Makosa 3 wanayoyafanya wanawake wanapochepuka ambayo hupelekea kukamatwa!

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Copy and pasted

Sio kwamba nawafundisha namna ya kuchepuka, hapana! Lakini huwa naona wanawake wengi wanaochepuka na kufanya makosa haya nawaonea huruma. Nawaonea huruma si kwasababu wanayoyafanya ni mazuri hapana , nawaonea huruma kwani najua muda si muda watakamatwa na kama mnavyojua wanaume sisi kusamehe ni ngumu.

Lengo la makala hii ni kwaajili ya kukuambia kua hauko salama, kwamba kama unachepuka kweli basi ujiweke tayari kuachika, kwamba uwe umeshaichoka ndoa unasema poteli ya mbali. Lakini kama sivyo hembu acha kwani tofauti na wewe ambaye ukimfumania mumeo utamsamehe, yeye akikufumania mbali na kipigo lakini atakuacha na mbaya zidi huo mchepuko nao ukishaachika unakukimbia.

Sasa kama wewe ni mwanamke kabla ya kuchepuka hembu jiulize kwanini unachepuka, najua una sababu zako, wakati mwingine hata huna sababu za msingi. Lakini hapa najua utasoma kimyakimya ila kama unachepuka nina uhakika ushafanya angalau kosa moja kati ya haya matatu. Lakini kama hujafanya hata moja basi wewe ni mzeefu katika kuchepuka.

(1) Wanamuambia Rafiki Wanayemuamini:
Nadhani kuwa kila mmoja wetu ana yule rafiki yake mmoja ambaye anamuamini sana, ambaye ana umbea wake wote yule ambaye kila siku ukishamaliza kuongea unasema “Usimuambie mtu nimekuambia wewe tu kwakua ni mtu wangu wa karibu nakuamini sana…” Ndiyo hata mimi ninaye. Kwa wanawake wanawaamini sana hawa marafiki, tena inawezekana hata wakati unatongozwa, kabla hujamkubalia jamaa ulikimbia na kuomba ushauri kwake.

Kwakua ulishamuambia matatizo yako ya ndoa, akakuambia chepuka upate faraja, lakini kwakua ana hela basi akakuambia nenda mchune tu kimya kimya mumeo hatajua. Inawezekana hata kuenda kukutana na jamaa unaongozana naye na kwamumeo unaaga unaenda kwa huyo rafiki! Nikuambie kitu dada yangu kama umefanya hili kosa basi jua hakuna siri tena. Kuna sababu kuu tatu kwanini rafiki yako huyu atakusaliti na kusema.

Sababu ya kwanza nikuwa inawezekana huyu unayemuona kama rafiki yako wa kumuambia siri zako zote, wewe si rafiki yake wa kumuambia siri zote, hata yeye ana rafiki mwingine ambaye anamuambia “Nimekuambia wewe tu usimuambie mtu mwingine….”. Hapa ndipo tunapokuja sababu ya pili kuwa kama wewe ulishindwa kuficha umbea wako, likakuwasha ukasema unafikiri yeye halitamuwasha na kwakua wewe ndiyo umemuambia basi atatafuta mtu mwingine ambaye naye ana rafiki yake, atamuambia mwingine na mwingine.

Mzunguko unakua mrefuuu. Lakini kuna jambo la tatu, huyo rafiki yako anakuonea wivu. Labda nayeye yuko kwenye mahusiano yanamshumba, hajaolewa au yuko ndoa ya mateso, anaona unavyochezea ndoa yako na anaumia au anatamani aina ya maisha unayoishi hivyo ipo siku mtagombana au hata bila kugombana atasema tu. Akiona watu wanakusifia wanakuona mtakatifu basi atasema huyo anajishaua mbona anamsaliti mume wake, huamini subiri utakuja kuona.

(2) Wanahongwa Na Kujisahau Matumizi;
Kuna wanawake ambao huchepuka kwasababu ya mapenzi, wanataka watu wa kuwakuna tu! Kuna ambao huchepuka kwakua tu ni vicheche na hawawezi kukataa wakitongozwa, lakini kuna wale ambao huchepukia pesa. Sasa hawa wapesa bwana ili pesa iwe na raha nilazima uile, kwamba huwezi kuwa na hamu ya kuku, una hela ya kuku halafu ukaacha kwenda kula ukasikia raha. Hapana hela raha yake itumiwe na matumizi yaonekane.

Sasa wanawake wengi wakiwa na michepuko ambayo huihonga hushindwa kubalance matumizi, yaani kama mwanaume ni mjanja tu kidogo atagundua. Najua mna mbinu zenu, kila siku unasingizia mchezo, unasingizia VICCOBA na kama unafanya kakazi unasema kua nimechukua mkopo, lakini kwa mwanaume mjanja atajua. Umechukua mkopo kweli, ukanunua gari lakini hela ya mafuta, vipi nguo unazoibadilisha kweli ni huo huo mkopo.

