Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,897
- 30,235
KATIKA KUTENGENEZA KIPINDI CHA SIKU YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Sijapata kufanya kipindi kama hiki.
Jua lilikuwa kali sana asubuhi ya saa tatu.
Gari la Azam TV lina ''full kiyoyozi,'' pembeni yangu amekaa Jaffar Mponda mtayarishaji wa kipindi hiki na hapo tulipokaa miguu yetu tumenyoosha kama vile tuko kwenye Emirates ''business class.''
Ipo nafasi ya kutosha sana ya kunyoosha miguu hata kuweka nne yaani unaonyanyua mguu mmoja unauweka juu ya mwingine.
Mponda alikuwa anapanga kipindi hiki siku nyingi na alikuja na wazo kuwa itapendeza sana ikiwa katika kumuenzi Mwalimu Nyerere tukafanya kipindi kueleza nyumba ambazo Mwalimu aliishi na halikadhalika sehemu ambazo zina kumbukumbu ya matukio muhimu katika historia yake Baba wa Taifa.
Zaidi akashauri kuwa kipindi hiki tukifanyie mabadiliko makubwa badala ya kufanya kipindi Maktaba iliyoko nyumbani kwangu tuhame twende kwenye nyumba na sehemu zinazomuhusu Mwalimu na yalipotokea matukio yenyewe.
Mwalimu kaishi Kariakoo ile ya miaka ya 1950 Karikaoo iliyokuwa na soko lililoezekwa kwa mabati na yote aliyofanya siku zile sasa imepita miaka 70.
Mwalimu kaikuta ofisi ya TANU New Street barabara ya vumbi na jengo lilijengwa kati ya mwaka wa 1929 - 1933.
New Street leo ni Lumumba Avenue na TANU haipo kuna CCM yenye ofisi ya kupendeza.
Huu ni mwendo mrefu sana.
Kutoka mwaka wa 1929 hadi leo ni miaka 93.
Nimempitisha Jaffar Mponda sehemu kadhaa ambazo zina historia za kusisimua lakini kwa bahati mbaya ni historia ya mambo ambayo watu wachache sana wanafahamu.
Tumeingia Mtaa wa Sikukuu tukitokea Mtaa wa Uhuru tunaelekea nyumba iliyokuwa ya Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey kiasi cha saa tatu asubuhi.
Hii ndiyo nyumba ya kwanza Mwalimu aliishi mwaka wa 1955 baaada ya kuacha kazi ya Ualimu Pugu.
Mtaa huu umebadilishwa jina mara kadhaa kuanzia Stanley, Aggrey hadi sasa unaitwa Makisi Mbwana lakini kibao hakijabadilishwa bado kinasomeka kibao cha zamani Aggrey ingawa ''spelling'' ya jina imekosewa vibaya sana ''Agray.''
Majina yote haya yana uhusiano mkubwa na historia ya Tanganyika.
Jua ni kali sana, watu na magari yameshonanana mwendo wa binadamu na vyombo vya moto magari, bodaboda na Bajaj zimejaza barabara yote.
Kama haya hayatoshi pembeni mwa barabara wafanyabiashara wameweka bidha zao kuanzia vikabu vyenye ubuyu wa Zanzibar wa kila rangi hadi nguo na vitu vingi.
Dereva wetu Bwana Ismail kaibanisha pembeni gari tushuke haraka na mizigo yetu vifaa vya kazi camera, stendi na korokoro nyingine.
''Bye bye,'' kiyoyozi nalisikia joto na jua kali linanipiga vizuri.
Tuko kwenye kona ya Makisi Mbwana na Sikukuu huoni zaidi ya mgongo wa mwenzako.
Watu wameona gari la Azam linashusha watu na camera wakajua leo hapa kuna jambo.
Muda si muda tumezingirwa.
Nimeipa mgongo biashara ya dada mmoja namtaka radhi.
Jaffar Mponda yuko tayari na mike yake na mtu wa camera ''headphones,'' kichwani, anampa ishara ya vidole kuwa yeye yuko tayari.
Anaanza kuzungumza.
Namuonyesha nyumba ya Abdul Sykes ile ya zamani ambayo haipo badala yake kuna ghorofa.
Sote tunaangalia jengo zuri la gorofa tano.
Naeleza upande wa nyumba ile ya zamani iliyojengwa mwaka wa 1942.
Naeleza na naonesha upande wa nyumba aliyokuwa anaishi Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru.
Mlango wake aliokuwa akiingia na kutokea ulikokuwa Mtaa wa Sikukuu.
Naeleza aivyokuwa anatembea kwa miguu kutoka pale anaelekea Soko la Kariakoo asubuhi anakwenda ofisini kwa Abdul Sykes ofisi ambayo zamani ilishikwa na Brian Hodges Mwingereza.
Nendelea kueleza na wasikilizaji wangu nawaona wako makini sana historia hii imewavutia.
