mashishanga anajua vizur haya ya uhasama.
Na kwa sasa Mashishanga amepata ujumbe wa NEC.
Ila hilo la Mwandosya nadhani hata mimi limeniacha hewani. Yeye ndo mwasisi wa makundi, kwa nini analaumu matokeo ya alichokiasisi? Hizi chuki za makundi haziwezi kwisha kwa porojo
 
Hii statement ya Prof. Mwandosya inahitaji kurekebishwa vinginevyo tasfiri yake siyo nzuri kwa Prof na wafuasi wake lakini pia Rais haimpi heshima. siyo mfano mzuri kutolewa na our president.

Ni kweli jk amechemsha lakini hilo hilinishangazi hata kidogo kwani hakuna wisdom ndani take. Ndio maana sikubaliani na sentensi yako ya mwisho. Sio raisi wangu.
 
Amegundua makosa yake, sasa anafikisha ujumbe kwa wengine........ mtu mzima yule jamani

Kikwete muongo. Yeye mwenyewe ni tunda na mnufaika wa makundi na takrima. Naona anataka kutafuta umaarufu kwa kujifanya ameona makosa yake wakati si kweli. Mitandao ipo hasa huo wa rafiki yake Lowassa aliyeanza kampeni za urais hata kabla ya kipenga. Sijui ni fisadi na juha gani atampa kura yake Lowassa ili amle?
 
Mchambuzi, unajua hata mimi nimeshtuka.

Nimesoma nika copy hiyo part ili niquote na kuuliza. Kikwete ana maana gani?

Ina maana ni Mwandosya aliyemfanyia mambo ya ajabu? Au kampeni yake?

Na je, kusema haya sasa kunajenga au kubomoa? Maana wengine kwa sababu tumesoma kauli "vague" tunaweza kutafsiri kauli kama Mwandosya alimfanyia Kikwete mambo ya ajabu lakini Kikwete kwa ukomavu wake wa siasa akamuweka tu katika serikali yake.

Je ni ukomavu wa kisiasa kusema haya kwa kumtaja mtu jina?
Huyu mkweree nadhani alikuwa anafanya reference ya uchaguzi wa 2005 na sio uchaguzi wa 2010 kwani hapo alikuwa peke yake kutoka ccm!! Hata hivyo sijui ana maana gani kuwa Mwandosya na kambi yake walimfanyia mambo mabaya sana hata hivyo alimuweka kwenye serikali yake; lakini kwa wale wanaojua historia ya kisiasa ya hawa wawili ,all along ni mkweree ndio alikuwa anamfanyia mambo mabaya mwenzie na hili liko well documented kwenye kitabu cha Mwandosya alichoandika kitwacho "SAUTI YA UMMA NI SAUTI YA DEMOKRASIA" ingawa hakumsema yeye huyu bwana directly inaonekana wazi jinsi vyombo vya dola vinavyoweza kutumika vibaya kuwathibiti na kuwaonea wale wasiopendwa na watawala!!
 
Ina maana JK kampa Mwandosya uwaziri kwa kinyongo? Kumnyima aliogopa reaction? Je tatizo la afya yake haina mkono wa mtu?

Ktk maisha, bora adui anayekukasirikia kuliko anayekuchekea maana utampa nafasi atakusogelea na kukuzuru.

Nakumbuka ya Mwakyembe alivyokuwa mbunge alikuwa safi, alipopata uwaziri afya ikaleta matatizo tukasikia mengi mara unaweza kugusishwa tu sio lazima ulishwe bora unapokuwa tofauti kuanza mapema uking'ang'ania chamani unakuwa karubu nao wana ku do.
 
Inashangaza Kikwete kulalamika. Anashangaa nini? Kasahau alivyowachafua Sumaye, Mwandosya na Salim A. Salim mwaka 2005?. Kweli nyani haoni kundule.
 
JK ni kinara na muasisi wa makundi na mtandao ndani ya CCM,walimchafua sumaye kwamba ana mabilioni nje ya nchi,pia walimchafua Dr Salim Ahmed Salim kwamba aliusika kwenye kifo cha Sheikh karume.
 
Back
Top Bottom