Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea

Status
Not open for further replies.
Magamba tumewapiga 4 by 1 kumbuka majimbo ya sumbawanga,meatu,singida na biharamulo.Na leo mahanga lazma ma ..Vi yake yatagonga chuup..I
 
Sasa Mkuu kama umeshafika mahakamani si uanze kuleta updates?! Najua mahakama haijaanza lakini ukituelezea hali ya uwanja ilivyo hapo nje itapendeza! Maana tulisikia jamaa anahamasisha watu kuja kushangilia. Hali ya uwanja muhimu mkuu, waamuzi na washika vibendera (Polisisiem) wanaonekanaje?
 
Magamba tumewapiga 4 by 1 kumbuka majimbo ya sumbawanga,meatu,singida na biharamulo.Na leo mahanga lazma ma ..Vi yake yatagonga chuup..I

Mchumipesa,Kesi ya Meatu bado haijatolewa uamuzi mpaka tarehe 4/5/2012 lakini magamba watalia tu!
 
Ndo tunatokea maeneo ya segerea tunaelekea mahakamani kusiliza hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wa makongoro kama kawahida simu yangu hiko full chagi full vocha kwa maupdate ya kufa mtu karibuni
---------UPDATE---------
Watu ni wengi sana waoelekea mahakamani
Still tune
 
Wakuu aliyepo mahakamani ajipambanue ili tuwe na source tunayoitegemea....
 
Wanabodi,

Hukumu hii inatarajiwa kuanza kusomwa muda wa saa 4 kamili asubuhi ya leo.Pamoja na madai mbalimbali yaliyowasilishwa na mdai akiwakilishwa na wakili Peter P. Kibatala wa Trustmark Attoneys, hapa chini nibaadhi ya hoja za upande wa mlalamikaji:

1. Msimamizi Wa Uchaguzi alitangaza matokeo pasipo kujumuisha vituo 120 vya Kiwalani, 129 Vingunguti, 4 buguruni, 2, Tabata na 4 Kipawa

2. Vituo tajwa hapo juu, havikufanya mahesabu na majumuisho ya uhesabu wa kura (Fomu 21B)

3. Fomu ya kurekodi matokeo (21B) hazikusambazwa katika baadhi ya vituo na hivyo kuwafanya wahusika kuweka matokeo kwa kutumia karatasi za kawaida(plain papers) ambazo ni rahisi kufanyiwa forgery na ubaya wowote.

4. Afisa Mtendaji Kata ya Tabata - Imelda Kafanabo – alikamatwa na fomu batili zenye matokeo yasiyo halali (ushahidi wa video uliambatanishwa)

5. Mwananchi mwingine alikamatwa Anatoglu akiwa na fomu na mihuri isivyo halali ikiwa imempa(video iliambatanishwa ikimwonyesha mtuhumiwa akikamatwa)


6. Maboksi ya kuhesabia kura kutoka Kata ya Buguruni yenye namba 15134, 151305, 151083, 15144, 15109, 15129, 151302 yalikuwatwa yakiwa wazi, hayana lakiri.

7.
Mdai akiwa na wagombea wenzake wa Civic United Front (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) walitoa malalamiko ya mdomo kuhusu kukosekana kwa kura kutoka kata za Vingunguti, Buguruni na Kiwalani. Pamoja na mapungufu hayo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo kwa kusema kwamba "ameamriwa kutangaza matokeo mpaka kufikia saa 8 mchana siku ya tarehe 03/11/2010" na aliwakataliwa wadai fursa ya kuweka madai yao kwa maandishi.

8. Mahesabu ya kura kutoka katika vituo yalionyesha Mpendazoe kupata kura 56,962 na Mahanga 44,904.
 
Ndo tunatokea maeneo ya segerea tunaelekea mahakamani kusiliza hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wa makongoro kama kawahida simu yangu hiko full chagi full vocha kwa maupdate ya kufa mtu karibuni

simu aina gani?
usijesingizia umebanwa na manjagu,
enewei, nakutakia kila la heri, utupe mauhondo direct kutoka mh. jaji.
 
Wanabodi,
Hukumu hii inatarajiwa kuanza kusomwa muda wa saa 4 kamili asubuhi ya leo.Pamoja na madai mbalimbali yaliyowasilishwa na mdai akiwakilishwa na wakili Peter P. Kibatala wa Trustmark Attoneys, hapa chini nibaadhi ya hoja za upande wa mlalamikaji:

1. Msimamizi Wa Uchaguzi alitangaza matokeo pasipo kujumuisha vituo 120 vya Kiwalani, 129 Vingunguti, 4 buguruni, 2, Tabata na 4 Kipawa2. Vituo tajwa hapo juu, havikufanya mahesabu na majumuisho ya uhesabu wa kura (Fomu 21B)3. Fomu ya kurekodi matokeo (21B) hazikusambazwa katika baadhi ya vituo na hivyo kuwafanya wahusika kuweka matokeo kwa kutumia karatasi za kawaida(plain papers) ambazo ni rahisi kufanyiwa forgery na ubaya wowote. 4. Afisa Mtendaji Kata ya Tabata - Imelda Kafanabo – alikamatwa na fomu batili zenye matokeo yasiyo halali (ushahidi wa video uliambatanishwa) 5. Mwananchi mwingine alikamatwa Anatoglu akiwa na fomu na mihuri isivyo halali ikiwa imempa(video iliambatanishwa ikimwonyesha mtuhumiwa akikamatwa)
6. Maboksi ya kuhesabia kura kutoka Kata ya Buguruni yenye namba 15134, 151305, 151083, 15144, 15109, 15129, 151302 yalikuwatwa yakiwa wazi, hayana lakiri. 7. Mdai akiwa na wagombea wenzake wa Civic United Front (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) walitoa malalamiko ya mdomo kuhusu kukosekana kwa kura kutoka kata za Vingunguti, Buguruni na Kiwalani.Pamoja na mapungufu hayo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo kwa kusema kwamba "ameamriwa kutangaza matokeo mpaka kufikia saa 8 mchana siku ya tarehe 03/11/2010" na aliwakataliwa wadai fursa ya kuweka madai yao kwa maandishi. 8. Mahesabu ya kura kutoka katika vituo yalionyesha Mpendazoe kupata kura 56,962 na Mahanga 44,904.

Kitu kinagonga!Sioni Dr.Mahanga atatokea mlango gani, labda ayeyuke kama barafu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom