Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
MAKTABA NDANI YA KIBATARI CHA MCHINA
Inawezekana kabisa kuwa katika wasomaji wangu wakawepo ambao hawajasikia neno, "kibatari," wala hawajakiona kibatari.
Nilipata kuwahadithia wanangu kuku wangu niliyekuwa nalalanae chumba kimoja yeye analalia yuko pembeni kwenye kona.
Mshtuko mkubwa.
Nawatahadharisha kuwa kuku akilalia mpitie kwa mbali ama sivyo atakuparura.
"Baba unalala na kuku chumba kimoja?
"Naam tunalala chumba kimoja."
Najua wapi shida yao ilipo.
Wao kuku wanamuona mezani katoka super market keshachinjwa.
Nyumba wanayojua wao ni hiyo waliyozaliwa yenye korokoro zote za kisasa pamoja na air-condition na mengineyo.
Nyumba yetu ilikuwa juu makuti na chini udongo na sakafu ni ardhi yenyewe ya Allah.
Moyoni wanajiambia baba analeta porojo kututisha.
"Taa yangu kibatari."
"Kibatari?"
Naulizwa.
Hawa hawawezi kuchangia computer moja kila saa naitwa kuamua ugomvi.
"Game over," mtu hataki kumpisha mwenzake wananishauri kila mtu anunuliwe computer yake kumaliza tatizo.
Hawana habari kuwa sisi sahani moja ya ugali tunakula watoto zaidi ya saba na hatugombanii chochote si katika ugali wenyewe wala yale maharage au dagaa.
Nikawaeleza kibatari kilivyo.
Kama ningewawashia kibatari chumbani kwao wote wangekimbia wanaogopa nyumba itawaka moto.
Hii shida ya umeme kazi nyingi zimesimama.
Maktaba huwezi kuifungua gizani.
Waingereza wana msemo: "An idle mind is a workshop for the devil," yaani ubongo usio na kazi ya kufanya ni karakana ya shetani."
Kutwa nzima sijaandika hata maneno 1000 naona shida.
Sasa kuepuka mimi kuwa gereji ya Iblis nimeona nitafute taa ya solar inisaidie kumulika Maktaba na kuiona keyboard.
Huo hapo chini ndiyo muonekano wa Maktaba nilipokiwasha kibatari cha Mchina leo TANESCO walipochomoa waya wao.
Kazi inaendelea.