Lakini mnajisahau, labda nikupe mfano mteja wangu mmoja yeye aliolewa na mwanaume pesa ya kawaida, na mzee wake akamnunulia gari akajifanya alichukua mkopo kazini na kanunua kwa pesa yake jama aakajifanya fala akakubali. Kwelia kachukua mkopo, lakini kwakua hakuuhitaji kununulia gari basi akauacha tu benki.

Sasa gari inawekwa mafuta na mchepuko siku moja jamaa kaangalia salio la mkewe anakuta ana mamilioni (ndiyo mumeo anajua passwed ya kila kitu chako labda kama hataki kujua), anaulizwa hana hata chakusema, ndiyo akakiri kosa mume kamuacha na mimba yake anafika kwa mchepuko umemuacha kabaki na gari tu.

Sasa wadada mnashindwa kubalance hiki kipengele, kwamba uhongwe na mchepuko lakini uishi maisha yaleyale ya kipato chako, ni ngumu, wengi hujionyesha na kama mumeo si fala fala basi anagundua. Kwani wakati mwingine unawaza kuna haja gani ya kuhongwa kama utaendelea kuishi kimasikini! Hivi ni mchezo gani kila siku wewe ndiyo unapokea, ni VOICCOBA gani wewe tu ndiyo unakopeswa wengine aahhhh!

Lakini hata kama unafanya kazi kweli mumeo si anajua mshahara, unaweka mafuta, uaachangia sherehe, unanunua nguo za gharama, unavaa na gold, kila kiatu chako…daaa mshahara huu huu ambao unajulikana, nywele ni za laki sijui ngapi! Nasema labda kama jamaa na yeye falafala hajiongezi ila ni wiki mbili tu najua kuwa hapa nasaidiwa kulea. So dada yangu hili kosa najua unalifanya sana... utajua mwenyewe!

(3) Wanaanza Dharau Kwa Waume Zao;
Kuna siku nilitoa mfano mmoja nilisema kama umevaa suruali ndani na kigauni juu upepo ukapiga hutahangaika kushikilia kigauni kwakua tayari una kitu cha kukustiri ndani. Lakini kama ndani hujavaa kitu, kigauni kikapigwa na upepo basi utahangaika kujishikilia. Sasa mchukulie mumeo kama kigauni na mchepuko kama suruali.

Mwanamke aliyekua ananyanyekea analalamika anajali baada ya kuchepuka, akakutana na mchepuko ambao labda unatoa hela sana, labda unamvunja vizuri kitandani Ndugu yangu hujisahau na kuanza dharau. Yaani anabadilisha, anaacha kuwa mke wa mumewe anakua mke wa mchepuko, kwamba kipaumbele chake cha kwanza kitakua ni kuhakikisha kua mchepuko unaridhika kisha mume. Ataanza dharau, dharau itaanzia kitandni ambapo hata mume akipiga show vipi, si akili haipo basi hubadilika na hata haonyeshi ushirikiano.

Kila siku hujifanya anaumwa hataki show, yaani kila siku utasikia yuko kwenye siku zake, yaani ulivyo sijui niseme mjinga unamdanganya hata na mumeo uko kwenye siku zako wakati anazijua. Haiishii hapo baada ya mechi ni dharau tupu, si anakunwa shemu. Sasa kwenye matumizi ndiyo shida, akimuomba mume pesa kasema huna ndiyo hukasirika, haombi mara mbili, anaenda kwa mchepuko anapewa, sasa mume atastuka kashanunua kitu flani. Akibanwa ndiyo vikoba, Mama kanipa, nimekopa kwa mtu flani. Kirahisi tu mwanaume mjanja anastuka na kujua huyu kuna mzee anamalizia pensheni yake.

Mke anaanza kufanya mamauzi yake ya pesa hamshirikishi mume, utakuta mke kanunua gari bila hata mume kujua, kiwanja bila mume kujua, hapa sisemi wote wanaofanya hivyo wanachepuka hapana, ila wanaochepuka hufanya hivyo kwa dharau. Kwamba mume kamuambia tuache gari tununue kiwanja yeye anasema anataka gari kwani kashaahidiwa na mchepuko hivyo akiacha bahati inayeyuka. Kwa dharau kabisa ananunua bila kumshirikisha mume.

Kuna mambo mengi ambyao mnayafanya ambayo kama mwanaume akichunguza tu kidogo basi anakugundua. Sasa hapa akili ni zako, sitaki nikufundishe namna ya kuchepuka lakini nikuambie tu kuwa, hembu kua makini, mimi nawaonea huruma hao watoto kwani jamaa akikufumania atakuacha. Kusamehe ngumu aisee ni wanaume wachache wenye huo ujasiri wa kufumania wake zao na kuwasamehe, mimi sina aisee sijafikia daraja hilo la juu kabisa la uanaume.

