Makonda: Rais Samia ameagiza Ujenzi wa Shule 56 za Kukuza Vipaji vya Watoto

Makonda: Rais Samia ameagiza Ujenzi wa Shule 56 za Kukuza Vipaji vya Watoto

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Rais Samia Suluhu ameagiza kujengwa kwa shule mpya 56 za kukuza vipaji vya Watoto ili waandalie na wakidhi vigezo na masharti yanayotakiwa kwenye kununuliwa au kusajiliwa na Timu kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema hayo leo Februari 9, 2026 wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam.

“Mkakati wa Wizara chini ya maelekezo ya Samia, kwanza tunaanza ujenzi wa shule za mfano 56 ambazo kwa awamu ya kwanza tutajenga shule 7 ambazo zitakuwa maalum kwa ajili ya kukuza na kutengeeneza fursa ya Watoto wenye vipaji kuandaliwa katika umri wa mdogo ili wakidhiti vigezo na masharti yanayotakiwa kwenye kununuliwa au kusajiliwa na Timu kubwa”

“Tunao mpango pia kama Wizara tuanze na Halmashauri 20 ambazo zitaweza kujenga viwanja na kujenga shule au centre za kukuza vipaji vya Watoto, mfano mathalani tupo Temeke alipotoka Samatta ila kwanini Temeke isiwe na shule ya awali ya kukuza vipaji vya Watoto ili club kubwa zije kununua Wachezaji”

Aidha, ameongeza kuwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kamati ya Utendaji ya CAF utafanyika hapa Tanzania tarehe 13 Februari 2026 katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam, ambapo utaongozwa na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe.

Nafikiri team za mipira ndio zingekuwa zinawafundisha mipira watoto kwa siku maalum kama weekend na wakati wa likizo.

Na huko ndio watawaona watoto wenye uwezo mkubwa wa kucheza.
Lakini kujenga shule ni kupoteza pesa tu.
 
Ni wazo zuri, vipaji vikuzwe lakini vijana wawe na shuke kichwani, shida yetu kubwa ni siasa.. jambo hili litaingia siasa, pesa zitaliwa, kazi kwa kujuana hata kama mtu hana sifa.. mwishowe jambo linakufa kibudu
 
Nafikiri team za mipira ndio zingekuwa zinawafundisha mipira watoto kwa siku maalum kama weekend na wakati wa likizo.

Na huko ndio watawaona watoto wenye uwezo mkubwa wa kucheza.
Lakini kujenga shule ni kupoteza pesa tu.
Niliwahi sema hiki kitu, hata huko academy, walimu na wakufunzi wawe wachezaji halisi, iwe wa zamani au sasa.
 
SHENZI KABISA.
VIWANJA VIWILI TU VYA AFCON VIMEWASHINDA WANAKUJA KUWADANGANYA KUHUSU SHULE

PUMBAVU KABISA
 
Yan hii nchi haijulikan kama tunaenda mbele au tunarudi nyuma,
Je hapo hawali hizi shule hazikuwepo?
Kipi kilichopelekea hizo shule kupotea?
Kiufupi tunafanya mambo kitoto zaid
 
Hii ni kwa nchi yoyote wangejipanga naamini wangeanza na

Kukuza hayo kwa shule zilizopo kwanza, kwa kuanzia kuziboresha na mengineyo kufata.. Pesa iliyopangwa na kubaki yaweza fanya mengi mazuri zaidi
 
Kwani kwanini wasirekebishe sera ya michezo ili kuvilazimisha vilabu viwe na academy zao na pia kuwe na ligi ya academy kama ilivo ulaya kuliko kuja tena kujenga shule mpya hiyo bajeti si waziwezeshe tu team zote madaraja yote mfano wakipewa bilion 10 kila msimu si wataweza kuhudumia hao watoto.
 
Nafikiri team za mipira ndio zingekuwa zinawafundisha mipira watoto kwa siku maalum kama weekend na wakati wa likizo.

Na huko ndio watawaona watoto wenye uwezo mkubwa wa kucheza.
Lakini kujenga shule ni kupoteza pesa tu.

Niliwahi sema hiki kitu, hata huko academy, walimu na wakufunzi wawe wachezaji halisi, iwe wa zamani au sasa.

Kwani kwanini wasirekebishe sera ya michezo ili kuvilazimisha vilabu viwe na academy zao na pia kuwe na ligi ya academy kama ilivo ulaya kuliko kuja tena kujenga shule mpya hiyo bajeti si waziwezeshe tu team zote madaraja yote mfano wakipewa bilion 10 kila msimu si wataweza kuhudumia hao watoto.
Serikali na yenyewe ina wivu mnapovisifia vilabu ndiyo maana huwa wanalazimisha kujipenyeza katika hivyo vilabu vinapoanza kufanya vizuri.

Hawataki kufanya program hii kupitia vilabu kwa sababu hamtawapa wao sifa.

Kiuhalisia hii program inapaswa isimamiwe na kuendeshwa na TFF kwa kushirikiana na vilabu. TFF kupata pesa za CAF na FIFA na kuendesha kwa ufanisi zaidi ni rahisi kuliko kufanya kupitia ukiritimba wa kiserikali.

Tumekuwa na wazo la kijiji cha michezo kwa miaka mingapi sasa? UMISETA na UMITASHUMTA ziko wapi na zinachangiaje maendeleo ya michezo?

Kuhusu michezo mashuleni, ingekuwa bora zaidi kujenga kituo cha michezo katika ngazi ya kata au wilaya na shule za eneo hilo zitumie pamoja facilities hizo. Niliwahi kusema hata uwanja wa KMC una hadhi ya matumizi kama hayo.
 
Binafsi maswala ya michezo ni jambo ambalo mtu unafanya shule ikikataa.

Dunia bila elimu utachapika mno.
 
Huwezi amini huyu kijana wazazi wake wana asili ya bongo

Malik Hashi

1770681703582.png
 
Back
Top Bottom