Makongoro Mahanga na Kabaka wakimbia kikao cha Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
227
Ndiyo wakuu! Habari zilizo nifikia muda huu ni kuwa mawaziri Mahanga na Kabaka wamelala mitini i.e. hawajatokea kwenye kikao cha kamati ya bunge ya huduma za jamii kilichokuwa kimepangwa kuanza leo jijini Dares salaam. Lengo la kikao hiki ni mwendelezo wa mjadala mpana kuhusu mafao ya wafanyakazi ndani ya mifuko ya hifadhi za kijamii.

Ikumbwe kabisa kuwa ni bunge hili la serikali legelege na dhaifu lili ipitisha sheria hii mwezi April,mwaka huu ambapo inatakiwa mfanyakazi atimize umri wa miaka 60 ndo apate mafao yake. Naomba nisi eleze sana kwani suala hili si jipya masikioni na machoni mwa watanzania.

Kwa mjibu wa taarifa ni kuwa wadau walio hudhuria ni wengi sana kutoka mifuko mbalimbali ya jamii pamoja na wawakilishi wa wafanyakazi wa migodini kutoka mikoani ambao ndio wahanga wakubwa wa sheria hii kandamizi. Katika hali ya kushangaza ,Mbunge Komba ndiye anaesumbua wajumbe wa kikao hicho kama mpiga debe upande wa serikali.

Kama hali ita endelea hivi, baadae wadau watafanya Press conference kutoa dukuduku zao. Naomba kuwasilisha. Source. Mmoja wa wadau ndani ya kikao.
 
Ndiyo wakuu! Habari zilizo nifikia muda huu ni kuwa mawaziri Mahanga na Kabaka wamelala mitini i.e. hawajatokea kwenye kikao cha kamati ya bunge ya huduma za jamii kilichokuwa kimepangwa kuanza leo jijini Dares salaam. Lengo la kikao hiki ni mwendelezo wa mjadala mpana kuhusu mafao ya wafanyakazi ndani ya mifuko ya hifadhi za kijamii.....

Kama sheria haisemi lazima Waziri ndo ahudhurie kikao hicho na serikali imepeleka mwakilishi nadhani hakuna tatizo.
 
Wakikimbia vikao vyenye maslahi kwa wananchi, basi wakatafute wananchi wa kuwaongoza. Moja ya athari za sheria kandamizi ni kupelekea nchi kutotawalika. Kama nchi haitawaliki wao watakuwa mawaziri wa nani?
 
Wakikimbia vikao vyenye maslahi kwa wananchi, basi wakatafute wananchi wa kuwaongoza. Moja ya athari za sheria kandamizi ni kupelekea nchi kutotawalika. Kama nchi haitawaliki wao watakuwa mawaziri wa nani?

uchaguzi ukifika kanga, vitenge, pilao, viroba, pombe za kienyeji na buku buku, bila kusahau kofia na t-shirt nani anakumbuka mafao ya wafanyakazi au maishi duni?? heri umaskini wa mali kuliko umaskini wa akili!
 
sasa sheria wamezitunga wenyewe....alafu wanamkimbia..si wajitokeze waielezee jamii kwanini wamefanya walichoamua kufanya na waliopo hapo nao wato yaliyopo moyoni mwao...lakini hakuna kitu kinachonishangaza kwenye hii serikali anymore
 
Wewe subiri wacheze na hazina za watu,hawajui imesemwa kwamba hazina yako ilipo ndipo na roho yako ilipo? That means wanataka kutuua hawa!!
 
Watuambie kama vipi tuingie barabarani tukadai vyetu, kwanza life expectancy imepungua sana
 
UP TO DATE:

Baada ya mvutano mkubwa sana na wa muda mrefu kwa hoja toka upande wa wadau mifuko ya hifadhi za jamii, Mbunge Sugu wa CHADEMA aliiomba kamati na wawakilishi wa serikali wasikilize hoja za wadau.

Hatimaye wakapata nafasi na muda wa kuwasilisha hoja zao za msingi ambazo ki msingi ni nzito na ni vilio vya wafanyakazi wa sekta binafsi juu ya fao la kujitoa.

Wadau wamefika mbali zaidi na kutoa tamko kuwa hawataki uzushi /usanii na propaganda juu ya hatima ya maisha yao. Naomba kumshukuru Rais JK kwa kuwafikisha hapa watanzania kwani Mwl Nyerere alipata kusema "Ipo siku binadamu atachagua kifo kuliko fedheha."

SOURCE: ROGERZ MWANA WA LUHEGA, Mbunge kivuli geita kama mdau kwenye kikao.
 
Alafu huyu Naibu Waziri Makongoro nilimuona kwenye Ukumbi wa Blantyre-Mtwara tar 19 wakati Jahazi Moden Taarab wanatumbuiza.Kumbe issue za maana anakwepa ila kwenye mambo ya ajabu ajabu kama haya anahudhuria.Inakera .
 
Mahanga lazima akimbie coz sio mwakilishi wawananchi ila ni mwakilishi wa baba Mwanaasha.
ndiye aliyemsaidia kuchakachua na hata aliposhitakiwa ndiye aliyegeuka wa kumwamlisha
Jaji Juma ili afanye kila analoweza kumbeba huyo kilaza Mahanga.
 
Wadau waliojivinjari italian house Tabata embu mtujuze,week end hii hakuwepo pale?labda ana hang over ataanza kazi jumanne....tehe!!!
 
Inabidi wapewe wito wa kufika wasijifanye mbuni kuficha kichwa kwenye mchanga wakati makalio yapo wazi
 
Huyu Makongoro Mahanga anajua sasa ndio lala salama yake; juzi yeye na nduguye Masaburi wamepigwa chini kwenye uchaguzi wa Nec ;sidhani kama atagombea ubunge tena kwani upepo unaovuma sio mzuri kwake!! Ajiandae kuuza baa aliyojenga hapo kwenye open space ya wananchi.
 
Back
Top Bottom