security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
MAKOSA YA MAALIM
(Na Dkt.Muhammed Seif Khatib)
Kosa ni kushindwa kupata kitu au jambo litakiwalo. Kosa huwa pia kuvunja sharia, kanuni au dasturi jamii iliyojiwekea. Kwa waumini wa dini kwenda kinyume na makatazo yake.
Duniani mamlaka huweka adhabu kwa wakosaji. Maisha baada ya kifo, imani zinaelekezwa kuadhibiwa kwa watendao dhambi duniani. Kosa kwa mkosaji hana salama. Kosa huweza kuwa halina adhabu lakini kule kutofanikiwa kwa jambo wenye hamu nalo adhabu hiyo nayo si ndiyo. Wakati mwingine kosa la mmoja huwaadhibu wengi.
Maalim au wengine huita mwalimu ni anayefundisha kwa kutoa taaluma. Hafikiriwi wala hatarajiwi kuwa naye atatenda makosa. Imani imejengeka kuwa kila maalim anajua baya na zuri. Hatendi kosa kwa sababu ya uelewa na uweledi wake. Maalim ni ruwaza njema ya kufatwa.
Utamaduni huo ndiyo unaowapa heshima kila mtu aitwaye “Maalim”. Huko Zanzibar wanaye Maalim. Mwanasisa aliyewahi kufundisha katika Skuli ya Lumumba miaka ya sabini. Ingawa hakuwahi kusomae aualimu lakini alisomesha na hadi sasa jina limemselelea na wengine kudhania kuwa ndiyo jina lake halisi.Tamaa na hamu ya kutaka kuingia Ikulu imemtawala sana.
Alijaribu kwa kuchuana na Mzee Wakili ndani ya chama. Ingawa kiumri yeye na Wakili ni mtu na mwanawe. Busara ilikataa kumzindua kumwachia mzee wake. Kokosa nafasi ya kuteuliwa Maalim akala njama kuhakikisha Wakili hapati kura za kushinda. Ni mwanzo wa mpasuko kati ya Pemba na Unguja hadi leo. Mbegu ikapandikizwa kwa baadhi ya watu. Kumifunza wapemba kwamba yeye hakupitishwa kwa sababu ya Upemba wake.
Jeraha la Upemba na Unguja bado libichi. Hili lilikuwa kosa la alfajiri ya safari yake ya siasa. Wakili alimteua kuwa Waziri Kiongozi ili kutibu huo mpasuko. Hata hivyo, alimfanyia njama mzee Wakili akaamua kumtimua. Hili nalo kosa.
Mwalimu Nyerere akamchukua katika chama na kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa NEC. Ndani ya chama akaanzisha vuguvugu chini kwa chini la kuupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pia kuendeleza mpasuko wa Upemba na Unguja.
Mwalimu Nyerere aliyekuwa kipenzi cha Maalima kakasirika na akaongoza katika kumtimua. Hili kosa jengine ndani ya chama limemugharimu. Mwaka 1995 vyama vingi vikazaliwa.
Maalim na Mapalala, maadui pacha wa Mwalimu Nyerere, wakaunda chama. Ndoa haikudumu ya mahasimu wa mwalimu hawa wawili. Mapalala akatimuliwa kwa maelekezo ya masahibu wa Maalim huko nje.
Kwa vile dhamira yake ni Urais wa Zanzibar kuachana na Mapalala si jambo la kumsumbua. Kama hoja ni kuwa ya Wanyamwezi tumbo na wapo tele bara? Hili nalo kosa. Uchaguzi ukakaribia, akaunda chama cha siasa na kukipa jina la “Chama cha Wananchi”. Jina hili kwa Kiarabu ni “Hizbuel Watan” au kwa Kimombo “Nationalist Party”. Kwa siasa za Zanzibar majina haya yanabeba dhana ya chama kilichopinduliwa na Afro-Shirazi Party kilichokuwa kinashabikiwa na Sultan Jamshid aliyepinduliwa mwaka 1964.
Kama vile hilo halitoshi Maalim na wenzake wakahubiri kuwa wakingia Ikulu, mali zote zilizotaifishwa yakiwemo majumba na Mashamba watapewa wenyewe. Chama hiki kikaungwa mkono na wakimbizi wa Mapinduzi ya Zanzibar, sehemu kubwa ya Pemba na maeneo ya Unguja ambao kabla ya Mapinduzi yalishabikiwa na chama cha Hizbu. Mwelekeo huu ukaibua hisia kali za Afro-Shirazi na kulinda “Mapinduzi” kwa wafuasi wa Chama cha Mapinduzi.
