Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,243
- 44,524
Na mwanaume je?Ukipata mwanamke asie samehe
utajuta kumfaham......
Na mwanaume je?
Katika mapenzi watu hukoseana na wakati mwingine hata kuchukizana na kukasirikiana. Na kuna wakati makosa hayo huzaa hadi vurugu na hata kusababisha matumizi ya nguvu (violence) na katika matukio mengine makosa hayo hufikia kukatishia maisha.
Makosa yapo mengi kuanzia madogomadogo kama mtu kuwa msahaulifu, kufanya kitu ambacho kinasababisha usumbufu n.k na yapo makosa makubwa kama kwenda nje ya mahusiano na kuzaa nje ya ndoa..
Makosa hayo yote huita mwitikio kwa pande zote mbili, kuna mwitikio wa uchungu, kisasi, hasira, wivu na hata kinyongo cha muda mrefu. Na wakati mwingine haya yote yanadumu siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi na hata miaka. Hivyo makosa haya ya mapenzi yanaweza kusababisha madhara ya kihisia, kisaikolojia na hata kimaumbile kwa yule ambaye amakutwa nayo.
Na kutokana na hayo kuna mambo ambayo watu hufikia mahali na kusema kuwa makosa fulani hayasameheki na kuwa mtu wake akifanya kosa x basi hawezi kumsamehe kamwe..
(itaendelea)...
Pamoja na ugumu wa kusamehe, ili tuishi maisha yasiyo na presha, ni lazima tujifunze kusamehe. Hakuna jinsi maana sisi kama binadamu hatuwezi kuacha kukosa. Imagine, itabidi uamue kusihi na malaika kama hutataka kusameheWapendwa mimi nadhani mwanaume siku zote ndio huwa mgumu sana kusamehe, yaani anaumia rohoni na kutamani hata kutoa roho ya mtu, Mimi nafahamu wanandoa fulani kabla ya kuoana past ya mwanamke ilikuwa chafu kidogo, lakini hakumwambia mwenzie pengine kwa kuhofoa kutemwa labda kwakuwa alimpenda sana, lakini hadi wasiochelewa na wenye visa na mkewe wakaanza kumsemea kwa mumewe, mume hadi leo hajasamehe kwa kile anachokiita ati mkewe hakuwa mkweli kwake, na tayari wana miaka minne ya ndoa yao kwa sasa na watoto. Lakini mwanamke kuna wakati aligundua uhusiano wa mumewe na msichana wa zamani kabla ya wao kuwa kitu kimoja, mume aliomba kusamehewa na alisamehewa, ingawa si kwa urahisi lakini ALISAMEHEWA, lakini hiki cha sasa cha huyu bibie,.. mume anashindwa kusamehe, ndoa imekuwa ndoano, sijui wataishia wapi. Point yangu ni kuwa mwanaume siku zote ni mgumu sana katika kusamehe!
Na mwanaume je?
Pamoja na ugumu wa kusamehe, ili tuishi maisha yasiyo na presha, ni lazima tujifunze kusamehe. Hakuna jinsi maana sisi kama binadamu hatuwezi kuacha kukosa. Imagine, itabidi uamue kusihi na malaika kama hutataka kusamehe
Mimi nashida na kimaumbile kivipi mtu anaweza kuathirika kimaumbile,unamaanisha kwa kupigwa?Katika mapenzi watu hukoseana na wakati mwingine hata kuchukizana na kukasirikiana. Na kuna wakati makosa hayo huzaa hadi vurugu na hata kusababisha matumizi ya nguvu (violence) na katika matukio mengine makosa hayo hufikia kukatishia maisha.
Makosa yapo mengi kuanzia madogomadogo kama mtu kuwa msahaulifu, kufanya kitu ambacho kinasababisha usumbufu n.k na yapo makosa makubwa kama kwenda nje ya mahusiano na kuzaa nje ya ndoa..
Makosa hayo yote huita mwitikio kwa pande zote mbili, kuna mwitikio wa uchungu, kisasi, hasira, wivu na hata kinyongo cha muda mrefu. Na wakati mwingine haya yote yanadumu siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi na hata miaka. Hivyo makosa haya ya mapenzi yanaweza kusababisha madhara ya kihisia, kisaikolojia na hata kimaumbile kwa yule ambaye amakutwa nayo.
Na kutokana na hayo kuna mambo ambayo watu hufikia mahali na kusema kuwa makosa fulani hayasameheki na kuwa mtu wake akifanya kosa x basi hawezi kumsamehe kamwe..
(itaendelea)...
Mimi nashida na kimaumbile kivipi mtu anaweza kuathirika kimaumbile,unamaanisha kwa kupigwa?
hapana yaani kutokana na kutokusamehe mwili utaanza kuonesha udhaifu na hata magonjwa mbalimbali yanaweza kuukumba. Kwa sababu kuna uhusiano usiotenganishwa kati ya afya ya akili (mental health) na afya ya mwili (physical health)..
Ukipata mwanamke asie samehe
utajuta kumfaham......