MAKOSA YANGU MZIGO WANGU (simulizi) seh 01.

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Ni bora nijuue kuliko haya yatayo nifika, nitakufa kikatili na kupoteza kila kitu nilichokipigania kwa jasho na vitisho ( Vera aliongea na moyo wake akiwa kwenye basi akitokea wilaya ya handeni kuelekea nyumbani kwake makorora mtaa wa Gatundu).

Wakati huu siyo wa kupoteza bora nikalipe na kuweka fedha kwenye kampuni kwa ajili ya mwanangu Delvin, wakija kunimalizia mwanangu asikose maisha bora ( aleandelea kuwaza).

Gari aina ya Costa iliendelea kusafiri hadi kupita barabara ya Handeni, waliingia njia ya korogwe , hatimaye walifika kituo cha mabasi Muheza, gari ilishusha abiria na kupakia abiria wengine na kuendelea na safari.

Ikiwa getini kuna mwanaume, aliingia kama abiria akiwa amevaria kanzu nyeupe na alikuwa na harufu kali sana ya pafyumu, alitazama pa kuketi , siti aliyokaa Vera ilikuwa tupu kiti kimoja, alielekea na kuketi na kumsalimia “ hallo dada Vera, asalam aleikum?”
Vera: salama, karibu, umenijuaje?
Nyahega: yah! Wewe tena mjasiliamali mkubwa, karibia kila mtu humu ndani anakujua, za mtoto wako kipenzi?

Vera: mmh! Kweli unanijua, hajambo ndio naelekea hivi nilikuwa safarini hivyo sijaonana nae siku ya tatu leo yaenda ya nne.

Nyahega: vyema (gari iliondoka) ila amefanana sana na baba yake, dah Yule jamaa bwana alijizaa aisee ameacha alama yake.

Vera: ni kweli , kila jambo la Mungu, saizi ndio hayupo tena nendelea kumlea mwenyewe.

Nyahega: ila wewe ni bonge la mwanamke vera.

Vera: why?

Nyahega: Umepambana sana. I wish nami niwe na maendeleo kama wewe.

Vera: no! utafika wala usiwe na haraka, umeoa?

Nyahega: yes, na watoto watatu, vipi unataka nikuongeze uwe mke wa pili?

Vera: Uwii! Hapana nimependa tu kujua how rensponsible you are, kuoa na kuwa baba sio kitu kidogo.

Nyahega: yah! ( kondakta anaita, wakushuka Pongwe, pongwe wanaoshuka Pongwe)

Vera: Good( simu yake inaita ulikuwa ni ujumbe umeingia) alichukua simu yake na kuusoma ule ujumbe ila alipousoma aliamsha kichwa vyem na kuangalia kushoto na kulia.

Ujumbe ulieleza “ jikaze utachoona njiani, usishtuke”
Alipoitazama namba iliyotuma ujumbe ilikuwa haionekani na alipojaribu kuipiga ilishindwa kwenda, aliamua kupuuza na kuendelea na mawazo ya safari aendayo.

Muda ulipoenda iliingia ujumbe wa pili, alitoa simu na kutazama tena aliona ni mtumaji Yule Yule ambaye namba yake haionekani.
“ kuwa mtiifu kwa kila jambo, utaeleweka” . aliwaza kuwa ni kweli huko alikotoka kilicho mfanya arudi hai ni utiifu la sivyo asingerudi hai.
******* ------- ***

Moja ya simulizi tamu kati ya simulizi zangu zenye kufunza, kusisimua na kuburudisha, sijaisahau hii kama ni msomaji wa gazeti la Mwangaza "NYUMBA YA KUPANGA ILIVYOHARIBU MAISHA YANGU".
#karibu
textgram_1653898400.jpg
 
itafika mwisho au tusijihangaishe kusoma vitu vya kubuni tu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom