Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]

Maktaba na Makumbusho ya Urais [Presidential Libraries & Museums]

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,313
Reaction score
144,691
Tangu miaka ya mwisho ya '30 [1930s] wenzetu Wamarekani wamekuwa na utaratibu wa kujenga maktaba na makumbusho ya marais wao waliopita.

Mpaka sasa wana maktaba na makumbusho hayo arubatashara [hiyo ni 14/ kumi na nne kwa wale mliokuja Dar ukubwani...natania tu hahahaa]. Kuanzia kwa FDR hadi Barack Obama [ingawa huyu yake bado haijaisha kujengwa, kama sijakosea].

Lengo kuu la maktaba na makumbusho hayo ni kuhifadhi historia muhimu ya taifa kwa kuyaweka sehemu moja mambo yamhusuyo rais wa kipindi husika na hivyo kuwa rahisi kufanya tafiti na kujifunza.

Sasa kwa Tanzania sijui tunafanyaje. Makumbusho ya taifa?

Kama kuna mambo ambayo ni mazuri kuiga toka kwa wenzetu hawa basi hili la maktaba na makumbusho ya urais ni mojawapo.

Sasa hivi hata historia za marais wetu nadhani wengi wetu hatuzijui vizuri. Lakini zikiwepo maktaba za hii basi naamini watu tutapata fursa nzuri sana ya kujifunza kuhusu taifa letu na watu waliopata kuliongoza.

Pichani ni jengo la maktaba na makumbusho ya rais wa 41 wa Marekani, George Herbert Walker Bush [au Bush Sr. ukipenda] huko College Station, Texas.

8684094428.jpg
 
Kumbuka historia ya Tanganyika/Tanzania ilipindishwa na watawala wa kwanza na kwa mantiki hii hata nyaraka zimejaa maandiko ambayo hayana uhalisia.

Hii siyo kwa Tanzania pekee bali kwa nchi nyingi zilizokuwa na mlengo wa kikomunisti. Hazina historia ya kweli.

Karibu kila nyaraka ya Rais inagongwa muhuri wa siri!

Kikubwa zaidi hata viongozi wetu ni vigumu sana kujua maisha yao halisi ndiyo maana kwa mfano utasikia mtu kama Yericko Nyerere anakuambia ni mtoto wa Mwl. Nyerere au ana undugu wa karibu wakati ni uwongo.

Kama historia ya watawala wetu ingekuwa inafahamika ninaamini tusingepata matapeli wa historia au wanaojifanya ni ndugu wa karibu wa watawala.

Ukichunguza utagundua hata hii taasisi ya Mwl. Nyerere haiko wazi kwenye nyaraka za Mwl. Nyerere kutokana na sababu nilizozisema.

Wenzetu kila kiongozi akitaka kugombea Urais ni kawaida ataandika kitabu ili kuelezea maisha yake. "Sisi ni siri kwa manufaa ya usalama wa taifa"

Fikiria hatujui hata watoto wote wa wenyeviti wa vyama vyetu vyote vya siasa nchini na pia hata watoto wote wa marais wastaafu.
 
Tanzania pia tumeanza tunajenga ya Nyerere na Karume

Hatimaye Serikali yawaenzi Rasmi 'Nyerere na Karume'! Yawaundia Bodi ya Kuwaenzi!

Sijapata update wamefikia wapi.

P
Wanaunda Bodi kweli serious, Hizi bodi za tumbua tumbua kila siku, Bodi za kwenye makaratasi tutafika kweli

Ndio maana mpaka leo Viongozi wa Tanzania hawatakumbukwa kwa kitu walicholifanyia Taifa bali wanakumbukwa na kukumbukwa kwa maneno wanayosema na waliyosema

Ukiuliza hawa watu wamelifanyia nini Taifa hakuna jibu ila ukiuliza walisema matamko mangapi real we will remember

Haina haja ya kuweka makumbusho ya matamko na vitisho
 
Tanzania pia tumeanza tunajenga ya Nyerere na Karume
Hawa kuna VITU vya kumbukumbu walivyofanya, kusema na kuandika ambavyo vinaweza kuwa sehemu kubwa ya Amali ya kuhifadhi. Mwalimu Nyerere alikuwa Mwandishi na Msomaji mahiri. Alikuwa na Hotba ambazo waweza kuzihifadhi katika maandishi kama vitabu. Je, huyu Raisi wa sasa hotba zake, kwa mfano, zaweza kuhifadhiwa katika maandishi na kuvutia wasomaji?
 
Back
Top Bottom