Maktaba Imepokea: ''Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Photographic Journey''

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
MAKTABA IMEPOKEA: MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE PHOTOGRAPHIC JOURNEY

Rafiki yangu ndugu Ali Sultan mmoja wa watayarishaji wa kitabu hiki kikubwa cha Mwalimu jana alikuwa Ikulu Dodoma kwa uzinduzi wa kitabu hiki.

Leo kafika Maktaba kunikabidhi kitabu.

Kiswahili hakina msamiati wa kueleza shukurani zangu kwake.
"Nayajua mapenzi yako kwa Mwalimu," kaniambia akinikabidhi hazina hii.

Kitabu hiki kina historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika katika picha na maelezo.
Yapo mengine mengi katika maisha ya Mwalimu.

Maneno hayatoshi kueleza yaliyomo ila uwe na kitabu hiki wewe mwenyewe mkononi unafungua ukurasa baada ya ukurasa.

Hakika kazi kubwa imepitika.
Tuna deni kubwa kwa waandishi wa kitabu hiki ambalo si rahisi kulilipa.

1745769484779.jpeg
 
Natumaini wazee wako wamewakiliswa ipasavyo katika hicho kitabu
Yoda,
Wazee wangu ni kitu kingine kabisa katika historia ya Mwalimu.

Endapo nitakuwekea picha nilizonazo kwenye Maktaba na nikakuwekea maelezo nina hakika utashangaa kupita kiasi.

Kuna picha ya Mwalimu Nyerere Maktaba ambayo nimepewa na marehemu Maulidi "Chubby," Tosiri inamuonyesha Mwalimu aneshika mkuki na ngao.

Nadhani hii ni katika picha za mwanzo sana za Nyerere baada ya kuundwa TANU 1954.

Maulidi ni mtoto wa Iddi Tosiri ambae kadi yake ya TANU ni no. 25 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954 Arnautoglo Hall.

Katika Photographic Journey ipo picha ambayo Iddi Tosiri yupo na Mwalimu na wanachama wengine wa TANU, New Street.

Picha hii ipo Maktaba na nilipewa pia na marehemu Maulid Tosiri.

Picha nyingine ya zamani sana ya Mwalimu katika TANU nilipewa na Faiz Mafungo, mtoto wa Iddi Faiz Mafungo.

Huyu Iddi Faiz Mafungo na Iddi Tosiri ni ndugu na kadi yake ya TANU ni No. 24 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo.

Iddi Faiz Mafungo ni Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Picha hii niloyopewa na Faiz Mafungo imepigwa Dodoma mwaka wa 1955 au 1956.

Inamwonyesha Mwalimu, Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.

Iddi Tosiri, Iddi Faiz Mafongo na Sheikh Mohamed Ramiyya hawa watatu ni ndugu na Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafongo ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo mguu kwa mguu kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.

Picha nyingine ya zamani mwanzoni inaundwa TANU niliipata kwa Jim Bailey ilipigwa mwaka wa 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Nyerere UNO.

Hizi ni picha mbili.
Nyingine yuko Nyerere na Iddi Faiz Mafungo hapo uwanja wa ndege.

Iddi Faiz Mafongo ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO.

Picha hii yuko Mwalimu, Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas), Tatu bint Mzee, Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck.

Nina picha ya 1955 nilipewa na Bilal Rehani Waikela Nyerere yuko Tabora pamoja na Titi Mohamed, Bilal Rehani Waikela na wanachama wa New Young Strong Team katika juhudi ya kuunda TANU.

Picha nyingine ni ya 1956 safari ya pili ya Mwalimu UNO imepigwa Arnautoglo Hall dhifa ya kumuaga Mwalimu yuko Abdulwahid Sykes, Nyerere, Dossa Aziz na Nangwanda Lawi Sijaona.

Picha hii alinipa mtoto wa Abdul Sykes, Kleist Sykes.

Nyingine Mwalimu yuko Shambani kwa Chaurembo, Mtoni 1956 kwenye dua ya kuomba salama kwa harakati za kudai uhuru.

Dua hii ilifanyika baada ya watu kutoka Hijja na ilihudhuriwa na masheikh wengi na watu maarufu wa mji wa Dar-es-Salaam.

Picha hii alinipa Mohamed Chaurembo sasa yapata miaka 40 lakini maelezo ya picha nilipata kwa Sheikh Iddi Chaurembo mtoto wa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo.

Yapo mengi.
 
MAKTABA IMEPOKEA: MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE PHOTOGRAPHIC JOURNEY

Rafiki yangu ndugu Ali Sultan mmoja wa watayarishaji wa kitabu hiki kikubwa cha Mwalimu jana alikuwa Ikulu Dodoma kwa uzinduzi wa kitabu hiki.

Leo kafika Maktaba kunikabidhi kitabu.

Kiswahili hakina msamiati wa kueleza shukurani zangu kwake.
"Nayajua mapenzi yako kwa Mwalimu," kaniambia akinikabidhi hazina hii.

Kitabu hiki kina historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika katika picha na maelezo.
Yapo mengine mengi katika maisha ya Mwalimu.

Maneno hayatoshi kueleza yaliyomo ila uwe na kitabu hiki wewe mwenyewe mkononi unafungua ukurasa baada ya ukurasa.

Hakika kazi kubwa imepitika.
Tuna deni kubwa kwa waandishi wa kitabu hiki ambalo si rahisi kulilipa.

View attachment 3317692
Huyo sasa ndiye mwandishi tunataka siyo wewe uandishi wako wote unatetea familia ya Kleist Sykes na wanae. Wenyewe hawajawahi kulalamika kwa kuwa JKN aliwapa fursa. Ila wewe 24/7 kupotosha historia yetu nzuri.

Najuwa machungu na husda uliyonayo moyoni japo umekipokea
 
Picha hii yuko Mwalimu, Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas, Tatu bint Mzee, Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck.

Muuliza swali alitaka kujua kama jina Sykes limo cc Yoda
 
Stuxnet,
Hapana "sijatetea."

Nimeandika historia ya Sykes na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika kama wengine walivyoandika mchango na historia ya Mwalimu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sina hasad.
Nimeshiriki katika kuhariri na kutafuta mchapaji wa kitabu, "Tanzania The Story of Julius Nyerere," (1993).

Halikadhalika nimeshiriki katika kuandika maisha ya Julius Nyerere (2020) iliyoandikwa na Prof. Shivji at al.

1745812423747.png

1745812524234.jpeg

Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr,
Ng'wanza Kamata wakinihoji kuhusu Mwalimu
(sionekani).
 
nina swali nje ya mada kidogo, kwa nini waislamu wanapenda sana communism? i mean, hata walioleta communism tanzagiza ni waislamu, je, kuna uhusiano wowote kati ya uislamu na communism? kwa maana ukiangalia karibia nchi zote zenye waislamu wengi kuna commumism …
 
Muuliza swali alitaka kujua kama jina Sykes limo cc Yoda
Njinjo,
Abdulwahid na Ally Sykes majina yao yapo, "Formation of TANU (7 July 1954)," lakini kwa bahati mbaya kuna kosa badala ya kuweka picha ya waasisi wa TANU wameweka picha ya Mwalimu na Kamuzu Banda na watu wengine New Street.
 
Yoda,
Wazee wangu ni kitu kingine kabisa katika historia ya Mwalimu.

Endapo nitakuwekea picha nilizonazo kwenye Maktaba na nikakuwekea maelezo nina hakika utashangaa kupita kiasi.

Kuna picha ya Mwalimu Nyerere Maktaba ambayo nimepewa na marehemu Maulidi "Chubby," Tosiri inamuonyesha Mwalimu aneshika mkuki na ngao.

Nadhani hii ni katika picha za mwanzo sana za Nyerere baada ya kuundwa TANU 1954.

Maulidi ni mtoto wa Iddi Tosiri ambae kadi yake ya TANU ni no. 25 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU August 1954 Arnautoglo Hall.

Katika Photographic Journey ipo picha ambayo Iddi Tosiri yupo na Mwalimu na wanachama wengine wa TANU, New Street.

Picha hii ipo Maktaba na nilipewa pia na marehemu Maulid Tosiri.

Picha nyingine ya zamani sana ya Mwalimu katika TANU nilipewa na Faiz Mafungo, mtoto wa Iddi Faiz Mafungo.

Huyu Iddi Faiz Mafungo na Iddi Tosiri ni ndugu na kadi yake ya TANU ni No. 24 na alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo.

Iddi Faiz Mafungo ni Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Picha hii niloyopewa na Faiz Mafungo imepigwa Dodoma mwaka wa 1955 au 1956.

Inamwonyesha Mwalimu, Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu.

Iddi Tosiri, Iddi Faiz Mafongo na Sheikh Mohamed Ramiyya hawa watatu ni ndugu na Iddi Tosiri na Iddi Faiz Mafongo ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo mguu kwa mguu kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.

Picha nyingine ya zamani mwanzoni inaundwa TANU niliipata kwa Jim Bailey ilipigwa mwaka wa 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Nyerere UNO.

Hizi ni picha mbili.

Nyingine yuko Nyerere na Iddi Faiz Mafungo hapo uwanja wa ndege.

Iddi Faiz Mafongo ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya UNO.

Picha hii yuko Mwalimu, Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas, Tatu bint Mzee, Bibi Titi Mohamed na Lucy Lameck.

Nina picha ya 1955 nilipewa na Bilal Rehani Waikela Nyerere yuko Tabora pamoja na Titi Mohamed, Bilal Rehani Waikela na wanachama wa New Young Strong Team katika juhudi ya kuunda TANU.

Picha nyingine ni ya 1956 safari ya pili ya Mwalimu UNO imepigwa Arnautoglo Hall dhifa ya kumuaga Mwalimu yuko Abdulwahid Sykes, Nyerere, Dossa Aziz na Nangwanda Lawi Sijaona.

Picha hii alinipa mtoto wa Abdul Sykes, Kleist Sykes.

Nyingine Mwalimu yuko Shambani kwa Chaurembo, Mtoni 1956 kwenye dua ya kuomba salama kwa harakati za kudai uhuru.

Dua hii ilifanyika baada ya watu kutoka Hijja na ilihudhuriwa na masheikh wengi na watu maarufu wa mji wa Dar-es-Salaam.

Picha hii alinipa Mohamed Chaurembo sasa yapata miaka 40 lakini maelezo ya picha nilipata kwa Sheikh Iddi Chaurembo mtoto wa Sheikh Abdallah Iddi Chaurembo.

Yapo mengi.
Tunasubiri Lissu anyongwe na Samia, ili wajukuu zako waje kuandika mchango wa wazee wako kwenye mageuzi ya mfumo wa uchahuzi na vita dhidi ya ubaguzi, ufisadi, dhulma na mauaji
 
nina swali nje ya mada kidogo, kwa nini waislamu wanapenda sana communism? i mean, hata walioleta communism tanzagiza ni waislamu, je, kuna uhusiano wowote kati ya uislamu na communism? kwa maana ukiangalia karibia nchi zote zenye waislamu wengi kuna commumism …
Kijakazi,
Nifahamishe nchi zenye Waislam wengi walio Wakomunisti.
 
Tunasubiri Lissu anyongwe na Samia, ili wajukuu zako waje kuandika mchango wa wazee wako kwenye mageuzi ya mfumo wa uchahuzi na vita dhidi ya ubaguzi, ufisadi, dhulma na mauaji
Huo sasa ni uchuro. Unatoka nje ya biti kizembe
 
Nmaanisha hawa wahuni baada ya mwaka 1961 waliona wamemaliza.

Kila siku Nyerere Nyerere aliwanyima ulaji, utafikiri nchi hii matatizo yameisha.

Leo Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uongo ya kunyongwa ila wako kimya kama vibudu.

Kama ni wapenda haki, mbona hatuoni hiyo haki wakiitetea.
 
MAKTABA IMEPOKEA: MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE PHOTOGRAPHIC JOURNEY

Rafiki yangu ndugu Ali Sultan mmoja wa watayarishaji wa kitabu hiki kikubwa cha Mwalimu jana alikuwa Ikulu Dodoma kwa uzinduzi wa kitabu hiki.

Leo kafika Maktaba kunikabidhi kitabu.

Kiswahili hakina msamiati wa kueleza shukurani zangu kwake.
"Nayajua mapenzi yako kwa Mwalimu," kaniambia akinikabidhi hazina hii.

Kitabu hiki kina historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika katika picha na maelezo.
Yapo mengine mengi katika maisha ya Mwalimu.

Maneno hayatoshi kueleza yaliyomo ila uwe na kitabu hiki wewe mwenyewe mkononi unafungua ukurasa baada ya ukurasa.

Hakika kazi kubwa imepitika.
Tuna deni kubwa kwa waandishi wa kitabu hiki ambalo si rahisi kulilipa.

View attachment 3317692
Hongera mwanahistoria naamini kuna mchango wako kwenye hicho kitabu.
 
Back
Top Bottom