Pia ya hoja kwamba tokea mwaka 1964 hadi 2010 Zanzibar Marais wake wanatoka Unguja, Maalim akaivalia njuga ili aonewe huruma. Vipindi vitatu vya miaka kumi na tano akashindana na Salmin na Amani Karume, Maalim hakufanikiwa sera yake Upemba na kuyabeza Mapinduzi. Hili kosa jengine la Maalim.
Mwaka 2010 mgombea kupitia CCM kwa mara ya kwanza akatoka Pemba na akawa Mpemba halisi. Hoja ya ukame wa wagombea wa Urais kutoka Pemba ikafa. Hoja nyingine zikaendelea. Mwaka wa jana Maalim akafanya makosa mengi zaidi.
Hoja ya UKAWA ikamtafuna. Yeye Maalim ni mbinafsi sana. Ukinyemelea masilahi yake ya uongozi na Urais wa Zanzibar, atakuandama. Mnakumbuka alipogombanana Prof Safari na Hamad Rashid walipotaka nafasi yake. Wote walitimuliwa.
Yeye madhali UKAWA hautagusa Urais wa Zanzibar hatagombana na mtu. Kwa kujithamini yeye tu akamtelekeza sahiba wake wa karibu Prof Lipumba katika Urais Muungano na kumthamini Lowassa agombee Urais wa Muungano. Lipumba akawa muhanga kama Mapalala, Hamad Rashid, Prof. Safari, Juma Othman, Fatuma Maghimbi na wengine kama hao.
Hili kosa la kusababisha kukimbiwa na Mwenyekiti wake na mwandani wake. Kosa jengine ni lile la kupanga uhalifu wa kuiba kura zaidi ya laki mbili katika mazingira ya uchaguzi wa Zanzibar wenyewe ushindani. Tokea mfumo wa vyama vingi ushindi unakuwa wa elifu chache.
Sina haja kuelezea mbinu chafu tokea CCM kunyimwa mawakala, vituo bubu kuwepo, wapiga kura kupigwa Pemba, matokeo ya vituo kuletwa asubuhi ya siku ya pili ya uchaguzi na sehemu nyingi matokeo yanaonesha watu wote wamepiga kura hapana aloumwa au kufa. Na kila kituo kura zake Maalim akaongoza CCM yafatia na hakuna vyama vyengine.
Makosa ya kwanza kujitangazia yeye mwenyewe ushindi Maalim. Hili kosa lilitosha kumtia hatiani. Kosa la pili, kuita waandishi wa habari na kumpa Rais Shein amri ya mwisho “altimetum” ya saa 48 hapo tarehe 02.02.16 awe amehama Ikulu. Endapo asipofanya hivyo nguvu za umma itatumika. Muda umefika Rais Shein hakuondoka Ikulu na nguvu za umma hazikuonekana.
Kosa jengine la Kuwataka mawaziri wa Chama chake wasiende kazini kwani muda wa serekali umekwisha. Yeye anaendelea kwenda kazini, kuwa Makamo wa Rais, analindwa, analishwa, analipwa na kuhudumiwa matibabu ya India, Hindu mandal, na huduma sasa za hotel ya kitalii.Yeye kubaki na uluwa, madaraka na mamlaka sawa. Kosa jengine la kuweka siku ya kuuapishwa yeye. Amewapa watu tamaa na matumaini. Siku haikufika hadi sasa.
Ili Rais kuapishwa lazima uwepo uchaguzi wa halali na huru. Lazima mgombea ashinde, atangazwe na Tume na hatimaye aapishwe na Jaji Mkuu wa Zanzibar. Maalim hawezi kuwa Rais bila kufata utaratibu huu.
Kosa linalofata ni kutaka mazungumzo kabla kufika mwisho kukimbia meza ya mazungumzo. Kutoa siri ya mazungumzo hadharani kinyume na makubaliano. Huku ni kuwadharau viongozi wenzake walioombwa kuwepo katika meza ya mazungumzo. Kosa kubwa kuliko yote aliyoyafanya katika siasa ni kuwazuia wenzake wawakilishi wasigombee kwa sababu yeye hakushinda.
Kuwakataza wafuasi wake wasipige kura kuchagua watu wawapendao. Hii ni dhambi kubwa ya kisasa itakayomuuandama katika maisha yake yote. Historia itamuhukumu Maalim.
Watani”