makovu mwilini

makovu mwilini

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
15,347
Reaction score
11,626
Helo team, tusiokuwa na viburudisho ! hebu kujeni hapa tupige story leo weekend kama unaona haikuhusu naomba upotezee!

Najua wengi wetu tuna makovu kwenye miili yetu madogo kwa makubwa! Wengine waliungua udogoni,wengine wamepigwa mapanga kwa ujambazi wengine mafumanizi nk!

Leo naomba tupige story kila mtu amwage kisa cha kovu lake hapa.Mimi ninalo kwenye bega sema kwa ajili ya unene huu na kukua naona limeishia ishia limebaki kwa mbaali sana ila linanikumbusha mbali sana
story yangu ilikuwa hivi.

Nikiwa mdogo kuna siku mama yangu akanituma buchani nyama nusu kilo, akanipa elfu kumi ndio zimetoka toka nadhani nilikuwa sijawahi kuiona tena! sio hii ya sasa hivi. Nusu kilo ya nyama nadhani ilikuwa elfu au mia tano hivi.

Sasa kule buchani yule muuza bucha akanipa nyama na chenji wakati mimi nilikuwa sijampa hata hela huyooo nikaishia zangu.So ile elfu kumi ya mama ikawa yangu mi nikampa mama chenji yake.

Kuna ndugu yangu tumefatana ila kanizidi miaka 4 nikamueleza jinsi nilivyopata hilo zali asubuhi asubuhi hao tukaenda kufunga mtaa kwa pipi gololi na biscuit za bibi! Ila kumbe mwenzangu roho ilimuuma so ikatokea sasa mama akitaka kumtuma mtu buchani anagombania sana na mimi sikubali ikawa ni vita vita!

Siku moja katika kupigana na akanibamiza ukutani ule ukuta una chuping sijui mafundi wanaita wenyewe ukanichumbua ndio source ya kovu langu!
 
liko wapi?
mbona wewe makovu unayo mengi tu....au huyajui?
ya kuzaliwa huyaoni? lol
 
liko wapi?
mbona wewe makovu unayo mengi tu....au huyajui?
ya kuzaliwa huyaoni? lol
ahaaa mi sina mengi bwana...kuna wanafunzi niliona shule wameungua makalio aisee utoto sijui sasa hivi wanauzikaje sokoni duniani hapa na kaka zetu mlivo na mashauzi...
 
ahaaa mi sina mengi bwana...kuna wanafunzi niliona shule wameungua makalio aisee utoto sijui sasa hivi wanauzikaje sokoni duniani hapa na kaka zetu mlivo na mashauzi...

Show me your tattoo and i will show you mine lol
cc Nyani Ngabu...
 
Last edited by a moderator:
kuna mtu humu alisema wewe ni jini hata utajwe saa ngapi unatokelezea dah ! miss u big time my super mkareee baby yakeee smile!
cc@Superman

Hahahaaaa.....mimi niko 'wired' 24/7.

Hata nikiwa gym nasukuma ratili bado access ya mtandao ninayo.

Super mbebs mkareeez majuu watasubiri sana mwaka huu.
 
Hahahaaaa.....mimi niko 'wired' 24/7.

Hata nikiwa gym nasukuma ratili bado access ya mtandao ninayo.

Super mbebs mkareeez majuu watasubiri sana mwaka huu.
ahaaa hiyo wired yako nadhani hata ya jk haifui dafu mzee ..umenikumbusha kitu ngoja niingie gym bana...thax mjini hapa kila kitu kwa mchina utapata isipokuwa kiuno aka nyonga
 
ahaaa hiyo wired yako nadhani hata ya jk haifui dafu mzee ..umenikumbusha kitu ngoja niingie gym bana...thax mjini hapa kila kitu kwa mchina utapata isipokuwa kiuno aka nyonga

JK ain't got nothing on me.

Unavaaga nini ukienda gym? Sports bra? One piece? Two piece?
 
Mie ninalo pembeni ya shingo, upande wa kushoto.
Aisee...sitasahau.
 
ahaaa hiyo wired yako nadhani hata ya jk haifui dafu mzee ..umenikumbusha kitu ngoja niingie gym bana...thax mjini hapa kila kitu kwa mchina utapata isipokuwa kiuno aka nyonga

Cant wait to see u itv asubui. Kuna mdada mmoja anakiuno balaa.
 
Back
Top Bottom