Ni kweli una hongwa, labda unafikishwa kileleni na una furaha ukiwa na mchepuko, lakini je umejiandaa kuachika. Ni muhimu kabla ya kuchepuka ujiandae na kuachika kwani siku ukifumaniwa wote hukuacha, mume na mke.
 
Mwanamke akichepuka anajiamini aisehhh kama CCM kwenye kampeni.

Nilipokuwa chuo jamaa angu mmoja alichepuka na mke wa mtu kilichotokea yule mke aliamia room chuoni mpaka jamaa angu akatafutwa ikabidi aache na chuo.

jingine ni swala la kukojozwa ukipatia hapo utapendwa sana na wanawake
 
Kuna siku nilimuona mtu anahangaika kutaka suluhu baada ya kuugundua mchepuko wa mkewe akaudunda. Mkewe alipoambiwa na mchepuko akakasirika na kuondoka nyumbani na watoto. Literally Mwanaume anatafuta pa kuombea msamaha ili Mkewe arudi.

Nina mpango wa kum'bipu Paw nijue ananipenda Sana ama kiduchu.
Mwanamke akichepuka hasamehewi...shauri yenu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilimuona mtu anahangaika kutaka suluhu baada ya kuugundua mchepuko wa mkewe akaudunda. Mkewe alipoambiwa na mchepuko akakasirika na kuondoka nyumbani na watoto. Literally Mwanaume anatafuta pa kuombea msamaha ili Mkewe arudi.

Nina mpango wa kum'bipu Paw nijue ananipenda Sana ama kiduchu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Nitamsamehe mwanamke makosa mengine yote lakini sio issue ya kuchepuka...nkijua hata kama ana flirt na mtu huwa anaenda na maji
 
Siamini Kila mwanamke mchepukaji anatafuta kukojozwa. Wengine wanatafuta tu emotional cushioning. Awe na mtu tu wa kumsikiliza iwapo huko nyumbani hakuna maongezi tena.

Asilimia kubwa ya wanawake walioolewa wanaochepuka wanatafuta ambacho hawapati nyumbani ( Mara nyingi sio sex wala pesa)
Mwanamke akichepuka anajiamini aisehhh kama CCM kwenye kampeni.

Nilipokuwa chuo jamaa angu mmoja alichepuka na mke wa mtu kilichotokea yule mke aliamia room chuoni mpaka jamaa angu akatafutwa ikabidi aache na chuo.

jingine ni swala la kukojozwa ukipatia hapo utapendwa sana na wanawake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa Mwanaume, ningemsamehe Mke anaechepuka baada ya kujadili kwa kina sababu za yeye kufanya hivyo. Ofcoz ningemuuliza pia kama bado anataka kuendelea na ndoa (nami naamini mwanamke akiamua kuchepuka ujue hakutaki kabisa anakupigia hesabu za kukuacha). Tofauti na mwanaume, ambaye kiuhalisia hahitaji sababu za kutosha kuchepuka, naamini mwanamke anachepuka kwa sababu ambazo ukiangalia kiumakini hata uewe unazijua ila ulizichukulia poa tu
Mwanamke anayefikia kuchepuka wacha aende huko alipoona panafaa...ukisamehe uchepukaji jua umesharuhusu aendelee


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa Mwanaume, ningemsamehe Mke anaechepuka baada ya kujadili kwa kina sababu za yeye kufanya hivyo. Ofcoz ningemuuliza pia kama bado anataka kuendelea na ndoa (nami naamini mwanamke akiamua kuchepuka ujue hakutaki kabisa anakupigia hesabu za kukuacha). Tofauti na mwanaume, ambaye kiuhalisia hahitaji sababu za kutosha kuchepuka, naamini mwanamke anachepuka kwa sababu ambazo ukiangalia kiumakini hata uewe unazijua ila ulizichukulia poa tu



Sent using Jamii Forums mobile app
unamuacha mwenza kisa kagegedwa na mtu mwingine kwani kuna shida gani?
 
Ningekuwa Mwanaume, ningemsamehe Mke anaechepuka baada ya kujadili kwa kina sababu za yeye kufanya hivyo. Ofcoz ningemuuliza pia kama bado anataka kuendelea na ndoa (nami naamini mwanamke akiamua kuchepuka ujue hakutaki kabisa anakupigia hesabu za kukuacha). Tofauti na mwanaume, ambaye kiuhalisia hahitaji sababu za kutosha kuchepuka, naamini mwanamke anachepuka kwa sababu ambazo ukiangalia kiumakini hata uewe unazijua ila ulizichukulia poa tu



Sent using Jamii Forums mobile app

Deception is the biggest felon
 
Back
Top Bottom