screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,926
- 15,982
MsemajiUkweli kwahiyo TIss ndio wamemkataza Bashite kuweka vyeti mezani?
Kuna kamwimbo nakasikiaga kwenye harusi za wangoniYoooote haya kisa, bashite hataki kuonyesha vyeti
"Kitengo" ilikuwa zamani, sasa hivi hakuna kitu twendeni hivyo hivyo mlivyoamua muda utamalizika watakuja wengine maisha yaendelee! Eti mpaka watu wa "kitengo" watakapojiridhisha kuwa kazi waliyomtuma Bashite ameshindwa kuifanya au makosa anayoyafanya ni makubwa ...". Hebu acheni propaganda zenu mfu za kutaka kuaminisha umma kwamba Bashite anafanya kazi za "kitengo" . Hivi hamuoni kuwa mnazidi kuivua nguo serikali? Mkamateni Bashite mmpeleke mahakamani kwa kosa la udanganyifu wa elimu, acheni blah blah na waacheni wananchi wapumue jamani!Kuna habari zilizoko chini ya viunga vya watawala zinasema watu wa ‘’kitengo’’ wameamua kulifanyia kazi suala la Mchungaji Gwajima, Clouds Media International na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa sababu halitoi afya njema kisiasa.
Kwa kifupi, ‘’kitengo’’ ni neno ambalo kwa kiingereza ni ‘’The ruling class/The Establishment’’. Hawa ni watu ambao moja ya kazi zao ni kutathmini kwa kina hali ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi nchini halafu baadaye hutoa mwelekeo kwa taasisi zinazohusika.
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hatutaweza kumsikia tena Mchungaji Gwajima akimzodoa Makonda katika mahubiri yake kanisani.
Ieleweke kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika, watu wa ‘’kitengo’’ walifanya tathmini na kubainisha watu ambayo wataweza kufanikisha mikakati ya kisiasa kwa CCM na kiuchumi kwa serikali katika mikoa ambayo inaonekana ni muhimu sana kisiasa na kiuchumi. Mikoa hiyo muhimu sana ilipelekewa viongozi ambao watafanikisha mikakati hiyo na mojawapo ni Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa wale wanadhani Makonda ataondolewa hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam, nadhani wataendelea kusubiri sana mpaka pale watu wa ‘’kitengo’’ watakapo jiridhisha kuwa kazi waliyomtuma ameshindwa kuifanya au makosa anayofanya ni makubwa kiasi kwamba yanaondoa hata madhumuni makuu ya uwepo wake kama Mkuu wa Mkoa.
Nimalizie kwa kusema, Mkuu wa taasisi ya watu wenye ‘’suti nyeusi’’ ametoa onyo kali kwa vijana wake kwa yaliyotokea Clouds Media International na kwa Nape Nnauye kwa sababu kazi waliyopewa ni kumlinda Mkuu wa Mkoa na sio yeye Mkuu wa Mkoa awape kazi za kufanya nje ya misingi yao ya kazi. Ieleweke kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kiulinzi ilibainika Makonda anatakiwa kuboreshewa ulinzi.
Msishangae sana kwa nini Nape Nnauye ameamua kuwa kimya kuhusiana na kadhia ya kutishiwa bastola. Ameelezwa ukweli wa hali halisi iliyopelekea kitendo hicho kutokea.
Mjumbe hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!
ssa kwanni wasifanye maamuzi kwa maslahi ya taifa??? je uwizi kma ule bandarini kitengo hicho hawakuuona??? mikataba mibovu ya TPDC hao kitengo hawaionagi?? au wao wanaona tu ccm ikimkandamiza ukawa
Mungu ibaliki Tanzaniawanatumia pesa nyingi ili wamulinde bashite. Sisi wananchi hatuchoki tutatumia hii mitandao (kabla malaika hajashuka kuifunga) kumsema basit maana bunge limeshindwa.
Kwa akili ya kawaida ndalichako yupo sawa? Je anaweza kusimamia aliyayasema? Au analinda ugari asitumbuliwe? Kama kweli basi elimu yake naiona kama ya darasa la saba,
wana matamko ya kunyanyasa wanyonge na vyeti fake bashite anakumbatiwa.
Hili la bashite lingemkuta mpinzani tungeona kila rangi
hivi huyu bashite ana kitu gani "special" ambacho serikali hadi bunge wako kimya?
Hivi inachukua dakika ngapi mtu kuonesha vyeti?
Wanapoteza mda mara kamati ya bunge wakae hizo pesa wanapoteza za nn si mtu aoneshe vyeti mambo yaishe?? Hata kama ni kuogopa "not to that extent"
Madhumuni ya Chama chochote cha kisiasa ambacho sio cha kisanii huwa ni kushika dola. Chama makini kinaposhika dola hakiwezi kuruhusu kishindwe kwa njia za kivivu vivu.ujinga uleule..pale ambapo hao watu wataacha kuifanyia kazi ccm na kuanza kuifanyia kazi nchi...ndipo nchi hii itabadilika.
Tiss inapaswa kutoshiriki kwenye shughuli zinazohusu masuala ya chama cha CCM
Hakuna wapi?Unaambiwa Hakuna jina Bashite
Gwajima kalitoa wapi
Madhumuni ya Chama chochote cha kisiasa ambacho sio cha kisanii huwa ni kushika dola. Chama makini kinaposhika dola hakiwezi kuruhusu kishindwe kwa njia za kivivu vivu.
CCM imetawala kwa muda mrefu katika mazingira ya siasa za nchi za Afrika sio by default bali kwa uwezo wa kuunganisha chama na dola. Siku ambayo chama na dola vitatengana ndio siku ambayo CCM itaondoka madarakani.
Kwa maana nyingine, CCM is ruling state party.
Huu ndio ukweli halisi pamoja na kwamba ni ukweli mchungu kwa wapinzani!