Tanzania ni waoga sana na wengi tunashabikia bila kuelewa... Mimi niko Kenya Nafanya Kazi sikulipa hat senti kuomba residence/work permit hapa Kenya lakini sisi tunawatoza wakenya fee kwa kitu hii ya permit. Tuna matatizo ndo maana hatuendelei KIA ni uwanja mkubwa sana wa ndege lakini umechoka nyufa zake hata chatu anaishi ndani..HAKUNA FEDHA REAL? HAKUNA MAWAZO YES
Hivi sasa Uganda imetoa kibali cha kuruhusu raia wa Kenya na Rwanda kuwa huru kuingia nchini humo na kufanya kazi ambazo raia wa Uganda wanafanya. Kwa maana nyingine, ikotokea kuna nafasi ya ajira, Mkenya na Mnyarwanda ruksa kushiriki kwenye mchakato wa usahili!
Lakini hatua hiyo kwa nchi hizo tatu imeenda sambamba na kututenga Watanzania katika makubaliano hayo. Je, huu ni mwanzo wa jitihada za muda mrefu za kututoa kwenye picha? Au ni uoga wetu tu Watanzania wa kutokuwa tayari katika ushindani wa kitaaluma kwenye soko la ajira?