Makonda na Mchungaji Gwajima kupatanishwa!

Makonda na Mchungaji Gwajima kupatanishwa!

Kwa chizi hata akiumbwa upya atabaki na element zilezile. Nawasilisha. Tatizo tz kila taasisi zinafanya kazi kisiasa. Kweli nimeamini ukistaajabu ya musa utakutana na filauni ahaaaaa nimesahau utayaona ya filauni
 
Elimu tz sio kipaumbele kabisaaaa ila ubabe na dharau kwa wanyonge ndo kipaumbele. Ikumbukwe kuwa mfalme Sulemani alishindwa kuomba Mali bali akaona aombe HEKIMA NA BUSARA ambapo kizazi hiki hilo nalo kwa tz hatuna sasa kama elimu sio kigezo basi Busara na Mdogo wake Hekima vitusaidie bado tumeshindwa. Mhhhh Mungu sasa tumwachie maana huenda kachukua maarifa na kutuachia fuvu
 
Bashite atoe vyeti tena apelekwe jela kabisa. Kama ameshindwa ligi na Gwajima shauri yake, Gwajima sio NECTA.
 
Kuna habari zilizoko chini ya viunga vya watawala zinasema watu wa ‘’kitengo’’ wameamua kulifanyia kazi suala la Mchungaji Gwajima, Clouds Media International na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa sababu halitoi afya njema kisiasa.

Kwa kifupi, ‘’kitengo’’ ni neno ambalo kwa kiingereza ni ‘’The ruling class/The Establishment’’. Hawa ni watu ambao moja ya kazi zao ni kutathmini kwa kina hali ya kisiasa, kiuchumi na kiulinzi nchini halafu baadaye hutoa mwelekeo kwa taasisi zinazohusika.

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hatutaweza kumsikia tena Mchungaji Gwajima akimzodoa Makonda katika mahubiri yake kanisani.

Ieleweke kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 kumalizika, watu wa ‘’kitengo’’ walifanya tathmini na kubainisha watu ambayo wataweza kufanikisha mikakati ya kisiasa kwa CCM na kiuchumi kwa serikali katika mikoa ambayo inaonekana ni muhimu sana kisiasa na kiuchumi. Mikoa hiyo muhimu sana ilipelekewa viongozi ambao watafanikisha mikakati hiyo na mojawapo ni Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa wale wanadhani Makonda ataondolewa hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam, nadhani wataendelea kusubiri sana mpaka pale watu wa ‘’kitengo’’ watakapo jiridhisha kuwa kazi waliyomtuma ameshindwa kuifanya au makosa anayofanya ni makubwa kiasi kwamba yanaondoa hata madhumuni makuu ya uwepo wake kama Mkuu wa Mkoa.

Nimalizie kwa kusema, Mkuu wa taasisi ya watu wenye ‘’suti nyeusi’’ ametoa onyo kali kwa vijana wake kwa yaliyotokea Clouds Media International na kwa Nape Nnauye kwa sababu kazi waliyopewa ni kumlinda Mkuu wa Mkoa na sio yeye Mkuu wa Mkoa awape kazi za kufanya nje ya misingi yao ya kazi. Ieleweke kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina kiulinzi ilibainika Makonda anatakiwa kuboreshewa ulinzi.

Msishangae sana kwa nini Nape Nnauye ameamua kuwa kimya kuhusiana na kadhia ya kutishiwa bastola. Ameelezwa ukweli wa hali halisi iliyopelekea kitendo hicho kutokea.

Mjumbe hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!
Gwajima aliahidi kunyamaza tangu mapema tu in case hachokozwi.

Kwahiyo kupiga ramli eti kuna uwezekano asiongee ni kujifurahisha tu.

Mwenyewe ashasema hatazungumza mpaka akichokozwa
 
Gwajima aliahidi kunyamaza tangu mapema tu in case hachokozwi.

Kwahiyo kupiga ramli eti kuna uwezekano asiongee ni kujifurahisha tu.

Mwenyewe ashasema hatazungumza mpaka akichokozwa
Mleta mada huenda ni mmoja wa hao anaowaita kitengo, na ameanzisha mjadala huu kwa makusudi kupima upepo ili watathmini kama kupatanishwa huko kutawezekana au kutaendeleza malumbano.
 
Gwajima uckubali mpaka aonyeshe vyeti Huyo.ss baada yakufikwa shingoni ndo mpatane?nia yake yakutaka udhalilishwe na Clauds imegonga mwamba,ndo anaomba radhi? Dawa ni kuwasuca yy na boss wake waendeshe nchi wawili na kibaraka wao zee la kunywa sumu mwakuembe.
 
kwa nini kitengo hakikumchunguza kabla ya kumpa hiyo kazi...?
ila nimeanza kumuonea huruma Bashite...nilipomuona mbele ya wabunge kwa kweli amenitia huruma...
lakini anawezaje kusamehewa huku wengine wameadhibiwa kwa kosa kama lake la vyeti?!
Tuwasamehe wote tuanze upya...else na yeye achukuliwe hatua staiki...
 
Polished grave though may appear beautiful but will still be a grave.
 
Kitengo ni muhimu sana kwa ustawi na ukuaji wa taifa letu.

Kila nchi ina kitengo na moja ya majukumu yake ni hilo, kuhakikisha ustawi salama wenye tija na manufaa kwa kila mtanzania na taifa kwa ujumla.
kitengo zero kabisa mbona maufisadi mengi yanatokea wenyewe hawajui au hawazuii??? mbona nchi maskini hii hku tunaibiwa kila siku kwa mikatab mibovu hao kitengo wanakuwaga wapi??? kitengo ni muhim ila sio hiki cha tanzania yaani mpaka siku kipiganie maslahi ya tanznaia na sio ccm ndio tutaona maendeleo ya kweli
 
Ni aubu kwa tiss kufanya kazi za chama badala ya taifa wauge mfano
USAambao cia, fbi wanafanya jazu za taifa zima na si kwa republican/demicratic.
Kwani kila chama kinatakiwa kujitegemea kiusalama.
 
Back
Top Bottom