GE2025 Makonda: Nikiingia bungeni moto utawaka, nitapiga spana watu mpaka kitaeleweka

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema endapo atashinda uchaguzi na kuingia bungeni, ataweka nguvu kubwa katika kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030.

Makonda amesema anatarajia kutumia nafasi hiyo kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa serikalini na vijana wa Tanzania wananufaika na matunda ya maendeleo yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.

“Niwahakikishie kule bungeni moto utawaka, nitapiga spana watu mpaka kitaeleweka. Tunataka haki na kila mtu awajibike kwa nafasi yake ili kila kijana wa Tanzania afurahie matunda ya Taifa lake,” amesema Makonda Jumatano, Oktoba 9, 2025, alipokuwa akizungumza na wakazi wa Lamadi, mkoani Simiyu.
Your browser is not able to display this video.
 
Kama spana zako hazita husu kupatikana waliotekwa na kupotezwa haina hata sababu ya kujibebesha maspana!
 
Atawapiga spana wasiojulikana wake ili tupate haki?
 
Mtu mwenyewe ni snitch! Sasa hizo spana atampiga nani, na wakati muda wote atakuwa awaza tu namna ya kuwachongea wenzake kwa Bosi wao Bi Khadija Kopa!
 
1. Passive
2. Msigwa
Vijana wa hovyo tena hovyo ila Mungu yupo ipo siku na si nyingi watahesabiwa tu
 
Fisiemu wakiwa nje ya mfumo wanakuwaga kama nakondoo tu pumbav zao, ila wakirudi kwenye mfumo wanageuka kuwa chui.

Huyu Makonda nakumbuka mwaka 2021 December nilikuwa namuona sana pale Bonasera Karibu na chuo cha Bank kuu, Mwanza... jamaa alikuwa mpole sana kwanzia mwili mpaka sauti alikuwa amebadilika sana, yaan alikuwa kama kondoo.

Ila sasa hivi amerudi kuwa makonda yule tuliyekuwa tumemzoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…