barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Anaandika Mhe Dr. Milton Mahanga
Nimesoma kwenye gazeti moja leo kwamba Serikali Kuu inaweza kuzichukua na kuzitumia zile shs. bilioni 5.8 za UDA zilizokataliwa na mwenye hisa (Jiji la Dar es Salaam). Wala sibishi kwamba hilo haliwezekani kwa kuwa utawala wa kisheria una walakini katika enzi hizi hapa nchini.
Lakini kama utawala wa kisheria utafuatwa, kinachotakiwa kufanywa kabla ya Serikali Kuu kuchukua fedha hizo ni kuanzisha kwanza mchakato wa kuhamisha hisa zilizokuwa Jiji kwenye Shirika la UDA na kuzihamishia Serikali Kuu. Baada ya hapo Serikali Kuu sasa ndiyo iuze hisa hizo za UDA kwa Simon Group
Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 145 na 146, ikisomwa pamoja na Sheria zilizoanzisha Serikali za Mitaa, Sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982, Serikali za Mitaa zina mamlaka kamili ya kuamua kuhusu mali na rasilimali zake. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeamua kusitisha uuzaji wa hisa zake asilimia 51 kwenye UDA kwenda kwa Simon Group.
NB:Makongoro Mahanga amekuwa muibuaji wa mijadala ya Kikatiba inayoonekana kukiukwa na Serikali ya awamu ya tano.Mjadala wa uteuzi wa Wabunge wanaotokana na nafasi za Rais uliibuliwa na Makongoro Mahanga.
Mjadala huo ulisababisha Mh.Rais kufanya mabadiliko ya "ghafla" ya uteuzi wake kwa kumtoa Dr Possi na kumuweka Anna Kilango Malecela.
Na pia ibaki ktk kumbukumbu kuwa wakati wa uuzwaji huu wa "kisanii" wa UDA,Dr Milton Makongoro Mahanga alikuwa Naibu Waziri na Mbunge wa Jimbo la Segerea ambapo kwa mujibu wa taratibu anakuwa sehemu ya baraza la Madiwani Dsm.
Lakini Marehemu Didas Masaburi ambaye nyaraka nyingi za uuzwaji wa UDA zimemtaja,ni ndugu wa Dr Mahanga.Ukiwa ndani ya mfumo kijani nyeusi huwa na mchangayiko wa blue na kijani,lakini nje ya mfumo....NYEUSI NI NYEUSI KWA MAANA YA NAMNA INAVYOONEKANA