Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,497
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, ametangaza mpango wa kumuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kiasi cha hadi Shilingi bilioni mbili kwa ajili ya mikopo ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya vijana waliojiajiri kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni na mitandao ya kijamii.
Akizungumza leo, Januari 13, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi, Makonda amesema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha vijana kumiliki kamera na kompyuta za kisasa ili kutoa maudhui yenye ubora wa kimataifa yanayoitangaza Tanzania vizuri badala ya kutegemea vifaa duni.
Pamoja na uwezeshaji huo, Waziri Makonda ametangaza mkakati mpya wa kuanzisha timu maalum ndani ya wizara itakayoshughulika na mawasiliano ya lugha mbalimbali za kimataifa. Lengo ni kuhakikisha kuwa habari na matukio ya Rais Samia na Serikali yanarushwa na vyombo vikubwa vya habari duniani kwa ufanisi zaidi.