Kama mnaziona hizo opportunities, mnawashawishi vipi wananchi kuwa mna uwezo wa kuongoza bila pasipo shaka?
Hata hivyo, Mh Zitto failure comes from within na waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako. Muuaji wa upinzani ni upinzani wenyewe kuendekeza mambo yanayoipa system uwezo wa kuwafanyia hujuma. Sidhani kama Mrema alikuwa hajui uwezo wa serikali baada ya kutoka nje. Ila ndo hivyo tena ajilaumu mwenyewe
Duh, umetupiga sana. Hata hivyo unfairly. Unapoangalia makosa ya kambi ya upinzani ni vema uangalie 'factors' za ndani na za nje. Katika SWOT analysis hizi ni fursa na vitisho. Hapo utaweza kutoa hukumu sahihi kabisa.
Vilevile ni muhimu sana kuangalia historia ya vyama hivi katika muktadha wa historia ya Tanzania na utamaduni wa kisiasa wa Watanzania. Vyama katika nyakati tofauti - kuanzia kina Marando na Bagenda, Mtei na Makani, Fundikira na Kasanga Tumbo na Mapalala na Seif walipoamua kujitoa mhanga na kuanzisha vyama - kumekuwa na hatu kadhaa zimepigwa katika kujenga dmeokrasia ya kweli katika nchi yetu.
Watu wanaiweka Tanzania katika mizania ya nchi nyingine jambo ambalo ni kosa kubwa maana Tanzania inapaswa kupimwa kutokana na historia yake. Zoezi la ujenzi wa Taifa na kuwa na Taifa moja chini ya uongozi mahiri wa Mwalimu lilifanywa katika misingi ya udikteta mkubwa sana na chini ya amri moja ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tanzania ikajenga jamii ya watu wanaoheshimu mamlaka bila kuhoji na hata vyama vingi vilipoanzishwa vilionekana ni vya wasaliti. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa ambaye alikonga nyoyo za Watanzania na kuaminiwa - Augustino Lyatonga Mrema - lakini naye akavurugwa sana na dola, kuitwa pandikizi na kuondoa kabisa credibility yake katika jamii. Jamii imefanywa kuamini kuwa Mrema ni 'kichaa' na hana sifa ya uongozi. Hii ni kazi iliyopangwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba leo ni watanzania wachache sana ambao wanakumbuka sacrifice ya Mrema katika ujenzi wa demokrasia nchini.
Tusipojifunza na kuelewa historia hii ya vuguvugu la demokrasia Tanzania tutaishia kulaumu watu kila kukicha bila kwenda mbele. CCM itaendelea kutawala na kila baada ya miaka mitano kutakuwa kinatokea chama kina nguvu na baadae kuangushwa, wabunge wenye nguvu na baadae kuangushwa na hata wanasiasa wenye mvuto na baadae kupakwa matope na kunuka.
Demokrasia hulindwa. Viongozi hulindwa zaidi ili kubakia kama alama ya harakati. Raila Odinga aliongoza harakati za mapinduzi Kenya mwaka 1982, akaswekwa lupango kwa miaka zaidi ya tisa na kuishi uhamishoni nchini Norway kwa miaka mingi. Akajiunga na chama cha baba yake mwaka 1992 FORD, kikavunjika na kuwa na FORD-K na FORD-A. Baba yake Mzee Jaramogi alipokufa Raila akataka kunyakua uongozi wa chama, akashindwa na Michael Kijana Wamalwa na Raila akaenda kuanzisha chama chake NDP. Akaivunja NDP na kuingia KANU kuwa Katibu Mkuu na akaipasua KANU vipande 2 na kuanzisha LDP. Akaingiza LDP katika muungano wa NARC na kumpa Kibaki Urais (literally alimpa Urais maana Kibaki alikuwa armchair leader of opposition). Akatoka NARC na kuanzisha ODM-K, akagombana na Kalonzo na kuanzisha ODM na leo ni Waziri Mkuu mwenye nguvu Kenya.
Mchakato wote huu Raila alionekana msaliti, mpenda vyeo na mtu wa vita. Lakini leo huna tena KANU na Raila alipata kuniambia, demokrasia Afrika itaimarika tu iwapo vyama vilivyoleta uhuru vitapasukapasuka na kuondoa ile claim yao ya sisi tulileta uhuru - hii ni claim ya CCM na hata kumkumbatia Mwalimu kama wao.
Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
Mwanakijiji utaandika mpaka utachoka na kutulaumu mpaka utakasirika. Demokrasia ya Tanzania itajengwa kwa sober approach ya kutazama historia yetu na kujua 'political culture' ya Watanzania. Unatutaka tuchukue fursa inapotokea. Wazo murua kabisa. Lakini capacity ipo wapi? Wapo wap wanaofikiri na kuziona fursa? Wapo wapi watu wanaojenga scenerios na kujiuliza what if?
Tulianza vizuri zoezi la kujenga imani kwa wananchi kupitia Bunge. Tulifanikiwa kupata sizable number ya wabunge wa CCM na kujenga coalition nzuri na kupashana habari. Tukamezwa. Tukajikuta tumewauzia ajenda tukijua kabisa hawatafika nayo mbali.
Ndani ya CCM hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa Rais ajaye kati ya Membe na Lowasa. Hakuna ajenda ya Taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe Mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.
Juzi nilisema hapa JF, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee Sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri - Ignore CCM
Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwamba kutokana na mlolongo wa matukio yanayotokea nyumbani ni wazi kwamba vyama vyetu vya upinzani vingetumia fursa hii kujiimarisha na kijipambanua kwa wananchi kama vyama mbadala mbavyo vinaweza kutufikisha huko tunakotaka kwenda,bahati mbaya kama Zito alivyogusia hii dhana ya SWOT .
In a nutshell,we are passive people and our history backs us up.
Where did cowards of the Nguni people run to?
And where did losers in the Bantu succession disputes flee to?
The skulkers of Bantu leaders' harsh control?
Need I say more?
sasa kama RAIS MTARAJIWA Tanzania ni FREEMAN MBOWE then ujue kuna tatizo Tanzania
sielewi kwa nini CHADEMA hawataki kumpa nafasi ZITTO KABWE
Lakini hiyo nayo ndio demokrasia ya CHADEMA aua UPINZANI
Duh, umetupiga sana. Hata hivyo unfairly. Unapoangalia makosa ya kambi ya upinzani ni vema uangalie 'factors' za ndani na za nje. Katika SWOT analysis hizi ni fursa na vitisho. Hapo utaweza kutoa hukumu sahihi kabisa.
Vilevile ni muhimu sana kuangalia historia ya vyama hivi katika muktadha wa historia ya Tanzania na utamaduni wa kisiasa wa Watanzania. Vyama katika nyakati tofauti - kuanzia kina Marando na Bagenda, Mtei na Makani, Fundikira na Kasanga Tumbo na Mapalala na Seif walipoamua kujitoa mhanga na kuanzisha vyama - kumekuwa na hatu kadhaa zimepigwa katika kujenga dmeokrasia ya kweli katika nchi yetu.
Watu wanaiweka Tanzania katika mizania ya nchi nyingine jambo ambalo ni kosa kubwa maana Tanzania inapaswa kupimwa kutokana na historia yake. Zoezi la ujenzi wa Taifa na kuwa na Taifa moja chini ya uongozi mahiri wa Mwalimu lilifanywa katika misingi ya udikteta mkubwa sana na chini ya amri moja ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tanzania ikajenga jamii ya watu wanaoheshimu mamlaka bila kuhoji na hata vyama vingi vilipoanzishwa vilionekana ni vya wasaliti. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa ambaye alikonga nyoyo za Watanzania na kuaminiwa - Augustino Lyatonga Mrema - lakini naye akavurugwa sana na dola, kuitwa pandikizi na kuondoa kabisa credibility yake katika jamii. Jamii imefanywa kuamini kuwa Mrema ni 'kichaa' na hana sifa ya uongozi. Hii ni kazi iliyopangwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba leo ni watanzania wachache sana ambao wanakumbuka sacrifice ya Mrema katika ujenzi wa demokrasia nchini.
