Makonda uadilifu ameanza lini?

Makonda uadilifu ameanza lini?

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,172
Reaction score
48,689
Habari!

Nami leo nimeona nitie neno juu ya Paul Makonda. Huyu jamaa Mimi simwiti mheshimiwa. Hata kama atakuwa Rais kwa mifumo yetu bado nitamwita Rais Makonda sitaweka neno Mh.

Makonda akiwa kwenye ukuu wa mkoa ndani ya mwaka mmoja na nusu tayari alikuwa na utajiri usiopimika mpaka kuweza kumzawadia mke wake gari ya zaidi ya sh. Million 200 za Tanzania ilhali hakuwa mfanyabiashara awali kwamba tungesema pesa alizipata kwenye biashara zake.

Makonda akiwa RC Dar es salaam alipata kashfa ya blackmail na kujipatia majumba na magari ya fahari.

Makonda alipata kashfa ya kupitisha mzigo bandarini na kutaka kukwepa kodi ya billioni 2. Na kati ya zile Mali zipo za watu wengine na zake mwenyewe, hapo maana yake nini?

Maana yake watu walikuwa wakimpa pesa kama tozo yeye mifukoni kwake kisha kurahisishiwa mipango yao.

Tuhuma zote alizotuhumiwa yakuwahi kutoa ufafanuzi wa maana mpaka leo zaidi ya kuwalaani wanaomfuatilia .
Issue ya vyeti feki pia hajaijibia mpaka kesho.

Kichaka cha haya yote anajificha kwenye neno kuchapa kazi.

Kuna madaktari walikuwa wapo vizuri kazini, module zote wako njema ila cheti cha form 4 kiliwang'oa.

Kwahiyo jinai yoyote haisafishwi kwa
kuchapa kazi.

Issue ya USA kumtuhumu kuua watu (kudhulumu haki ya kuishi) hajawahi kuipinga kwa hoja.

Huyu Makonda mnayemsifia na kumtukuza ni lini ameanza uadilifu?

Mahakama wamempigania sana asichafuliwe jina baadaye kapata cheo akaanza kuwatukana watumishi wa mahakama. Hili lilinipa furaha maana hao mahakama walimlea wenyewe akawanyea mavi kiganjani.
 
ninachojua pesa ni sabuni ya roho uipate kwa udanganyifu au kwa halali...... tusimlaumu jamaa maana hata sisi wengi wetu tungepata hizo nafasi ni ngumu kufumba macho na kuacha pesa.... tuendelee kuibiana mwenye nacho aongezewe maskini abaki na watoto wake wapauke kama misukule
 
Makonda akili kubwa , Ukiwa na kichwa maji lazima utamjadili juu juu.

Ngoja nikuulize, Makonda anapata wapi Hela za kuzawadia Pikipiki Jeshi la Polisi, Magari??

Kwahiyo nahilo unasema ni wizi ? Udhulumaji?.

Kuhusu Marekan, ni Kwa sababu ya Makonda kupambana na mashogam..wee ni shoga?.
 
Acha uongo
 
Haya uliyoandika unaweza kuyathibitisha kwenye court of law mbali na humu JF ambako unaweza kuandika chochote ilimradi una bandle?

Maana nakumbuka kuna bwana mmoja anakaa ughaibuni aliweka mawakili wasomi waendeshe kesi yake ya kudhulumiwa gari na Mwamba Makonda, halafu kesi ilipoanza jamaa akaingia mitini hataki tena kiwasiliana na mawakili wasomi wake! Ahahahahaha!!!
 
Kuna wanaomchukia kwa sababu zao binafsi kabisa na kuna wale wanaosikia tu kwamba fulani mwizi nao wanaunga tu bila kuwa na uelewa (hawa ni wengi)

Hata ikitokea wakaitwa mahakamani kuthibitisha unaona wanaanza kulia na mwisho kusema familia inanitegemea.

Haya mambo unatakiwa kuwa na akili ya kuchambua siyo kukimbilia tu kisa nasoma kwamba aliiba gari ya mtu.

Je, ni wangapi wanafanya ufisadi mkubwa na bado wanatesa kwa zamu?.
 
Hivi hakuna ndugu wa watu waliodhulumiwa na Makonda wakampeleka mahakamani?,
Hakuna watu waliotendewa huo ubaya na Makonda wakampeleka mahakamani.

Kwanini wapinzani wasishinikize na familia za wahanga + wahanga wenyewe Serikali ikaanzisha uchunguzi dhidi yake?

Watu wa haki za binadamu hawapo Tanzania wakashinikiza Serikali ianzishe uchunguzi dhidi yake, au kuitisha wahanga na kufungua kesi.

Hivi hakuna wanasheria wanaoweza kukusanya evidence na sign za wahanga wakamburuza mahakamani au wakaiomba mahakama itoe amri kwa Serikali kuanzisha uchunguzi dhidi yake?.

Tunasemasema sana, ushahidi hatuleti, hatua hatuchukui basi taflani tu.
 
Je ukiambiwa hizo pesa ni za urithi baada ya kuuza mashamba makubwa ya tumbaku kule Tabora aliyoachiwa na Marehemu Baba yake Brigedia Jenerali mstaafu Bashite.
Utaanzishwa uchunguzi wa kina kama kuna Brigedia aliwahi kumiliki hizo mali kwa kutumia wapelelezi binafsi kujua Aa na Chee!
 
Makonda akili kubwa , Ukiwa na kichwa maji lazima utamjadili juu juu.

Ngoja nikuulize, Makonda anapata wapi Hela za kuzawadia Pikipiki Jeshi la Polisi, Magari??

Kwahiyo nahilo unasema ni wizi ? Udhulumaji?.

Kuhusu Marekan, ni Kwa sababu ya Makonda kupambana na mashogam..wee ni shoga?.
👎👎👎👎👎👎👎
 
Umejibu kiwepesi Mkuu. Kiufupi ejibu kikasuku. Mtoa mada anataka kujua kivipi kijana mdogo hasiye na biashara kubwa RC ndani ya muda mfupi aweze kununua gari la 200M, amiliki jumba la bilioni? Kuna mfanya biashara anaweza kukupa bilioni bila kutegemea fadhila na kulindwa?.

Je mtu akisema aliwabana wauza unga ili timu yake pekee ndiyo iuze then awe anapata mgao unaomuwezesha kumiliki utajiri huo utabisha?.Au hiyo ndiyo akili kubwa yenyewe?.
 
Back
Top Bottom