Makonda na Mchungaji Gwajima kupatanishwa!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Kuna habari zilizoko chini ya viunga vya watawala zinasema watu wa ‘’kitengo’’ wameamua kulifanyia kazi suala la Mchungaji Gwajima, Clouds Media International na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa sababu halitoi afya njema kisiasa.

Kwa kifupi, ‘’kitengo’’ ni neno ambalo kwa kiingereza ni ‘’The ruling class/The Establishment’’. Hawa ni watu ambao moja ya kazi zao ni kutathmini kwa kina hali ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi nchini halafu baadaye hutoa mwelekeo kwa taasisi zinazohusika.

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hatutaweza kumsikia tena Mchungaji Gwajima akimzodoa Makonda katika mahubiri yake kanisani.

Ieleweke kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika, watu wa ‘’kitengo’’ walifanya tathmini na kubainisha watu ambayo wataweza kufanikisha mikakati ya kisiasa kwa CCM na kiuchumi kwa serikali katika mikoa ambayo inaonekana ni muhimu sana kisiasa na kiuchumi. Mikoa hiyo muhimu sana ilipelekewa viongozi ambao watafanikisha mikakati hiyo na mojawapo ni Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa wale wanadhani Makonda ataondolewa hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam, nadhani wataendelea kusubiri sana mpaka pale watu wa ‘’kitengo’’ watakapo jiridhisha kuwa kazi waliyomtuma ameshindwa kuifanya au makosa anayofanya ni makubwa kiasi kwamba yanaondoa hata madhumuni makuu ya uwepo wake kama Mkuu wa Mkoa.

Nimalizie kwa kusema, Mkuu wa taasisi ya watu wenye ‘’suti nyeusi’’ ametoa onyo kali kwa vijana wake kwa yaliyotokea Clouds Media International na kwa Nape Nnauye kwa sababu kazi waliyopewa ni kumlinda Mkuu wa Mkoa na sio yeye Mkuu wa Mkoa awape kazi za kufanya nje ya misingi yao ya kazi. Ieleweke kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kiulinzi ilibainika Makonda anatakiwa kuboreshewa ulinzi.

Msishangae sana kwa nini Nape Nnauye ameamua kuwa kimya kuhusiana na kadhia ya kutishiwa bastola. Ameelezwa ukweli wa hali halisi iliyopelekea kitendo hicho kutokea.

Mjumbe hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!
 

They were Together Once but Anymore
d11490b7c5db12bc.png
 
Kitengo... a.k.a system. Nawakubali sana jamaa... yaan president pale ni kama geresha tu lakin nyuma yake kuna watu wanaofanya maamuzi
 
Akitoa vyeti sawa,
La sivyo hata hao wapatanishi watatolewa nduki na Gwajima...
 
Kitengo... a.k.a system. Nawakubali sana jamaa... yaan president pale ni kama geresha tu lakin nyuma yake kuna watu wanaofanya maamuzi
ssa kwanni wasifanye maamuzi kwa maslahi ya taifa??? je uwizi kma ule bandarini kitengo hicho hawakuuona??? mikataba mibovu ya TPDC hao kitengo hawaionagi?? au wao wanaona tu ccm ikimkandamiza ukawa
 
Kitengo ni muhimu sana kwa ustawi na ukuaji wa taifa letu.

Kila nchi ina kitengo na moja ya majukumu yake ni hilo, kuhakikisha ustawi salama wenye tija na manufaa kwa kila mtanzania na taifa kwa ujumla.
 
Gwajima kesha maliza kazi yake,sisi wengine tutamsulubu mpaka akombie na hao kitengo ni mabashite wengine,wanawezaje kumpa kazi kilaza?

#mungu_wa_daresalamu onyesha vyeti
 
Back
Top Bottom