TANU imepamba moto Soko la Kariakoo na kwa Mwalimu kuwa pale sokoni watu sasa ndiyo wanaanza kumfahamu Rais wa TANU chama kinachopigania uhuru wa Mwafrika katika nchi yake.
Wasikilizaji wameongezeka sasa wamenizunguka wananisikiliza kwa makini na wanasikilkiza maswali ninayoulizwa na Jaffar Mponda.
Gumzo limenoga...
Tulipomaliza watu wametuzunguka kama vile wanatuzuia tusiondoke wanataka kujua zaidi historia ya nyumba ile ambayo haipo badala yake kuna jumba ambalo wao kwa miaka sasa wanaliona pale lakini hawakuwa wanafahamu kuwa hapo ndipo Baba wa Taifa alipoanza kampeni yake na TANU dhidi ya ukoloni wa Mwingereza.
Kazi yetu hapo imekamilika.
Hatuna muda tunakimbilia nyumbani kwa Clement Mtamila Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) ukivuka Mtaa wa Uhuru ushafika ilipokuwa nyumba yake.
Hapa ndipo palipofanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya TANU mwenyekiti akiwa Mzee Mtamila kujadili barua ya Mwalimu kutoka kwa mwajiri wake iliyomtaka achague siasa au kazi ya ualimu.
Mponda anawatuliza watu na maswali yao anawaambia wawe na subra kipindi kitarushwa siku ya Nyerere Day.
Kutoka ilikpokuwa nyumba ya Mzee Clement Mtamila tukavuka upande wa pili wa Mtaa wa Sikukuu tukasimama kwenye kona ya Mtaa wa Lindi na Sikukuu kuangalia sehemu ambayo Mwalimu Nyerere siku moja akipita mitaa ya Gerezani alimuona Bi. Mruguru bint Mussa, mama yake Abdul Sykes akasimamamisha masafara wake akatoka ndani ya gari kumwamkia.
Vijana wa bodaboda waliokuwa pale walisisimkwa na kisa hiki.
Wanamjua Nyerere lakini hawamjui Bi. Mruguru wala hawajamsikia Abdul Sykes.
Tulipotoka hapo tukaenda Mtaa wa Kipata alipokuwa akiishi Ally Sykes na mkewe Bi Zainab.
Nyumba ndogo ya kawaida haipo na badala yake kuna gorofa ndefu ya kuishi watu na chini kuna ofisi na maduka.
Hapa nilihadithia kisa cha mashine iliyokuwa ikichapa makaratasi ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TAA mashine ambayo Special Branch makachero wa serikali walikuwa wanaitafuta.
Nikaeleza na kikao kilichofanywa hapo mwezi Julai 1954 kati ya Abdul Sykes, Ally Sykes na Julius Nyerere kupokea kutoka kwa Nyerere taarifa ya tasjila ya TANU mara tu baada ya kupeleka maombi ya kusajili TANU.
Waingereza walikataa kuisajili TANU.
Tulipotoka hapo tukaende Arnautoglo Hall mahali ambao mwaka wa 1953 Nyerere aligombea nafasi ya urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes.
Nilimuonyesha Mponda ukumbi wenyewe ulipofanyika mkutano na kueleza ilikuwaje hadi Nyerere kufika pale na kueleza kuwa hafla ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO ilifanyika Ukumbi wa Arnautoglu na safari ya kwanza hafla ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Mtaa wa Stanley na New Street.
Tukaondoka hapo tukaenda Mtaa wa Lumumba na Kariakaoo kwenye nyumba ya Bi. Mwamtoro bint Chuma aliyekuwa akivunja ua wake na kuunganisha na ua wa TANU kila Mwalimu alipokuwa anataka kuwa na mkutano wa ndani na wanachama wa TANU.
Nyumba hii bado ipo hadi leo ngawa watu wachache sana ndiyo wenye kuijua historia yake na Mwalimu Nyerere.
Tukahitimisha kwa kufika Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Mtaa wa Ifunda Magomeni.
PICHA:
Mwandishi akizungumza.
Jaffar Mponda.
Watu wanasikiliza.r
Nyumba ya Abdul Sykes ya zamani aliyoishi na Julius Nyerere na nyumba ya sasa.
Bi. Mruguru bint Mussa.
Kushoto wakwanza aliyesimama ni Said Chamwenyewe na wa mwisho kulia waliokaa ni Mzee Clement Mtamila.
Ally Sykes na Julius Nyerere 1958.
Ukumbi wa Arnautoglu kama ulivyokuwa 1950.
Abdul Sykes na Nyerere Ukumbi wa Arnautoglu, 1956.
Bi. Mwamtoro bint Chuma akipiga kura 1970.
Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Haidar Mwinyimvua mama alikuwa mstari wa mbele TANU na halikadhalika mtoto wake.