Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
62,190
Reaction score
128,243

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Chanzo: Mpekuzi

===========

My take:

Sema chochote kwa Mkuu wa Mkoa
 
Intelijensia ilibaini mashoga 150 wamekaa kikao cha kutaka kumdhuru, ila vyombo vya usalama vimekamata baadhi yao tu, kha! hao walioachwa wameachwa ili waendelee kutoa huduma au? Makonda kuchokoza mashoga ni sawa na kukimbizana na mwendawazimu jalalani, hawa wtu akili zao haziko sawa ujue, umetoa tamko nyamaza acha vyombo vya dola viwakamate kama kuna sheria ya kuwatia hatiani wataenda jela. Dar bado chafu sanaaaa, bora uende kusafisha mitaroni huko kama huna kazi ya kufanya ofisini.
 
Kuna mambo meng muhimu ya kufanya Makonda achana na hayo ya ushoga!

Huo mda alio utumia hapo clouds angeutumia kuutangaza mlima Kilimanjaro angalau, kuliko kuogea mambo ya starehe za watu
 
Kuanzisha vita na mashoga ni kujitafutia balaa. Soon the war will cross the borders into the unkown
Hii vita ilisha wasumbua watu wengi....kwa kifupi.....
1.Bondia maarufu duniani manny pacquiao...
2.Muimbaji maarufu wa reggae Alpha Blondy
Unajua kwa nini haya yanatokea...Sababu kubwa hawa mashoga nyuma yao kuna watu wakubwa ...Hebu fikiri mwanamuziki Elton John ni shoga lakini malkia wa Uingereza alimpa heshima ya Knight Bachelor...na kuwa Sir Elton John....Hivyo basi RC kupambana na watu kama hawa ni dhahiri anapambana na watu asiowajua.
Kwa sasa shetani ndio yuko kazini.DEVILS AT WORK.
USHOGA TUUKATAE KWA NGUVU ZOTE NA KWA GHARAMA YEYOTE.
 
siku nitakayoona wamepelekwa mahakamani hawa washenzi hapo ndio nitayaamini matamko Yake maana anawajua vizuri kabisa na idadi yao kwa nini asiwapeleke mahakamani ?
Hilo neno washenzi limenikumbusha mbali mno mkuu hahahahahahahhahahaha
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Chanzo: Mpekuzi

===========

My take:

Sema chochote kwa Mkuu wa Mkoa
Duh..... Hii kali kuliko.......

Rais wa Mkoa awahofia mashoga kutaka kumuangamiza?

Duh..... Hivi Makonda na vyombo vyake vyote vya dola 'anavyovimiliki' mkoani kwake anaweweseka na mashoga wabwia unga?!

Kweli hii naweza ifananisha na story ya ukubwa wote wa Tembo anavyomuogopa kupita kiasi hata nyuki mmoja tu kupita mbele yake!
 
Mkuu yashakulinaa jicho nini manake nakuona unatoka mapovu sana hahahaha.
Hawa watu ni kuwakataa kwa nguvu zote kwenye jamii yetu naungana na makonda asilimia Mia nyinyi wateteeni tu hili swala ata maandiko matakatifu yanalipinga makonda asikate tamaa hawa watu wanaungwa Na watu wengi pambana ni Vita hii
 
Back
Top Bottom