Tusipojifunza na kuelewa historia hii ya vuguvugu la demokrasia Tanzania tutaishia kulaumu watu kila kukicha bila kwenda mbele. CCM itaendelea kutawala na kila baada ya miaka mitano kutakuwa kinatokea chama kina nguvu na baadae kuangushwa, wabunge wenye nguvu na baadae kuangushwa na hata wanasiasa wenye mvuto na baadae kupakwa matope na kunuka.
Demokrasia hulindwa. Viongozi hulindwa zaidi ili kubakia kama alama ya harakati. Raila Odinga aliongoza harakati za mapinduzi Kenya mwaka 1982, akaswekwa lupango kwa miaka zaidi ya tisa na kuishi uhamishoni nchini Norway kwa miaka mingi. Akajiunga na chama cha baba yake mwaka 1992 FORD, kikavunjika na kuwa na FORD-K na FORD-A. Baba yake Mzee Jaramogi alipokufa Raila akataka kunyakua uongozi wa chama, akashindwa na Michael Kijana Wamalwa na Raila akaenda kuanzisha chama chake NDP. Akaivunja NDP na kuingia KANU kuwa Katibu Mkuu na akaipasua KANU vipande 2 na kuanzisha LDP. Akaingiza LDP katika muungano wa NARC na kumpa Kibaki Urais (literally alimpa Urais maana Kibaki alikuwa armchair leader of opposition). Akatoka NARC na kuanzisha ODM-K, akagombana na Kalonzo na kuanzisha ODM na leo ni Waziri Mkuu mwenye nguvu Kenya.
Mchakato wote huu Raila alionekana msaliti, mpenda vyeo na mtu wa vita. Lakini leo huna tena KANU na Raila alipata kuniambia, demokrasia Afrika itaimarika tu iwapo vyama vilivyoleta uhuru vitapasukapasuka na kuondoa ile claim yao ya sisi tulileta uhuru - hii ni claim ya CCM na hata kumkumbatia Mwalimu kama wao.
Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
Mwanakijiji utaandika mpaka utachoka na kutulaumu mpaka utakasirika. Demokrasia ya Tanzania itajengwa kwa sober approach ya kutazama historia yetu na kujua 'political culture' ya Watanzania. Unatutaka tuchukue fursa inapotokea. Wazo murua kabisa. Lakini capacity ipo wapi? Wapo wap wanaofikiri na kuziona fursa? Wapo wapi watu wanaojenga scenerios na kujiuliza what if?
Tulianza vizuri zoezi la kujenga imani kwa wananchi kupitia Bunge. Tulifanikiwa kupata sizable number ya wabunge wa CCM na kujenga coalition nzuri na kupashana habari. Tukamezwa. Tukajikuta tumewauzia ajenda tukijua kabisa hawatafika nayo mbali.
Ndani ya CCM hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa Rais ajaye kati ya Membe na Lowasa. Hakuna ajenda ya Taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe Mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.
Juzi nilisema hapa JF, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee Sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri - Ignore CCM
Mfano wa akina Raila kwa Tanzania hauwezekani. Alijaribu Mrema kuutumia akashindwa. Na sio mfano mzuri wa kuigwa. Ni bora twende Ghana tuone wapinzani kule wanafanyaje mambo yao
Mara nyngi natatizwa sana na dhana hii sijui kwa kiswahili niiteje lakini kwa kiingereza ni "Copy and Paste". Hili naona nitatizo letu kubwa Tanzania na hatupendi ku-originate vitu vyetu wenyewe ili viweze ku match na particularities zetu. Hapa utaona watu wana sema "Raila wa Tanzania", Tuende Ghana tukajifunze and so on.
Nionavyo mimi bila kukubali responsibility yetu watanzania kama individuals tusitegemee kubadilika karibuni. Mabadiliko yeyote kutokea nijambo gumu sana na somebody has to pay a price for it, for old is always Gold na watu wanahofu fulani ya kubadilika ni normal kwa every humanbeing. Sasa hata CCm wangekuwa malaika hawawezi kukubali kubadilika kirahisi lazima kuwe na driving force to that change. The question is who is to lead and be a driving force for that change? Mchezo ninao ona ni kila mtu anafikiria somebody will sacrifice for and agree to lead to bring that change ndo maana utaona macho yetu yana kimbilia kwa wale ambao angalau wanaonyesha kuwa na mwelekeo wa ku lead the change.
Mwanakijiji juzi juzi hapa was talking about the "Meshack, Abednego and Shadrack" of Tz. And that is the problem maana ukiangalia hao hapo juu hawaku fanya reference kwa kitu chochote isipokua imani yao na hawaku copy kutoka kwa mtu yeyote bali walisimamia walichokiamini regardless of the outcome.
Sasa either of the two is possible for our situation either change iletwe kwa lazima na mazingira na hapo ndo huwa inatokea kama explosion kwasababu vitu vinakuwa out of hand haviwezekaniki tena na watu wanasema enough is enough nakama kesi na iwe....Jambo ambalo si zuri sana
ama
Watu wenye maono wajitolee kuwa hao watatu hapo ili waweze ku risk for majority na hapo kuna wawili watatu ku-pay price kama Mheshimiwa Mrema lakini wakipata mass support reward inakuwa kwa every body.
Maoni kwa vijana wa Taifa hili tuunge jitihada zetu na kusaidia kuleta programmed change. Hii mambo yakuacha vitu viende kwa gravity vita cost wengi na kuvirudisha kwenye normal state inaweza ikawa kitendawili. Itakuwaje hivi? Ni kwa kila moja wetu kukataa kutumiwa kwa faida binafsi na kukubali realities njaa ya siku moja isitukoseshe urithi wa miaka yote kwetu na vizazi vyetu. Tuungane na wale wanaoonekana kukataa faida binafsi na wote tutajikuta sehemu moja bila kuambiwa kwani kila mwanadamu ana utashi tofauti ni uvumilivu wa kukaa na njaa.
Sha'abash! Kijembe hiki hakitoshi kwa CCM pekee, hali kadhalika kiende kwa Chadema, TLP, UDP na vyama vingine vyote vyenye umangimeza...Ignore CCM
Zitto,
""Tatizo la upinzani ni kuiga mambo mengi kama wanavyofanya CCM""
Na muunga mkono mshika dau "Engineer wa Kyela"kuhusu hilo hasa kushindwa kwa vyama vya upinzani kujitofautisha na CCM kwenye maamuzi yao,wao na CCM kama uchumi tungewaita "homegenious products"!
Uchaguzi na maamuzi ya CCM kila siku huwa ya kiimla kama ambavyo uamuzi wa wazee wa CHADEMA walipoibaka demokrasia ili kumpa ushindi wa chee mwenyekiti mteule Mbowe dhidi ya mgombea Zitto Kabwe;au maamuzi ya kukera ya watu wachache ndani ya CUF kupingana na sauti ya UMMA dhidi ya kumtambua Rais Karume kwa gharama chee ya kupewa nyadhifa ndani ya serikali kwa baadhi ya vigogo wa CUF!
Kama alivyosema M.K na wengine waliotangulia,vyama vyetu vya upinzani lzm wawe sera tofauti na hizi za CCM,then wasiwe rahisi kukubali kutekwa na hila za CCM kama ambavyo CUF kila mwaka wanapodanganywa na kwa kuhaidiwa serikali hewa ya mseto znz!