Ntu Mpyaaa
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 986
- 1,823
Arusha ni mji wa wafanyabiashara huwenda kuliko miji yote Tanzania
Arusha kila mtu ni mfanyabiashara
Arusha wahuni ni wengi saana
Juzi nipo na wazee na viongozi baadhi waandamizi wa CCM mkoa wa Arusha, wengi wanaonesha kukerwa sana na Anayoyafanya Makonda kwa Gambo.
Wazee hawamkubali kabisa kabisa, kwanza anaharibu biashara za watu kila siku anaziba barabara kwaajili ya maslahi yake kisiasa
Bado anaharibu taswira ya chama kwa kuropoka hovyo kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.
Lakini cha muhimu zaidi, tangu aende Arusha hakuna ch maana kilichobadilika Arusha tofauti na Mwanzo
Kiufupi, Makonda ni Mzigo
Ataje hata wazee wawili waandamizi wa CCM aliokutana nao Arusha.Mbona kichwa cha habari ni cha kiume na kina maudhui mazito ila uzi wenyewe hauna hata hoja za msingi?
Mara Arusha ina wafanyabiashara wengi kuliko mkoa wowote,umejaribu kukaa Dar na mwanza?
Halafu mara useme wazee,hao wazee ni akina nani eneo la shughuli za kiserikali au katika maamuzi ya mwisho ya kitaifa?
Jambo lingine,ina maana makonda akikorofishana na Mrisho Gambo ndio amekorofishana na Arusha nzima kwamba hakuna watu wanaomkubali?
Hao watu ni wakabila na hawawezi kuacha ukabila.Ukabila ni mbegu ya chuki achana nayo mkuu.
Sasa kwa taarifa yako wafanyabiashara wakubwa wengi wa hapo Arusha ni wachagaArusha ni mji wa Wamasai na Wameru. Wachaga ni wakuja tu kama Wasukuma na makabila mengine hapo Arusha. Eti Wachaga wa Arusha!!
Mkuu lile soko la Tengeru limejaa tope na vumbi nyie mnaishia kucheza sebene na nyama za bure.wewe sio mkazi wa Arusha ni mbea flani hivi kutoka mikoa ya ukanda wa Magharibi.
Halafu anataka kugombea Ubunge Arusha!Arusha ni mji wa wafanyabiashara huwenda kuliko miji yote Tanzania
Arusha kila mtu ni mfanyabiashara
Arusha wahuni ni wengi saana
Juzi nipo na wazee na viongozi baadhi waandamizi wa CCM mkoa wa Arusha, wengi wanaonesha kukerwa sana na Anayoyafanya Makonda kwa Gambo.
Wazee hawamkubali kabisa kabisa, kwanza anaharibu biashara za watu kila siku anaziba barabara kwaajili ya maslahi yake kisiasa
Bado anaharibu taswira ya chama kwa kuropoka hovyo kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.
Lakini cha muhimu zaidi, tangu aende Arusha hakuna ch maana kilichobadilika Arusha tofauti na Mwanzo
Kiufupi, Makonda ni Mzigo
Kwa takwimu gani? Mbona mnapenda sana kujitutumua?Sasa kwa taarifa yako wafanyabiashara wakubwa wengi wa hapo Arusha ni wachaga
Wazee wa kwenye kilabu cha pombe aina ya chang'aa majina yao tatayafahamu kweli hata akiyataja hapa.Ataje hata wazee wawili waandamizi wa CCM aliokutana nao Arusha.
Vimebadilika vingi barabara nyingi za mjini kati zilikuwa sio one road.Sasa zimekuwa za kupanda au kuteremka na hivyo kupunguza sana matatizo ya jam katika mitaa ya Bondeni,Pangani na Kaloleni.Na nyingi zimeanza kufanyiwa ukarabati.
Jiji limekuwa safi na upandaji wa miti milioni 1 na nusu unaendelea.
Hali ya usalama imeimarika sana ndani ya mwaka mmoja tokea Makonda awe Mkuu wa Mkoa.
Wafanyabiashara hawasumbuliwi na TRA kama ilivyokuwa ada.
Ni wenyewe, ni hati chafu kweli kweli.Huu sio mwandiko wa Gambo kweli?
Project kama ipiWewe ndio mzigo. Wafanyabiashara wa Arusha wanamuunga mkono sana Makonda ndio maana kila project anayofanya anapata michango ya wafanyabiashara. Pia wananchi na ccm wanamkubali sana kuliko huyo Gambo wako
Tusimlaumu sana sio kosa lake, nafikiri unatambua kuwa huo mkoa ndio unaongoza kwa kuwa na vijana wa ajabu ajabu hivyo basi usishangae kuona hata hili bandiko halieleweki kwa sababu hapo zilizoandika ni bangi pamoja na vitoko.Mbona kichwa cha habari ni cha kiume na kina maudhui mazito ila uzi wenyewe hauna hata hoja za msingi?
Mara Arusha ina wafanyabiashara wengi kuliko mkoa wowote,umejaribu kukaa Dar na mwanza?
Halafu mara useme wazee,hao wazee ni akina nani eneo la shughuli za kiserikali au katika maamuzi ya mwisho ya kitaifa?
Jambo lingine,ina maana makonda akikorofishana na Mrisho Gambo ndio amekorofishana na Arusha nzima kwamba hakuna watu wanaomkubali?
Mimi sikuongerea utajiri bali wenyeji wa Arusha. Kama utajiri hata wamasai wapo hapo Arusha matajiri.Sasa ushafuatilia kwa karibu maeneo wanakoishi hao Wamasai na Wameru? Maendeleo mengi ya majengo, na mandhari ya mji wa Arusha yameletwa na wageni!
Kama unabisha nenda Matejoo na Sokoni II.
Acha uongo. Mimi nimekaa Arusha miaka mitano sikuona hiyo difference unayoisema wewe. Nilikuwa naishi hapo maeneo ya Uzunguni karibu na uwanja wa mgambo.Wachaga wakiondoka Arusha kipindi cha mwisho wa mwaka mji unabakigi kama gofu
Labda ww unakaa arusha ya Karatu au ngarenanyuki
Ni hisia zako tu. Kwani huyo unayesema alishinda kimagumashi ni kabila moja na jiwe?Hao watu ni wakabila na hawawezi kuacha ukabila.
Huyo mambo mwenyewe hapo Arusha hakushinda alitangazwa mshindi kimagumashi kwa nguvu ya jiwe .
Wapi nimesema wote walioshinda kimagumashi ni kabila moja na jiweNi hisia zako tu. Kwani huyo unayesema alishinda kimagumashi ni kabila moja na jiwe?