Ketoka
JF-Expert Member
- Sep 23, 2015
- 1,121
- 1,983
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imesema kama makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, hayatapata wateja kama ilivyotokea katika minada miwili ya mwanzo, wanaweza kuchukua uamuzi wa ama kuyateketeza au kuyagawa. Mkurugenzi wa Huduma na E limu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo alilieza HabariLeo jana kwamba japokuwa mnada wa makontena hayo haujawekewa kikomo, lakini kama yatakosa wateja, ndipo maamuzi ya ama kuyateketeza au kuyagawa yatakapofanyika.
Kayombo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili kutaka ufafanuzi wa kauli iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere na kunukuliwa kwenye moja ya magazeti ya kila siku jana kuwa wanasubiri mnada wa tatu, utakaofanyika mwishoni mwa wiki ili waweze kufanya uamuzi. Alipoulizwa ni taasisi zipi zitanufaika na mgawo wa makontena hayo kama hayatapata wateja, Kayombo alisema hilo litajulikana wakati utakapofika. Alieleza kuwa kama bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo zitaonekana hazifai tena kwa matumizi ya binadamu, ndipo zitakapoteketezwa.
Jumamosi iliyopita, TRA kupitia Kampuni ya Udalali ya Yono, iliendesha mnada wa kuyauza makontena 20 yaliyopo Bandari ya Dar es Salaam, yaliyoletwa nchini na Makonda. Katika mnada huo, makontena hayo hayakununuliwa kutokana na wateja waliojitokeza kushindwa kumudu bei iliyotangazwa. Katika minada iliyotangulia, Kampuni ya Udalali ya Yono ilikuwa ikilinadi kila kontena moja kwa Sh milioni 6 0 , huku kikomo cha bei walichofikia wateja waliojitokeza kikiwa ni Sh milioni 30 . Kupigwa mnada kwa makontena hayo, kunatokana na agizo la Waziri wa F edha na Mipango, Dk Philip Mpango, kutembelea bandarini hapo hivi karibuni na kuiagiza TRA kuyapiga mnada kama Mkuu wa Mkoa huyo atashindwa kuyalipia kodi stahiki ya serikali.