Makosa makubwa matatu ya CHADEMA ( Mtizamo wangu)

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,712
5,033
Hakuna shaka kuwa katika historia ya siasa ya vyama vingi nchini hakuna chama cha upinzani kilichowahi kuwa na nguvu kama chadema.

Chadema wameweka historia ya kuwa chama cha upinzani kilichopata wabunge wengi zaidi pamoja kuungwa mkono na kundi kubwa sana la watu hasa vijana na wasomi mbalimbali.

Tangia 2015 trend ya Chadema ilibadilika , ile kasi ya ushawishi wake ikaanza kushuka, Chadema imepoteza ushawishi sehemu ambazo ilikuwa imezikamata kama vyuoni, mitandaoni na hata mtaani hasa kwa vijana, yafuatayo ni maoni yangu ya kwanini Chadema imepoteza umaruufu na ushawishi tofauti na miaka 6 iliyopita.


1. Lowassa

Viongozi wa chadema na mashabiki wa chadema ukiwauliza wanakwambia Lowassa aliwasaidia sana katika uchaguzi mkuu 2015, wanasahau kuwa Lowassa aliwapa faida za muda mfupi na kuwaachia athari za muda mrefu. Hivi sasa chama hakiwezi kabisa kuzungumzia agenda ya ufisadi kwa sababu haina tena moral authority ya kuukemea kwa kuwa waliweza kumkaribisha mtu waliomshutumu kwa muda mrefu awe mgombea wao wa Urais.

Ile connection iliyokuwepo kati ya Chadema na vijana maskini waliokuwa wengi imekatika, vijana wengi wanaona Chadema ni watu wa fursa muda wowote wanawabadilikia kama walivyoweza kubadilika na kuanza kumsafisha waliomchafua.

2. Kukosa Plan B

Rais J.P.M baada ya kuchaguliwa kuwa Rais alikuja na style yake utendaji wa kazi na ufanyaji wa siasa ambazo zilikuwa tofauti kabisa na Siasa za enzi ya J.k. Mikutano ilivyopigwa Stop Chadema hawakuwa na alternative zaidi ya kukaa na kulalamika huku CCM ikiendelea kutamba tuu.

Ni kama vile Chadema wanaishi kwenye kivuli cha siasa za enzi ya J.K , bado hawajakubali kabisa kuwa nyakati zimebadilika na wanatakiwa kuwa wabunifu na kuacha tactics zao za zamani maana zimegoma kufanya kazi.

3. Hamama na Matatizo mengine ya Ndani.

Viongozi wengi na mashabiki wa siasa za upinzani huwa wanapenda kubeza wabunge waliohama Chadema na kwenda kwingineko, wanasahau ya kwamba kuna wananchi waliuza mali zao , walipoteza muda wao kuhakikisha ushindi unapatikana kwa hao wabunge wa Upinzani.

Wananchi wengi wamekata tamaa ya kuwapigia kura au kuwapambinia viongozi ambao muda wowote wanawabadilikia na kwenda kwenye vyama vyenye itikadi ya tofauti, wakiuliza wanapewa majibu rahisi kuwa huyo kanunuliwa.

Just imagine unaacha kufanya kazi zako unaenda kumpigia mtu kura halafu baadae unaambiwa kanunuliwa , sasa kama amenunuliwa utakuwa na uhakika gani kwenye uchaguzi wa 2020 utakayempigia hatanunuliwa!!

Mwisho wa siku, ukweli mchungu Chadema ndiyo inaenda kupotea japokuwa siasa za upinzani zitaendelea kuishi kwa watu, maana mawazo kinzani yapo na yataendelea kuwepo.
 
Tunashukuru kwa maoni yako, hata kama yameegemea kwenye matamanio ya CCM.
 
Labda wewe watakujibu bila kukupa furushi la matusi.

MALAIKA WASIO SHAURIKA

Shauri lipo mikononi kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom