Makonda: Mchaga kusaidia walemavu na yatima ni jambo gumu sana

ZERO BRAIN Mkuu mtu mwenye akili timamu asingeweza kutamka hayo.

Kamalizia Kwa kusema KUBENEA ANADAIWA NA MENGI, ATIMIZE AHADI ILI MZEE ALALE SALAMA.... wallah sikutegemea Makonda atamke aliyoyatamka akiwa msibani.... BUSARA HAIJATUMIKA KABISA KWENYE KUTAMKA ALIYOYATAMKA...
 
Kuna haja ya kuangalia aina ya watu wanaopewa uongozi, sasa haya si maneno ya hekima kwa wachaga waliobaki hai eti kisa unatafta sifa kwa mchaga mmoja aliyekufa
Kaongea jambo la hovyo kabisa,eti 'Mengi ndiye mchaga bora kuliko wote'.Yeye huo ubora wa binadamu wenzie anaupima vp?mwanzoni nilidhani ni jokes tu lakini yupo kakaza sura kabisa anamaanisha.

Sijui waombolezaji wakichaga wamejisikia vp mle ndani aloo.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda akiwa msibani Karimjee Hall amesema hajawai kuona mchaga anasaidia yatima na walemavu isipokuwa Marehemu mzee Mengi.

Amesisitiza Mengi ndo alikuwa mchaga bora.
Makonda kama kasema haya inamaanisha hata historia haijui, aulize waliotoa nauli ya Mwalimu Nyerere kwenda kudai uhuru UN walikua kina nani, ajiulize Ndesa pesa alikua nani, au kina Chief Mareale etc etc na pia akumbuke kuna wachaga wengi tu wanatoa misaada ila hawajitangazi.
Haya sio maneno ya kiongozi kuyasema kwenye msiba, usidhani unawazalilisha wachagga bali unajizalilisha wewe mwenyewe
 
Uzi niandike mimi anapewaje mwingine? Kisa kawahi dakika moja kupost? Kichwa cha habari ni kilekile changu, habari ni ileile yangu yaani bila kupunguza wala kongeza kitu! Kama suala ni kuwahi mngeunganisha uzi wa kwake na sio kuugawa jinsi ulivyo wakati huyo mliomgawia hajaandika hiki na yeye kapost kwa maana yake kwamba 'makonda katukana wachaga'
Maxence Melo Moderator
Wewe nawe unalalamikaga vitu vya kipumbavu kwani ukiwa wa kwanza kuanzisha uzi unapewa nini ?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda akiwa msibani Karimjee Hall amesema hajawai kuona mchaga anasaidia yatima na walemavu isipokuwa Marehemu mzee Mengi.

Amesisitiza Mengi ndo alikuwa mchaga bora.
Haya sasa Bashite endeleeni na operesheni tokomeza Northerners!Nina wasiwasi na kifo chake siyo elimination ili mufanye ushetani na babayo!!?? references Ruge et al
 
Kwani ni mara ya kwanza kwa wana CCM kuwashambulia wachaga? Kinachokushangaza kwa CCM kutajwa ni nini wakati aliyesema maneno hayo ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Darisalama na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM?

CC: kenna
Jaribu kutumia akili japo kidogo, usiwaaibishe wapare wenzio , tumia protocol katika kutafsiri mambo.
 
Jaribu kutumia akili japo kidogo, usiwaaibishe wapare wenzio , tumia protocol katika kutafsiri mambo.
Protocol gani ningetumia. Kwani Makonda siyo Mwana CCM na siyo Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa wa Darisalama na pia si Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM?
 
Back
Top Bottom