Makonda: Zitto ndiye mwanasiasa makini kwa upinzani

Nami naungana na mhe. Makonda hakuna kama Zitto ktk siasa za upinzani huyu jamaa ni jembe kama hamuamini ngoja october ifike Act itakapofanya vema ndio mtaamini kama Zitto jembe.

Huyu naye hayo majembe mwisho sijui yatalima wapi???""
 
Majanga makonda katoka nche ya mstari, siasemetu mwana CCM mwezangu ninae mkubari zaidi zitto? Kwani zitto nae nimpizani? Mbona ndo walewale kwenye kapu moja LA CCM?
 
Wakati akiwa mpinzani wa kweli hakuwa mwanasiasa makini,wameshamuweka mfukoni amekuwa mwanasiasa makini wa upinzani.
 
namkubali sana zito kua ni miongoni mwa wapinzani wa dhati sana lakini kauli ua ubora wake nahisi imetoka kwenye mdomo si sahihi wa huyu jamaa ambaye ni plural ya konda
 
Hiv jaman tukiacha ushabik. Hiv unaweza kumlinganisha zitto na Lema, mbowe au slaa kwa hoja? Zitto ni moto wa kuotea mbali.
 
Namnukuu alisema hivi "Ukichanganya vyama vyote, na wanasiasa wote wa upinzani pamoja na viongozi wao kwa umoja wao hawamfikii zito kabwe, wanatakiwa wakae chini awafundishe siasa" mwisho wa kunukuu

Kama alisema kiushabiki hivi hakika alikuwa na mahaba yake binafsi, ila muulize Riz na Zitto nani anaijua siasa vyema? Atakuambia Riz…!! Apo ndipo utajua kuwa Makonda kichwa maji
 
Wanaosemaga Zitto ni Pro-CCM huwa nawashangaa sana. Mtu aliyeisumbua serikali ya CCM kwa uwazi bila kificho na kusababisha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri mara kwa mara ni CCM?

Mtu anayesaidiana na wenzake kwa kila hali kuibua ufisadi wa serikali ya CCM anawezaje kuwa CCM? Mtu anayekosoa mipango na ubovu wa mikataba ya serikali na kuanika uozo ni anakuaje CCM?

Kama ni kweli anatumiwa na CCM, Sasa pale CCM anafanya kazi gani?

Au mimi ndio sielewi mambo yanavyoenda? duh!

Hizo ndizo tabia za wanafiki.Usidhani yeye ni mjinga atumikie ccm direct.Zitto ni agent wa ccm na kazi hiyo huifanya kwa ustadi mkubwa.
 
Ukitaka popojo bavicha wajikojolee waambie Zitto ndiye mpinzani makini toka upinzani, wengine wote ma-dj, watangaza injili na maharamia wa silaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom